Si kwamba ungeiandika ukaweka gazetini kabisa ndo ungekuwa umetumia hekima zaidi? Kweli unaonekana u mzalendo pekee tanzania, sidhani kama umetafiti ni watanzania wangapi waliofurahia mauaji ya watanzania wengine katika harakati za kutoa maoni yao. Umefurahi sana, na pengine utapandishwa cheo kwa kutoa au kushabikia kutoa uhai wa binadamu mwingine, lakini usisahau damu za hao watu zilizo mwagika na machozi ya wananchi wazalendo zitakufuata wewe na wenzako wote. Ole wako na kizazi chako.Mheshimiwa RPC
Salaam.
Watanzania wote tunafuatilia kwa karibu yanayojiri sasa mjini Arusha.
Tunapenda kukupongeza wewe na vijana wako kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya katika kuhakikisha kuwa sheria za nchi yetu zinafuatwa na kila mtu. Mmeonesha weledi (professionalism) wa hali ya juu.
Tuko pamoja na wewe Kamanda. Tutalinda kwa gharama yeyote usalama na utulivu wa nchi yetu. Vitendo vya kihuni vilivyofanywa na viongozi wapuuzi wa cdm haviwezi kuvumiliwa kamwe. Aidha siasa za kishenzi hazina nafasi katika Tanzania ya sasa.
Wazalendo tunaendelea kuchapa kazi katika kujiletea maendeleo yetu, hatuna muda wa kupoteza wala hatutapotoshwa na wanasiasa uchwara wanaotaka kutumia siasa kutimiza malengo binafsi.
Mungu Ibariki Tanzania.
kny Watanzania Wazalendo.