Ndugu yangu wembemkali,ardhi ya zimbabwe ilikuwa na faida kwa weusi chini ya milki ya wazungu kuliko ilivyo chini ya weusi wachache wateule wa Mugabe...Nafikiri ni wakati wa Mugabe kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya UBINADAMU,Kama ni uhuru hakupigania peke yake,na si kweli kwamba MDC ni chama kwa wale ambao hawakupigania Uhuru na si kweli kwamba wanachama wa MDC wote wamepewa fedha na wazungu ili wapige kura dhidi ya mugabe na si kweli kwamba kwamba taarifa ya POLISI ina ukweli kwa sababu kama mkuu wa majeshi anatoa amri ya kumpigia kura Mugabe kwa wanajeshi wote na kutishia ajira ya yule atekwenda kinyume itakuwaje Mkuu wa polisi athubutu kunena kwamba vurugu zinafanywa na wafuasi wa Raisi wake ? Muda umefika waafrika tuungane dhidi ya Dikteta Mugabe...tuwahurumie wazimbabwe tuwaondolee mugabe,kutokana na umri wake mugabe hana cha kupoteza hata kama nusu ya wazimbabwe watachomwa moto,tuache kudanganywa na hoja ya kwamba MDC ni kwa ajiri ya walionyang'anywa mashamba hata kama wanaiunga mkono ni kwa ajiri ya manifesto yake na si upendeleo ikiingia madarakani,propaganda za ZANU-PF zisitupumbaze tukapuuza mateso ya ndg zetu...