Rafa kilenza
Member
- Jan 23, 2017
- 32
- 30
UJUMBE WA WAZI KWA MH RAISI JOHN JOSEPH MAGUFULI
Salam mkuu
Naandika huu ujumbe leo saa 03:07 usiku
Kabla ya yote naomba nikupongeze na kukupa pole kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuiongoza nchi yetu
Hakika kila siku zinavozidi kwenda napata amani zaidi kwamba tulipata raisi muafaka kabisa katika zama kama hizi
Taifa letu lina changamoto kubwa sana za umasikini lakini pia ni taifa ambalo linaongoza kwa majungu, unafiki na wivu zaidi duniani
Ni Tanzania pekee ambapo watanzania wanatamani kiongozi wa serikali akosee ndio roho zao zinapata furaha na sio kumuombea huyo mtu afanikiwe ili atimize majukumu yake kwa ufasaha
Baada ya kutoa pongezi hizo kwako naomba sasa nikukumbushe mambo Machache sana kuhusu hili vugu vugu linaloendelea kwa kasi sana na kasi ya ajabu zaidi kuhusu mteule wako ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Mh Raisi ukisoma taharifa mbali mbali katika nchi zilizoendelea kuhusu namna gani vita ya madawa ya kulevya imeshindikana kabisa kuizua au kuisambalatisha kabisa unaweza usiamini kama ni kweli
Taifa kubwa kabisa duniani Marekani kwa mwaka wanatenga sio chini ya tilioni 30 za kitanzania katika kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya lakini adi sasa soko kubwa la biashara hii lipo Marekani uko uko na inafanyika kwa wingi sana
Marekani hakuna vita ambayo inashindwa lakini vita hii wameishindwa kabisa
Ni ajabu sana watu hawa waliweza kumuua OSAMA, SADAM HUSSEIN lakini wameshindwa kupambana na wauzaji wa madawa ambao hawana hata Jeshi
Taifa la ufilipino na wao wameshindwa kabisa kuzuia kufanyika kwa biashara hii pamoja ja kutenga fedha nyingi sana katika haya mapambano lakini kwa njia hiyo wameshindwa kabisa adi ikafika kipindi Raisi wa nchi yao akaamua kutumia mamlaka aliyokuwa nayo yeye(Presidential power an authority) na kuamua sasa kuwa yeyote atakayekutwa anafanya hii biashara au akikutwa ni mtumiaji wa madawa ya kulevya apigwe risasi hadharani na kuuliwa papo hapo bila hata kusubilia hukumu ya mahakama.Aliamua kutumia njia ya kihuni tu na amefanikiwa
Raisi wa ufilipino aliona kwamba kwa njia zinazotumika sasa duniani ni vigumu kufanikiwa maana ni biashara ambayo inahusisha watu wenye pesa zao nyingi sana ambao wana uwezo hata wa kuingilia kazi za serikali, bunge hata mahakama na kuamua taasisi zote hizo zifanye kazi wanazotaka wao wenyewe
Adi leo hii naandika hapa biashara ya madawa ya kulevya ndani ya ufilipino imepungua kwa zaidi ya asilimia 70, Haya ni mafanikio makubwa sana katika historia ya vita ya madawa ya kulevya ambayo hata taifa kubwa zaidi marekani na nguvu zote zs kijeshi walizokuwa nazo lakini wameshindwa
Mh Raisi inasemekana kupambana na hii biashara kwa njia ambazo zinafanyika sana hapa duniani tofauti na njia inayotumika uko ufilipino kamwe haziwezi kufanikiwa hata kwa 20%
Wauzaji wa madawa ya kulevya wanakuwa na mtandao mkubwa sana adi ndani ya serikali yeyote ile, Kazi yao kubwa watu hawa wanapenyeza watu wao ndani ya serikali ili mipango yote ya serikali inayotoka ambayo sio rafiki kwao waipate mapema sana ili wajue jinsi gani ya kupambana na serikali
Tusishangae kwa siku za karibuni siri za serikali adi zile barua za siri( confidential letters) zote zinapatikana mitaani tena zinatumwa moja kwa moja kwa wausika wakuu, kamwe kwa hili hatuwezi kufanikiwa, ni usalitu mkubwa sana unafanyika ndani ya serikali yako
Mfano mkubwa na sahii kabisa tumeona kwenye vikao vya bunge lililopita kwa muda wa siku mbili bunge letu la Tanzania liliacha kabisa kujadili na kutatua matatizo yanayoikabili nchi yetu na kuanza kujadili mtu mmoja tu ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dsm
Wabunge wote kwa pamoja bila kujali itikadi zao za vyama waliungana na kuanza kumshutumu mkuu wa mkoa kuwa ana miliki mali nyingi sana na kila mtanzania mwenye akili timamu aliwaza sana kwa sababu zipi leo hii hawa wabunge wetu ambao siku za nyuma walitofautiana sana katika kupitisha muswada wa habari, makato ya bodi ya mikopo pamoja na sheria za mitandao walishindwa kuungana kwenye mambo kama hayo lakini leo hii wameungana kwenye swala dogo kama hili?
Wabunge hawa hawa siku za nyuma walikuwa wanarushiana maneno makali sana adi kutaka kupigana ndani ya bunge na wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni waligoma kabisa adi kuhudhuria vikao vya bunge
Hakika kila mtu alishangaa sana lakini baada ya siku kadhaa ukweli wote ulipatikana kwamba ni mtu mmoja tu ambaye ni msanii wa bongo movie ndiye aliyekwenda Dodoma na kuanza kuwatafuta mawaziri wako waandamizi pamoja na wabunge wa upinzani na wa chama chako akawabadilisha upepo na wote hao waliotajwa na ushahidi upo kabisa wa audio ndio walianza kupiga fujo bungeni, Kama mtu mdogo kama stive nyerere anaweza kubadilisha na kuzishika akili za watu hawa je hawa wauza madawa ya kulevya watashindwa.?
Paul Makonda kabla ya kuwa mkuu wa mkoa wa Dsm alikuwa ni DC wa Kinondoni na aliteuliwa kipindi wewe mh raisi ni waziri wa ujenzi. Lazima ujiulize sasa kwanini hizi kashfa anazopata sasa hivi kuhusu kughushi cheti hazikuanza kipindi akiwa Dc? Au hazikuanza kipindi umemteua kuwa mkuu wa mkoa? Mh raisi kwanini hizi kashfa zimeibuka kipindi cha baada ya kuanza vita yake na wauzaji, watumiaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya.? Mh raisi hii vita ni kati ya makonda na mtandao haramu wa wauzaji wa madawa ya kulevya na washabiki wao na sio kitu kingine
Nani hajui kuwa club billcanas ndio ilikuwa chimbo la wauzaji wa madawa ya kulevya.?
Hawa wafanyabiashara wa madawa haya haramu wana mtandao mpana sana adi ndani ya serikali yako hawa watakuwa na watu wao wengi sana ndio maana kila taarifa wanazipata tena zikiwa bado za moto sana
Ndani ya chama chako wana mtandao wao mkubwa tu, kila sehemu hawa watu wana mtandao wao
Hii vita sasa wewe ndio umebaki mtu wa mwisho sasa kuamua uwape ushindi wauzaji kwa kumtoa makonda au uwape ushindi wapiga vita wa biashara ya madawa kwa kumuacha makonda hapo hapo Dsm ili wabaya wake waendelee kuteseke. Mh raisi huu ni mtego mkubwa sana kwako
Nadhani unakumbuka kipindi mh raisi ukiwa waziri kulitokea seke seke kubwa sana kuhusu ufisadi katika mkataba kati ya Tanesco na IPTL
Wabunge wengi sana waliamua kulisimamia hili swala kuhakikisha waziri wa nishati na madini msomi mzuri sana Prof SOSIPETER MUHONGO anatoka katika huo wadhifa wake, walikuja na sababu na kelele nyingi sana na adi wabunge wengine walilia bungeni ili waonekane ni wazalendo haswaa
Walijitahidi kuhakikisha kuwa waziri MUHONGO anatoka wizarani na wakafanikiwa kabisa
Hakuna asiyejua kuwa kati ya mawaziri wa nishati na madini tangu nchi yetu ipate uhuru hakuna waziri bora zaidi kama Prof muhongo lakini huyu mtu aliziba madili ya watu katika hiyo wizara ndio maana akachukiwa sana
Baada ya kufanikiwa kumtoa muhongo zilianza kusikika taharifa mbali mbali kuwa kuna wafanyabiashara ambao walinyimwa vitalu vya mafuta na mh muhongo baada ya kubainika kuwa hawana uwezo wa kuchimba mafuta ndio waliokuwa wanachochea ile vita yote ndani ya bunge kwa kuwapa fedha wabunge wale wote waliokuwa wanasimamia swala la escrow akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa PAC wa kipindi kile
Kwa mujibu wa SALIM KHATRI ambaye ni mtu anayelijua kwa undani zaidi hili swala la escrow aliwashutumu wazi wazi Aliyekuwa mwenyekiti wa Pac kipindi hicho kaka yangu Zitto Z Kabwe pamoja na ndugu yangu David Kafulila kuwa walikuwa wanatumiwa na standard chartered bank, na bwana khatri alisema wazi wazi kabisa kuwa zitto kabwe alimkimbia kwenye mjadala uliondaliwa baina yake khatri na zitto na adi sasa zitto hawezi kukubali kukutanishwa kwenye mjadala na bwana khatri na ushahidi huo mimi ninao
Mh Raisi hizi ndio siasa za Tanzania zilivyo na kuhakikisha kuwa hii vita ni baina ya makonda na wauzaji wa madawa ya kulevya na hakuna kingine. Wewe sasa ndio umebakia umalize hizi kelele kuhusu haya yanayoendelea hapa nchini kwa kuwanyamanzisha hawa wapiga kelele ambao ni mawakala wa wauzaji madawa au kuendelea kusapoti vita ya madawa ya kulevya.Hii vita haipaswi kufanyika kama adui yako anavyotaka haiwezekani leo hii watu wakuchagulie njia za kupambana
Biashara hii inapaswa kufanyika kwa njia za kihuni kihuni tu na sio kwa njia wanayotaka wao na ndio maana raisi wa ufilipino aliamua kupambana anavyotaka yeye japo wamepiga kelele lakini anafanikiwa na anaenda kuikomesha ndani ya nchi yake
Mh raisi tambua kabisa vitu vizuri huwa vinapigwa vita sana, kuna ma Rc mizigo kabisa lakini huwezi kusikia wakipigwa vita
Mwisho kabisa kwa mujibu wa katiba yetu wewe ndio unayeamua kuteua na kutengua, hakuna mtu anayeweza kukupangia umteua nani na umchague nani lakini tambua kwa sasa upo kwenye mtego mkubwa sana kuhusu mteule wako wa Dar, wewe ndio umebakia sasa umalize hili sakata tunaomba sana tena sana usisikilize kelele za hawa mawakala wa wauza unga na ukiona wapinzani wako wanakushauri sana kuhusu mteule wako usifuate ushauri wao maana hakuna mpinzani hapa Tanzania anayemshauri mwenzake jambo la heri
Nakutakia kazi Njema
Ndimi
Rafa lukindo
0765499321