Barua ya wazi kwa mtoto pekee kwa baba yako Ben Focus Rabiu Saanane

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Comred Malisa Godlisten
BARUA YA WAZI KWA MWANANGU MPENDWA LAURA.

Kwako Laura kipenzi,
Mtoto pekee kwa baba yako Ben Focus Rabiu Saanane.

Najua ungali mdogo na pengine hujui chochote kinachoendelea juu ya suala la baba yako. Lakini una akili ya utambuzi ya kumjua baba yako. Ni mwezi mzima sasa umepita hujasikia sauti yake. Mama yako hajakupa simu umsalimie, hajakuunganisha kwa Skype uongee nae kama zamani.

Bila shaka unajiuliza kwanini hali hii. Na pengine kwa kuwa bado hujaweza kuongea unashindwa kumuuliza mama yako. Lakini moyo wako unahisi upweke, unahisi kilio umejawa simanzi. Unamtaka baba, umemiss baba, unamkumbuka baba.

Laura mwanangu, kwa kifupi baba yako alitwaliwa katika hali ya kustaajabisha ambayo imemuacha kila mmoja wetu na maswali. Ni siku ya 32 sasa haijulikani alipo. Haijulikani kama yupo hai au mauti.

Serikali imempuuza, asasi za kiraia zimempuuza, mashirika ya haki za binadamu hayana muda nae. Kwani alikua nani kwenye taifa hili? Hakuwa waziri, hakua Mbunge, hakuwa mkuu wa mkoa. Acha apotee. Nobody cares. Hivyo ndivyo akili zao zinavyowatuma.

Familia yake na rafiki zake wamehangaika usiku na mchana kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa lakini bado ni giza. Giza nene. Giza kuu.

Laura huko ulipo ni tofauti na huku kwetu. Huko kwenu mmestaarabika. Mnajali utu, mnathamini uhai, mnaheshimu binadamu. Akipotea mtu mmoja serikali yenu itahakikisha anapatikana kwa gharama yoyote. Ndio maana nchi zenu zinaitwa nchi za dunia ya kwanza. Ni tofauti na huku kwetu dunia ya 3 ambapo mtu huweza kupotea kama sarafu idondokapo ndani ya bahari na watu wakaona ni jambo la kawaida.

Huku kwetu tunaitwa bara la giza. Tunathamini wanyama kuliko binadamu. Amepotea faru mmoja serikali nzima inahaha kujua alipo, lakini walikufa/kuuawa binadamu 7 na kutupwa huko mto Ruvu hakuna anayejali.

Tumeomba sana maiti hizo zifukuliwe na zipimwe vinasaba ili waliopoteza ndugu zao wakahakiki, ikiwa ni pamoja na ndugu wa baba yako. Lakini serikali imepuuza.

Badala yake imeagiza faru afukuliwe na apimwe vinasaba lakini maiti 7 za binadamu ziendelee kuozea ardhini bila kujulikana ni za nani, walikufaje, na kwanini walitupwa mtoni.

Laura binti yangu unaweza kunishangaa lakini ndio ukweli. Huku kwetu Faru mmoja ana thamani kuliko binadamu 7, anaogopwa kuliko binadamu 7, anaheshimika kuliko binadamu 7.

Mawaziri wanahangaika usiku na mchana kujua faru huyo alipo, lakini hakuna anayejishughulisha kujua baba yako Ben alipo.

Hatujui kama atapatikana au ndio amepotea kabisa kama kama ndege ya Malaysia. Hatujui kama atarudi salama au mlemavu. Hatujui kama ataridi mzima au mwenye upungufu wa akili. Hatujui atarudi ktk hali gani kwa sababu hatujui alipo. Na hatujui hao waliomshikilia (kama wapo) wanamfanya nini kwa sasa.

Sitaki kuamini kama itakua ndio mwisho wa kumuona baba yako, akifurahi na wewe, kucheza na wewe na kukufundisha ujasiri. Sitaki kuamini kama ukikua utaambiwa, utasimuliwa, na utahadithiwa kwamba baba yako kipenzi alipotea na hakuonekana tena milele. Sitaki kuamini kama huna nafasi tena ya kumuona baba yako hapa duniani. Sitaki kabisa kuamini hivyo.

Wewe ni malaika unayehitaji upendo wa wazazi wote wawili, lakini viumbe wasiojulikana wamempoteza baba yako, na kumpeleka mahali pasipojulikana. Umekua mpweke, umekua mkiwa, umekua mnyonge.

Kama kuna watu wamefanya dhambi hii, ipo siku watailipa. Ama wakiwa hai au wakiwa wamelala mauti, lazima watailipa. Mungu huwa haachi damu ya mnyonge ipotee bure.

Laura binti yangu jipe moyo mkuu. Najua mama yako ana wakati mgumu sana kila unapomuuliza alipo baba. Unapotaka mumuona kwa skype au usikie sauti yake kupitia simu. Unamiss kumuona baba akikwambia anakupenda, anakujali na anakuombea ukue ktk hekima na kimo. Unamiss tabasamu la baba yako, unamiss ujasiri wake, unamiss ucheshi wake.

Ningekua na uwezo ningeomba serikali ya nchi yako iingilie kati, ije ifanye uchunguzi kujua baba yako alipo. Maana serikali yetu ipo busy na faru kuliko binadamu. Maandiko yanasema wamelaaniwa wote waabuduo na kusujudia wanyama. Sisi tumechagua kulaaniwa. Tumechagua kutukuza wanyama. Tumechagua kumsujudia Faru John.

Kwa sababu Faru John anatuletea watalii, anatupa pesa za kigeni. Baba yako hakua na chochote cha kutupa. Kwanza alikua chama cha upinzani, kazi yake ya kukosoa haikufurahisha wakubwa. Hata elimu yake ya PhD aliyokua amalize hivi karibuni, isingeweza kusaidia nchi maana yeye ni chama cha upinzani. Kwahiyo hawana muda wa kuhangaika nae. Wapo busy na faru anayeingiza pesa za kigeni. Hivi ndivyo mamlaka ilivyoamua.

Hata wale watetezi wa haki za binadamu hawajajitokeza kusema lolote hadi sasa. Hawana muda na Ben. Uhai wa Ben si kitu kwao. Haki za binadamu hazimhusu baba yako, zinamhusu Faru.

Lakini usivunjike moyo binti yangu kipenzi. Yote haya ni ya kitambo tu. Wanaotumia mamlaka yao vibaya kunyanyasa wengine, ipo siku wataomba milima iwafunike lakini milima itawakimbia, wataomba ardhi iwameze nayo itawakataa. Na hapo ndipo kitatokea kilio na kusaga meno. Hapa duniani hatuna mji udumuo bali sote twautafuta ule ujao.

Usihuzunike Laura. Usisikitike. Jipe moyo mkuu. Lolote litakalotokea kwa baba yako jiweke tayari. Arudi akiwa hai au akiwa maiti ni matokeo ya wanadamu. Lakini haiondoi ukweli kwamba yupo Mungu aliye mkuu kuliko wao. Mwenye nguvu kuliko wao. Mwenye mamlaka kuliko mamlaka zote za dunia hii. Na huyo ndiye kimbilio letu la mwisho. Yeye hajawahi kushindwa, hashindwi na hatokaa ashindwe. Yeye atafanya njia.

Vyovyote iwavyo Laura kumbuka baba yako alikupenda, alikujali na alikuthamini. Alipenda uwe na uwezo wa kuhoji kama yeye, uwe na ujasiri zaidi yake, upende maarifa kama yeye. Yaweke maanani hayo na ukue ukiyafanyia kazi. Popote nitakapokuona nitakua namuona Ben ndani yako. Keep growing towards your dad's charisma.

Wako akupendaye kwa dhati,
Malisa GJ.
Baba yako Mdogo,

NB: Laura sio jina halisi la mtoto wa Ben. Nimeamua kuficha jina lake halisi kwa sababu maalumu.! [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
FB_IMG_1482295798637.jpg
 
Hii ni historia Tanzania faru ana thamani kubwa kuliko binadamu 7 na haijawahi tokea mtu kupotea kwa siku zaidi 32 bila vyombo vya usalama kujua alipo na hii ni kwa Tanzania pekee nchi inayo jinasibu kufuata utawala bora duniani
 
Porojo hizo.
. Huko dunia ya kwanza wengi sana wanapotea kuliko kwetu.

Hatuwezi leo hii kumlilia mbeba sumu mmoja ambaye waajiri wake wanajuwa alipo.
Uwe unajiongeza basi wewe bibi siyo kila ni siasa.
Huku kwetu tunaitwa bara la giza. Tunathamini wanyama kuliko binadamu. Amepotea faru mmoja serikali nzima inahaha kujua alipo, lakini walikufa/kuuawa binadamu 7 na kutupwa huko mto Ruvu hakuna anayejali.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 
Hii ni historia Tanzania faru ana thamani kubwa kuliko binadamu 7 na haijawahi tokea mtu kupotea kwa siku zaidi 32 bila vyombo vya usalama kujua alipo na hii ni kwa Tanzania pekee nchi inayo jinasibu kufuata utawala bora duniani
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba yupo humu JF ameshindwa hata kutoa tamko kuhusu swala hili la Ben-Rabiu Saanane kupotea hajulikani kama huko alipo yupo mzima kwa nini serikali wamenyamaza kimya?
 
Porojo hizo.
. Huko dunia ya kwanza wengi sana wanapotea kuliko kwetu.

Hatuwezi leo hii kumlilia mbeba sumu mmoja ambaye waajiri wake wanajuwa alipo.
Kama kuna watu wamefanya dhambi hii, ipo siku watailipa. Ama wakiwa hai au wakiwa wamelala mauti, lazima watailipa. Mungu huwa haachi damu ya mnyonge ipotee bure.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 
Serikali imempuuza, asasi za kiraia zimempuuza, mashirika ya haki za binadamu hayana muda nae. Kwani alikua nani kwenye taifa hili? Hakuwa waziri, hakua Mbunge, hakuwa mkuu wa mkoa. Acha apotee. Nobody cares. Hivyo ndivyo akili zao zinavyowatuma.
Mkuu ebu acheni UNAFIKI......Ebu tuonyeshe ni mahali papi CDM imeonyesha kutopuuza kupotea kwa BEN???????HAPO ULITAKIWA KUSEMA PIA CDM imepuuza kupotea kwa BEN.....ACHENI UWOGA SEMENI UKWELI PINDI INAPOBIDI

Kazi yake ya kukosoa haikufurahisha wakubwa
Wakubwa include ndani ya CHAMA CHENU maana inasemekana ni mkosoaji mkubwa sana huko........

Hata wale watetezi wa haki za binadamu hawajajitokeza kusema lolote hadi sasa. Hawana muda na Ben. Uhai wa Ben si kitu kwao. Haki za binadamu hazimhusu baba yako, zinamhusu Faru.
Vp boss wake kasema nini mpaka sasa??????Ubora wa nyumba utegemea msingi bora kabsa wa nyumba......Tamko la m/kiti ndio tunaliita msingi wa nyumba so usitegemee matamko mengne yaye na impact ili hali msingi wa TAMKO ni zero kabsa.......
 
Kama kuna watu wamefanya dhambi hii, ipo siku watailipa. Ama wakiwa hai au wakiwa wamelala mauti, lazima watailipa. Mungu huwa haachi damu ya mnyonge ipotee bure.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]

Isijekuwa ni malipo ya kubeba sumu.
 
Back
Top Bottom