Barua ya wazi kwa mh. Zitto kabwe

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Mheshimiwa Zitto,
Namshukuru Mola kwa kunipa nafasi na wazo hili la kukuandikia barua hii ya wazi.

Kwanza nianze kwa kusema kwamba mimi ni miongoni mwa Watanzania ambaye nilikuwa ninavutiwa sana na misimamo yako ya kizalendo ndani na nje ya Bunge. Ulivunja rekodi pale ambapo ulitolewa Bungeni kwa sababu ya msimamo wako thabiti katika kutetea maslahi ya umma.

Ni muda mrefu sasa kumekuwa na tuhuma nyingi toka ndani na nje ya chama chako (CDM) ya kwamba wewe pamoja na watu wako wengine wa karibu mmekuwa mkikiasi chama na kufanya mambo ya kudhoofisha harakati za upinzani nchini Tanzania. Mheshimiwa, vilevile kumekuwa na tetesi nyingi ya kwamba chama cha ACT ambacho kinasimamiwa na Ndg. Mwigamba kama Katibu Mkuu ni moja ya mikakati yako ya kupambana na CDM.

Mheshimiwa, natamani kupata kauli yako kuhusu msimamo wako na ukweli wa moyo wako kuhusu chama cha ACT. Naamini ni Watanzania wengi pia wenaopenda kusikia msimamo wako wa kisiasa.

Asante kwa kutumia muda wako kusoma waraka huu mfupi, na ninaamini kwamba utachukua hatua ya kuweka wazi msimamo wako.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Mkuu, ungeweka bandiko hili kule Facebook ungempata na pengine angekujibu fasta. Humu alishakimbia siku nyingi. Kukaa humu unatakiwa ujipange na usijichanganye kabisa kwa kauli zako. Utapewa reference zako mwenyewe za nyuma ulizowahi kuzisema na kuziandika ambazo zinapingana na kauli zako za sasa hadi ukome. Muulize Mwigamba, alipewa za uso humu humu naye akasepa.
 
mleta mada una moyo sana,huyu mamuluki wa ccm alishakwisha habari yake! Dhambi ya usaliti inamtafuna kabaki kujificha MMU, facebook na twitter!
 
Huyo barua ndo kwanza itamfanya akimbie mitandao kabisa,unataka akubali ili ubunge uishie hapohapo? Hujui kuwa mahakama ndiyo imeshijilia ubunge wake?
 
mtoa mada kaandika vzr bt wachangiaji ndo wanahrbu jukwaa
jamani tumpe kila mtu uhuru wake wa kuamua haijalishi kuwa ni mwana ccm,cdm,cuf,act ,
tukianza kubezana na kudharauliana huku ipo siku tutatafuta kulipuana!!
wengi tunaamini zzk alfanya kosa kubwa la usaliti kama ilivyokuwa kwa yuda lkn isiwe kigezo cha kumhukumu
maandiko yanasema kuwa unapoelekea ukombozi unabii lzma itimie,,ila ole wake yule ambaye unabii utatimia kwake,,atalia na kusaga meno siku ya mwisho
kwa hiyo cha msingi tupambane kwa ajili ya ukombozi then tusubiri kiama cha walioifikisha tz hapa ilipo
 
Hivi nyie wehu msipomtaja Zitto mtakufa? kama kawasaliti simuachane naye na usaliti wake mpaka mumtukane? kawafanyaje mpaka muda wote mnamtukana? kama ni msaliti simmeshamfaham kwamba ni msalit na simmesha muweka kando ndan ya CDM? Mnawasiwasi gani naye? mbona nyie akili ndogo mnakaa mnajadili? je kukaa kwake kimya kunawachanganya nini nyie kanga moko? au alikuaga anawapulia kisogoni siku hizi kaacha? kuna nini mbona Zitto anawanyima usingizi? kama ni msaliti yeye ndo kawa wakwanza? je kukaa muda wote na kumtukana Zitto ndo siasa za kweli kwenu nyie wavuta bange na viroba? hamchoki kumtukana Zitto nyie mashetani? kama siasa imewashinda, kwanini msiwaache hawa MAGAMBA waendelee kutawala? Kati ya watu wote mnaowaita wasalita kwanini Zitto anaonekana kuwaumiza vichwa zaidi? kwanini kila anayepinga mawazo ya CDM au Mbowe na Slaa au mnamuita msaliti? ACHANENI NA ZITTO BWANA! IJENGENI CHADEMA NA NCHI KWA UJUMLA. Kichwa kimoja kinawapa presure!!!!!! mmekwisha!!!!!
 
Udini ndani ya chama ndio sababu ya Zitto kuonekana msaliti.Zitto yupo sawa na msimamo wake na dini yake na maslahi ya taifa kwa ujumla lakini pana ukweli ambao umefichwa hapa ambao Watanzania wengi hawajuwi.
 
ww ndo hujui chochote bora huendelee kuchunga mbuzi tuu unataka kucheza muziki ambayo huwezi kucheza utaabika bure kama ccm wanakutumia kama kondomu muda wao kuendelea kuwepo madarakani umeshafikia kikomo kula za mwisho ushauri wa bure huu
 
:llama:
mtoa mada kaandika vzr bt wachangiaji ndo wanahrbu jukwaa
jamani tumpe kila mtu uhuru wake wa kuamua haijalishi kuwa ni mwana ccm,cdm,cuf,act ,
tukianza kubezana na kudharauliana huku ipo siku tutatafuta kulipuana!!:llama::llama:
wengi tunaamini zzk alfanya kosa kubwa la usaliti kama ilivyokuwa kwa yuda lkn isiwe kigezo cha kumhukumu
maandiko yanasema kuwa unapoelekea ukombozi unabii lzma itimie,,ila ole wake yule ambaye unabii utatimia kwake,,atalia na kusaga meno siku ya mwisho
kwa hiyo cha msingi tupambane kwa ajili ya ukombozi then tusubiri kiama cha walioifikisha tz hapa ilipo
 
ww ndo hujui chochote bora huendelee kuchunga mbuzi tuu unataka kucheza muziki ambayo huwezi kucheza utaabika bure kama ccm wanakutumia kama kondomu muda wao kuendelea kuwepo madarakani umeshafikia kikomo kula za mwisho ushauri wa bure huu

huwezi kuona mpaka uoneshwe ipo siku utafahamu nina maana gani pole sana mdanganyika.
 
Udini ndani ya chama ndio sababu ya Zitto kuonekana msaliti.Zitto yupo sawa na msimamo wake na dini yake na maslahi ya taifa kwa ujumla lakini pana ukweli ambao umefichwa hapa ambao Watanzania wengi hawajuwi.

Hebu kuwa mkweli lini chama chake kilimtaka abadili dini?
 
,

Ni muda mrefu sasa kumekuwa na tuhuma nyingi toka ndani na nje ya chama chako (CDM)

[/FONT][/SIZE][/COLOR]

Mkuu,
With all due respect, Naomba kuweka records sawa katika hili.
Zitto si Mwana CHADEMA,Zitto ni Mwana Mahakama.
 
Mheshimiwa Zitto,
Namshukuru Mola kwa kunipa nafasi na wazo hili la kukuandikia barua hii ya wazi.

Kwanza nianze kwa kusema kwamba mimi ni miongoni mwa Watanzania ambaye nilikuwa ninavutiwa sana na misimamo yako ya kizalendo ndani na nje ya Bunge. Ulivunja rekodi pale ambapo ulitolewa Bungeni kwa sababu ya msimamo wako thabiti katika kutetea maslahi ya umma.

Ni muda mrefu sasa kumekuwa na tuhuma nyingi toka ndani na nje ya chama chako (CDM) ya kwamba wewe pamoja na watu wako wengine wa karibu mmekuwa mkikiasi chama na kufanya mambo ya kudhoofisha harakati za upinzani nchini Tanzania. Mheshimiwa, vilevile kumekuwa na tetesi nyingi ya kwamba chama cha ACT ambacho kinasimamiwa na Ndg. Mwigamba kama Katibu Mkuu ni moja ya mikakati yako ya kupambana na CDM.

Mheshimiwa, natamani kupata kauli yako kuhusu msimamo wako na ukweli wa moyo wako kuhusu chama cha ACT. Naamini ni Watanzania wengi pia wenaopenda kusikia msimamo wako wa kisiasa.

Asante kwa kutumia muda wako kusoma waraka huu mfupi, na ninaamini kwamba utachukua hatua ya kuweka wazi msimamo wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Potezea basi kama vipi. Sio issue.
 
Ni kweli msaliti na ametuangusha wengi na kajenga chuki dhidi ya wapenda haki hatumkubali tena! lakini tuchunge kauli zetu tunavyoandika na kuongea!
 
Udini ndani ya chama ndio sababu ya Zitto kuonekana msaliti.Zitto yupo sawa na msimamo wake na dini yake na maslahi ya taifa kwa ujumla lakini pana ukweli ambao umefichwa hapa ambao Watanzania wengi hawajuwi.

CHADEMA wanafukuza hadi Wakristo wenzao? Kwani katibu mkuu wa act ni dini gani? kumbuka huyu ndio alikua mwenyekiti wa CDM mkoa ambao nyie hua mnaita ngome ya CDM, Arusha! Sorry, hivi na Kitila Mkumbo nae ni dini gani kweli?
 
Barua hii ingeelekea Magogoni kuwauliza kwa nini nchi yetu ni maskini wa kutupwa ningefurahi sana, lakini kuwauliza hawa misukule wenye kuganga njaa wala haisaidii chochote
 
Zitto anawatesa sana hadi leo kama mwanachama wa mahakama mnamfuata wa nini? Jengeni chama chenu cha kikabira
 
Back
Top Bottom