Bonson
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 183
- 147
Mheshimiwa Zitto,
Namshukuru Mola kwa kunipa nafasi na wazo hili la kukuandikia barua hii ya wazi.
Kwanza nianze kwa kusema kwamba mimi ni miongoni mwa Watanzania ambaye nilikuwa ninavutiwa sana na misimamo yako ya kizalendo ndani na nje ya Bunge. Ulivunja rekodi pale ambapo ulitolewa Bungeni kwa sababu ya msimamo wako thabiti katika kutetea maslahi ya umma.
Ni muda mrefu sasa kumekuwa na tuhuma nyingi toka ndani na nje ya chama chako (CDM) ya kwamba wewe pamoja na watu wako wengine wa karibu mmekuwa mkikiasi chama na kufanya mambo ya kudhoofisha harakati za upinzani nchini Tanzania. Mheshimiwa, vilevile kumekuwa na tetesi nyingi ya kwamba chama cha ACT ambacho kinasimamiwa na Ndg. Mwigamba kama Katibu Mkuu ni moja ya mikakati yako ya kupambana na CDM.
Mheshimiwa, natamani kupata kauli yako kuhusu msimamo wako na ukweli wa moyo wako kuhusu chama cha ACT. Naamini ni Watanzania wengi pia wenaopenda kusikia msimamo wako wa kisiasa.
Asante kwa kutumia muda wako kusoma waraka huu mfupi, na ninaamini kwamba utachukua hatua ya kuweka wazi msimamo wako.
Mungu Ibariki Tanzania.