Barua ya wazi kwa Fatma Karume (Fetty).

Barua ya wazi kwa Fatma Karume (Fetty).

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Dada Fatma, awali ya yote nikupongeze kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa chama cha mawakili Tanzania (TLS), nina amini viatu vya Tundu Lissu vimepata mvaaji anayestahili.

Dada Fetty, ninaandika barua hii kwa uchungu sana na ninaomba uichukulie kwa uzito wake haya ninayoandika. Usipuuze hata moja, kwani kufanya hivyo utakuwa unamkosea hata Mungu wako.

Dada Fetty, alipoingia kwenye nafasi hiyo, Rais aliyekutangulia yaani Tundu Lissu na TLS kwa ujumla, waliahidi kuipeleka serikali mahakamani kuhusiana na hii mambo ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imegeuzwa kuwa shamba la bibi.

Kwa bahati mbaya sana, kaka Lissu, alipatwa janga kubwa kutokana na MAHARAMIA kutaka kuondoa uhai wake. Nachukua nafasi hii kuwalaani wote waliohusika, na kuratibu jaribio lile la kumuondoa Lissu duniani. Kutokana na janga alilopata kaka Lissu, mambo mengi sana yalisimama likiwamo hili la mpango na nia ya kuiburuza mahakamani serikali kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii.

Dada Fetty, siku kama mbili zilizopita, kupitia Mbunge wa Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe, wahanga wa mifuko ya hifadhi ya jamii tumearifiwa kwamba, CCM imekopa mamilioni ya shilingi toka mifuko ya hifadhi ya jamii na bado haijarudishwa pesa hiyo.

Kwa nafasi yako, na kwa kushirikiana na team nzima ya TLS, na wanasheria wenye nia njema na wapenda haki, tunaomba mfuatilie na mjiridhishe kisheria kuona iwapo mifuko hiyo inaruhusiwa kutoa mikopo kwa vyama vya kisiasa, na kwa makubaliano gani na wanachama ambao ni sisi. Tupiganieni sisi tuliotelekezwa na vyama vya wafanyakazi, vilivyopoteza dira na mwelekeo.

Naomba pia, kwa kushirikiana na wanasheria wa TLS, muangalie namna gani mtafanya ili kuiomba mahakama kwa hoja, iweze kutengua sheria inayomzuia mwanachama wa mfuko wa jamii kuchukua mafao yake eti mpaka afikishe umri wa miaka 55 au 60. Hili liangaliwe kwa kuzingatia uhaba wa ajira, umri wa kuishi, ugumu wa maisha, na watu wasio na ajira kukosa kuaminiwa kupata mikopo. Saidia hili, maana sisi wanachama ambao pesa zetu zimezuiwa na mifuko ya jamii, kwa sasa tunataabika mitaani, kazi hazipatikani, hatuna mitaji ya kuanzisha hata biashara ya ICE CREAM, halafu pesa zetu kuna watu wanagawana kwa kukopeshana bila taratibu. Hii si haki hata kidogo.

Baada ya kuainisha grievance yangu, nikutakie majukumu mema. Mungu akubariki na aibariki TLS.
 
umeandika kwa uchungu ...lkn before 2020 kweny Election Fao la kujitoa serikal itakuwa imeliludisha trust me kwan ccm iyo ndo uwa michezo yao na Ajira zitaanza kutoka serikalin.
 
tulivyo na wabunge wachumia tumbo walitunga sheria hyo ili wafaidike wao na chama chao,bila kujali ni watanzania wangapi wataumia kwa kigezo cha miaka 55 .TLS wateteeni watanzania wasioweza kusikika.
 
MAZWAZWA wakishindwa kwenye nguvu ya hoja basi hukimbilia kuteka, kutesa na hata kuua pia. Kwao wao wale wanaowachukia kwa sababu tu ya uelewa wao na kujitambua uhai wao hauna thamani hata chembe.

Kumbe Lissu ilikuwa lazima auwawe, agenda zake hazina majibu.
 
Msamehe ndugu! Ni mahaba yake na soka!
Sawa, ila kuna wakati lazima kusoma mood ya watu au mtu. Haiwezekani watu wako msibani wanaomboleza, halafu anatokea mtu na kuanza kucheka cheka utafikiri anawashwa. Na watu kama hawa ndiyo wanaturudisha nyuma. Yaani ni empty headed to the fullest.
 
umeandika kwa uchungu ...lkn before 2020 kweny Election Fao la kujitoa serikal itakuwa imeliludisha trust me kwan ccm iyo ndo uwa michezo yao na Ajira zitaanza kutoka serikalin.
Hawawezi kulirudisha, kwa sababu mbali na kua ccm imekopa na kukataa kulipa hela za wastaafu, serikali pia inadaiwa pesa nyingi za mifuko ya jamii
 
Kuna mengi yanaumiza sana...

Yanatia hasira sana...

Kila kukicha ni marekibisho tuu lakini pesa za wanyonge zinapokwenda haijulikani...


Cc: mahondaw
 
Hawawezi kulirudisha, kwa sababu mbali na kua ccm imekopa na kukataa kulipa hela za wastaafu, serikali pia inadaiwa pesa nyingi za mifuko ya jamii
Hakuna kinachoshindikana chini ya 'nguvu ya umma'. We ngoja waendelee na mambo yao ya hovyo hovyo. Hawajui kuwa kiwango cha uvumilivu kina ukomo.
 
Back
Top Bottom