Barua ya Steve Jobs kabla ya kufariki dunia

presider

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,034
1,280
Katika hali ya kukata tamaa aliandika haya!
“Nilifikia kilele cha mafanikio katika biashara duniani. Katika macho ya watu wengine, maisha... yangu ni kielelezo cha mafanikio. Hata hivyo, mbali na kufanya kazi, nina furaha ndogo. Kwa jumla, utajiri ni uhalisia tu wa maisha ambayo nimeyazoea.
Wakati huu ambao nimelala kitandani nikiwa mgonjwa na kuyakumbuka maisha yangu yote, ninagundua kwamba ufahamu utajiri nilionao umefifia kwa kuwa hauna maana wakati kifo kinakaribia.
Nikiwa gizani, ninautazama mwanga wa kijani kutoka katika mashine zinazonisaidia kuendelea kuishi na kusikia sauti za muungurumo wake, ninasikia na kuhisia pumzi za Mungu na za kifo zikinikaribia…
Sasa nafahamu kwamba tunapolimbikiza utajiri wa kutosha maishani mwetu, inatupasa kufuatilia mambo mengine ambayo hayahusiani na utajiri…
Kiwe ni kitu fulani ambacho ni muhimu zaidi:
Labda ni uhusiano, labda ni sanaa, labda ni ndoto inayoanzia katika siku za ujana…
Kutafuta utajiri muda wote utamwingiza mtu katika maisha yasiyofahamika, kama mimi.
Mungu alitupa hisia za kutambua pendo katika kila moyo wa mtu, si mauzauza yanayoletwa na utajiri.
Utajiri nilioupata maishani mwangu siwezi kuondoka nao.
Ninachoweza kuondoka nacho ni kumbukumbu zilizojaa upendo.
Huo ndiyo utajiri wa kweli utakaokufuata, utakaoungana nawe, ukakupata nguvu na mwanga wa kusonga mbele.
Upendo unaweza kusafiri maelfu ya maili. Maisha hayana kikomo. Nenda unapotaka. Fika katika kilele unachotaka kufika. Yote yamo moyoni na mikononi mwako.
Ni kitanda gani chenye gharama zaidi duniani? Ni kitanda wanacholalia wagonjwa…
Unaweza kumwajiri mtu akaendesha gari lako, mtu akakuingizia fedha lakini huwezi kumpata mtu wa kubeba ugonjwa wako.
Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna kitu kimoja ambacho hakipatikani pindi kikipotea – ni Maisha.
Mtu anapokwenda katika chumba cha upasuaji, atagundua kwamba kuna kitabu kimoja ambacho bado hajamaliza kukisoma – “Kitabu cha Maisha ya Afya”.
Hata tukiwa katika daraja gani la maisha hivi sasa, muda ukifika, tutakabiliana na siku ambapo pazia la maisha litashuka.
Thamini Upendo kwa familia yako, mpende mwenza (mke/mme) wako, wapende marafiki zako. Jitambue vyema. Wathamini watu wengine.”
Jobs!
Steven Paul Jobs 'Steve Jobs' ndiye alivumbua vifaa vya Apple, zikiwemo simu, tablets na Laptop' alizaliwa Februari 24, 1955 na alifariki 5 oktoba 2011 (akiwa na miaka 56)
Kitabu cha maisha yake kimekusanya mambo muhimu na ya kusisimua mno!
 
Kama ameweza kuyakumbuka na kuyasema hata kabla ya kufa,sina shaka amepata hata muda wa kukiri na kusema Yesu ni Bwana na kuomba toba.
RIP Steve Jobs dunia bado inajua you are the best!!
 
Matajiri wanapenda kutudanganya sana,at least he died decently and not naked.
Hakuna mtu asojua kuwa kufa kupo tu.
 
barua adhimu hii... barua hii iwaende wote matajiri na wenye mamlaka ya juu.. kwamba siku ikifika huwa amali njema ndo itakuwa faraja ya waliobaki na uelekeako
 
Pamoja na yote aliyoyasema,bado hajaondoa ukweli kuwa HATUFANANI.Matajiri wanaanza kuionja pepo hapa hapa duniani kabla ya huko tusikokujua.Sina uhakika kama tunapepo ya kiwango cha juu kuliko Suleiman [Solomon].
 
Huyu jamaa alikuwa kichwa sana hasa kwa kujua ni nini binadamu anataka hakuwa anajua programing wala masuala ya umeme ila alikuwa ana taste ya vitu na anajua marketing sana.
Ila alikuwa na matatizo yafuatayo
1. Alikuwa anaamini yeye anajua sana kuliko watu wote. Yani kile alichokuwa anaamini ndicho kwake kilikuwa sahihi. Hata hiyo cancer aliambiwa afanyiwe operation mapema tu kabla haijasambaa akagoma akidai atakula matunda na vyakula mbalimbali itapona.
2. Alikuwa ni mtu mwenye majivuno sana na alikuwa hajali hisia za wenzake. Mfano alikuwa anaweza kukufuza kazi just onspot kwa kosa dogo tu hadi wafanyakazi walikuwa wanamuogopa.
3. Alikuwa ni kigeugeu mfano Steve Wozniak anadai baada ya apple kuwa kampuni kubwa na Steve kuwa ndo CEO alikuwa hana muda naye tena yani ule ushikaji ukaisha.
4. Alimzalisha GF wake aliyempenda wakati steve akiwa hana kitu hadi anaenda chuo akiwa anapekua, alipompa mimba akaikataa na mpaka anakufa aligoma kumpa msaada huyo mzazi mwenzake na mtoto wake japo alikuwa ni tajiri na million dollars lakini hata a thousand dollars alikuwa hataki wapate kutoka kwake.
Japo na mapungufu yake ila jamaa alikuwa ana mawazo ya kipekee sana. Alikuwa akimdharau Billgates mpaka anakufa alikuwa akisema Bill Gates hana taste amebahatika tu akafanikiwa lakini hana lolote yani hakuwahi kumsifia alikuwa anasema products za Microsoft ni garbages tu.
Ila Bill kuna mambo yalikuwa yana muinspire toka kwa Steve mengi hadi aliwahi kuwambia wafanyakazi wenzake inabidi wajifunze kwa apple katika kudesign vitu.
Ila Bill Gates pia alikuwa anamdharau Steve kwakuwa Steve hakuwa programmer wala engineer, wakati streve wanataka kumrudisha apple awe CEO baada ya kampuni kuwa inaelekea shimoni, Gates alipiga simu kwa CEO aliyekuwepo akamwambia mbona anapotea huyo Jobs hakuna analojua kuhusu teknology anapoteza muda. Lakini Jobs alimprove wrong aliporudi apple akaitansform na sasa ni kampuni kubwa.
 
RIP Steve Jobs dunia bado inajua you are the best!!
1544281479285.png
 
Daa hii ni kweli kabisa kama aliweza kulitambua kabla mauti hayaja mfika, hakika hata uwe na mali kiasi gani hakuna mwenye kuweza kubeba ugonjwa wako.
Hii inatukumbusha sisi wengine tunaondelea kupigana kufa na kupona kuutafuta utajiri kumbe utajiri utauacha hapa duniani na cha muhimu ni kutafuta pesa ya kukupa maisha mazuri na nguvu nyingi kuweka kumtafuta Mungu na utukufu wake...
 
Negative or Positive show your self where are you? Maisha ni zaidi ya wengi tujuavyo lakini Mungu ni mwema zaidi.
 
Ni adhabu aliyopewa na MUNGU, yaani kufa huku anajiona...:.

Huwezi kuwa "msenge" tena unajisifia kuwa hivyo, yaani wewe unaingiliwa na wanaume wenzako na ni tajiri mkubwa , tena ukaamua kubuni nembo kabisa ya kuwa TUNDA LAKO LINAMEGWA halafu ukabaki salama.

Ndugu zangu tumrejeeni Mwenyezi Mungu kwa TOBA na SALA NYINGI
 
acha uongo wew stev jobs hakuwa shoga
 
Katika hali ya kukata tamaa aliandika haya!
“Nilifikia kilele cha mafanikio katika biashara duniani. Katika macho ya watu wengine, maisha... yangu ni kielelezo cha mafanikio. Hata hivyo, mbali na kufanya kazi, nina furaha ndogo. Kwa jumla, utajiri ni uhalisia tu wa maisha ambayo nimeyazoea.
Wakati huu ambao nimelala kitandani nikiwa mgonjwa na kuyakumbuka maisha yangu yote, ninagundua kwamba ufahamu utajiri nilionao umefifia kwa kuwa hauna maana wakati kifo kinakaribia.
Nikiwa gizani, ninautazama mwanga wa kijani kutoka katika mashine zinazonisaidia kuendelea kuishi na kusikia sauti za muungurumo wake, ninasikia na kuhisia pumzi za Mungu na za kifo zikinikaribia…
Sasa nafahamu kwamba tunapolimbikiza utajiri wa kutosha maishani mwetu, inatupasa kufuatilia mambo mengine ambayo hayahusiani na utajiri…
Kiwe ni kitu fulani ambacho ni muhimu zaidi:
Labda ni uhusiano, labda ni sanaa, labda ni ndoto inayoanzia katika siku za ujana…
Kutafuta utajiri muda wote utamwingiza mtu katika maisha yasiyofahamika, kama mimi.
Mungu alitupa hisia za kutambua pendo katika kila moyo wa mtu, si mauzauza yanayoletwa na utajiri.
Utajiri nilioupata maishani mwangu siwezi kuondoka nao.
Ninachoweza kuondoka nacho ni kumbukumbu zilizojaa upendo.
Huo ndiyo utajiri wa kweli utakaokufuata, utakaoungana nawe, ukakupata nguvu na mwanga wa kusonga mbele.
Upendo unaweza kusafiri maelfu ya maili. Maisha hayana kikomo. Nenda unapotaka. Fika katika kilele unachotaka kufika. Yote yamo moyoni na mikononi mwako.
Ni kitanda gani chenye gharama zaidi duniani? Ni kitanda wanacholalia wagonjwa…
Unaweza kumwajiri mtu akaendesha gari lako, mtu akakuingizia fedha lakini huwezi kumpata mtu wa kubeba ugonjwa wako.
Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna kitu kimoja ambacho hakipatikani pindi kikipotea – ni Maisha.
Mtu anapokwenda katika chumba cha upasuaji, atagundua kwamba kuna kitabu kimoja ambacho bado hajamaliza kukisoma – “Kitabu cha Maisha ya Afya”.
Hata tukiwa katika daraja gani la maisha hivi sasa, muda ukifika, tutakabiliana na siku ambapo pazia la maisha litashuka.
Thamini Upendo kwa familia yako, mpende mwenza (mke/mme) wako, wapende marafiki zako. Jitambue vyema. Wathamini watu wengine.”
Jobs!
Steven Paul Jobs 'Steve Jobs' ndiye alivumbua vifaa vya Apple, zikiwemo simu, tablets na Laptop' alizaliwa Februari 24, 1955 na alifariki 5 oktoba 2011 (akiwa na miaka 56)
Kitabu cha maisha yake kimekusanya mambo muhimu na ya kusisimua mno!
Mkuu wapi naweza kupata kopi ya hio barua,
Asante
 
Back
Top Bottom