Barua pepe ya mwaka 2007...(Miaka miwili baada ya JK kuwa Prez) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua pepe ya mwaka 2007...(Miaka miwili baada ya JK kuwa Prez)

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kibunango, Aug 8, 2011.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, Maubungo Plaza, Mayfair Plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile la Kibiti watasha wenyewe wanabloo! Na neshino stediumu mpya ikiisha litakuwa hamna tena Afrika nzima!

  Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi! Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Maselebriti wa vipaji vya kitaaluma, kisanii, kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!

  Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama wakati tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio la Arusha kwa kuwa bepari au kabaila kwa sababu ya kumiliki tivii! Eee bwana na magari mengine hata ughaibuni hamna sijui mabaluni, maviieksi, Mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!

  Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli na yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa inteki, yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!

  Siku hizi simu siyo big dili! Unaambiwa nilikuwa Nanjumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea na sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za TTCL ilikuwa uende kibanda cha simu tena ukikikuta nzima una bahati sivyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi teksi meseji au ukiona namna gani vipi unanda intaneti unatuma imeli!

  Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua bomba gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu!

  Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Siulimuona nanihii, alipoondoka kwenda ughaibuni alikuwa na mimba hiyoo mashavu utafikiri anapuliza moto! Karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete zako. Kuna majamaa hapa Bongo wanaishi kama mtoni asubuhi wanapata brekifasti ya masoseji, hambagi, juisi na chai ya maziwa matupu au uji uliopikwa na unga wa keki ukatiwa na mapande ya siagi na krimu! Lanchi chikeni chipsi na kuku, dina steki hevi grili pateto au raisi! Yaani wee acha tu, Bongo New York.

  Na manjagu wanakula mavitu hevi siyo kama enzi za Mahita tangu kaja Said Mwema manjagu wanatia vitu vya kimtoni maksi sijui mabelti, yaani we acha tu!
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu sikonge happy to see u back, nimecheka saaaanaaaa. Eti mtu aliondoka na mimba akarudi miguu ka mikono hahahahahahhaah.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ni Kibunango.... Kheeee heeee heeeee... Eeeh!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ungwana ni vitendo! That was a hoax barua pepe!
   
 5. s

  shosti JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhhh wabongo kukuza mambo,hizo shopping mall za kufananisha na majuu ziko wapi jamani...
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha! miss kata, uji wa unga wa keki,CHIKENI CHIPSI NA KUKU -hapo ndio funga kazi hahahaha!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyu alikuwa anaishi Buza au kimanzi chana lol!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Shem, angalia bandiko lipo ukumbi gani...
   
 9. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Umeniacha hoi bin taaban.
   
Loading...