Barua na salamu zangu kwa Airtel

Barua na salamu zangu kwa Airtel

Hapana ni airtel wanazo kuanzia 600 per 2days dk 60 1.2 Gb, 1500 150dk 1GBper 7 days na 6000 per 30 days mm hua natumia io ya 6000 dk500 5GB unltd sm
 
Nakumbuka niliamua kwa moyo mmoja kujiunga familia ya AIRTEL miaka mitatu iliyopita. Kwa miaka mitatu iloyopita niliishi kwa furaha san(of cause mi ni mtu wa bando za internet kuliko za kupiga na sms) kidogo wakaanza kupandisha gharama ila nilikua nawaelewa sana so nikaamua kuvimba nao.
Ila leo naaga rasmi familia yenu nawashukuru kwa marafiki mlionipa na hela zangu nlizowapa ila 5000 kwa GB 1 hapo mmeniweza.
Naskia kuna Haloteli ngoja nikaponee huko kama vile nyie mlivoniponya toka kwa Vodacom. Wacha nizidi kua mkimbizi sasa maana hamna namna.......
#nimeamini_muhindi_sio_ndugu_yako

Kwaheri ya kuonana

karibu sana Halotel, hadi huku kijijini kwetu net inashika vizuri, Salio kidogo Mb za kumwaga
 
Yaani mimi kinachonibakisha airtel ni UNI voucher. Ila wakizitoa hizi ni spidi kali sana kuelekea Halotel. Yaani hapa nina line ya Halotel ipo kama standby.
 
Yaani mimi kinachonibakisha airtel ni UNI voucher. Ila wakizitoa hizi ni spidi kali sana kuelekea Halotel. Yaani hapa nina line ya Halotel ipo kama standby.
Nakuambia na hiyo wataondoa wahuni sana.. nakumbuka zamani nilikua naweka bandle mpaka naaza kutoa hotspot bure kwa wana saabu ilikua simple tu
 
Back
Top Bottom