• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Barua kwa serekali yetu na bunge letu tukufu la kutunga sheria la tanzania na baraza la wawakilishi

A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
858
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
858 0WANANCHI TUNATEKETEA NA KILIO CHETU HATUNA WA KUMLILIA

Sinabudi kutowa malalamiko yetu kama mwananchi wa Tanzaniamwenye kustahili kupewa haki za nchi yangu kama Mtanzania yoyote yule.

Mimi nazungumzia sana kuhusu hawa Wabunge wetu na wawakilishikatika kazi zao na majukumu yao juu yawananchi walio wachaguwa katika majimpo yao.
Sisemi kwa mmoja mojanazungumzia kwa wote Wabunge wetu na Wawakilishi wetu wa .
Wabunge wetu naWawakilishi wetu wanapo hitajia kura za wananchi katika majimbo, huwa hawatokikatika majimbo yao ili kuwabembeleza wananchi wawachaguwe na kuahidi ahadi kem kem.
Lakini pindipo wakicha uvuga mtehani huu kuchaguliwa nakupewa ridhaa za wananchi , Baasi hukimbia kabisa katika jimbo lenyewe huwa mbali na watu wa jimbo lake,kifupi huwa haonekani tena ispokuwa baada ya miaka ya karibu na kampeni ndiohuja kujumuika na wananchi wa jimbo lake.
Wengine wamesikika wakisema ukiwa karibu na wananchi wajimbo lako basi kila siku utapokea matatizo na chida tu, bora uhamie mbali najimbo lako utaepukana na kero hizo.
Yani wananchi wako watakuona katika vikao vya Baraza nakukuskia katika redio na Televition tu.
Sasa utaratibu huu unatutia unyonge sana wananchi , hivisisi tukimchaguwa Mbunge na Muwakilishi wa Baraza la Uwakilishi ,Zamira yetu nikuwa mbali nae baada ya kwisha kumchagua?.
Au ni kujumuika na sisi wananchi wa jimbo lake ili kujakuskiliza matatizo yetu na kuyafanyia kazi au kuyapeleka katika vyombe husika?.
Sisi wananchi tuna kuwa na matatizo mengi yakijamii lakini tunashindwa wapi pakuyapeleka , Wabunge wetu na Wajumbe wetu wa Barazahutukimbia na huko wanako ishi ni masafa na inakuwa wao huwezi kuwafikia (unteachables) Nyumba yenye Security Gate ndani muna mbwa 2 wakali naMlizi na hata ukenda kuliza kutaka kuonana na Mbunge wako unambiwa hayupo auyuko busseys.
Na akitoka basi hutoka na Gari lake la kifahari tena lenyevioo vya tinted, hii inasababisha sana wananchi kuchanganyikiwa na matatizowalionaya na kujihisi Serekali chini ya watendaji wake imewaacha mkono wananchikutatua matatizo yao na hata kuchindwa kupata maelekezo na msada wa mawazo.
Kwa hio tunaiomba serekali yetu ipitishe sharia ya kuwalazimicha Wabunge naWawakilishi waweke utaratibu maalum wa juma la wiki au mwezi kuwa na siku 1au 2kuweko katika jimbo lao na kusikilizavilio tu vya wananchi wao ili kuvichukuwa na kuvipeleka Sehemu husika kamakatika Bunge au Baraza la Wawakilishi.
Sio watukimbie na kutupiga chenga baada ya kwisha kuwaparidhaa zetu , kufanya hivyo ndio kunakosababisha wananchi kutokuwa na imani naSerekali yetu na viongozi wake ambao ndio watendaji wakuu wa serekali katikajamii yetu.
 
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
858
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
858 0
Serekali ifanye utaratibu wa kupitisha sheria ya wabunge na Wawakilishi kuwa karibu mno ya wananchi wao ili kusikiliza shida zao sio kuwakwepa na kuwakimbia kwa kuwa mbali nao na kwenda kujenga katika sehemu za kifahari ili kukimbia matatizo ya wananchi.
 

Forum statistics

Threads 1,402,724
Members 530,976
Posts 34,403,460
Top