Barua kwa mzungu

Jajojo

Senior Member
Sep 1, 2015
155
95
Mpendwa Mzungu,
Jambo!

Kwanza- ulisema tuvae makoti kwetu kwenye joto kari, tumekubali bila kuuliza swali.

Pili- Umesema tuseme lugha yako na kujiona wa maana sana tukisema lugha yako, tudhalau lugha zetu tumetii tunafanya hivyo.

Tatu- Umehakikisha ukija kwetu tukunyenyekee sana na kukuheshimu, chochote ukisema tufuate, tumenyosha mikono juu kabisaaa ,tumekubali na hatukuulizi swali.

Nne- Umesema tuvae tie shingoni, tumekubali kabisaaaa.

Tano- Umefanya dada zetu wajidhalau rangi zao na nywele zao natural na kutaka kuwa kama wewe. wametii na kukufuata kwa moyo wote.

Sita- Umesema dada zetu wavae nguo fupi, badala ya nguo za heshima, wametii.

Saba- Unasema vijana wetu watoboe masikio na kuvaa heleni, wavae suluhali matakoni, tumekubali na tunafanya hivyo.

Nane- Umesema acheni kukutana na kubalishana mawazo, bali angalia TV/smart phone tu. tumetii na tumekubali.

Mwisho- Unasema sasa iwe haki mwanaume na mwanaume / wanawake na wanawake kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Kwa hilo hapana Mimi na wenzangu wengine tumekataa..

"hakuna matata"
Uwe na siku njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom