Barua Kwa Freeman Mbowe

Kutokuwa na chama hakumzuii mtu kuwa na mgombea wake wa urais ukichukua idadi ya wanachama wa vyama vyote na watu waliopiga kura utagundua wasio na vyama ni wengi kuliko wapiga kura.
Vyama vingi vina washabiki havina wanachama wasijidanganye na idadi ya wanaonunua kadi za uwanachama kwani wengi wao ama wamevutwa na mtu binafsi au maneno ya viongozi wa vyama lakini wengi hawajui sera wala itikadi za vyama vyao ndio maana kila siku tunasoma na kusikia watu wamehama vyama vyao.
Matatizo ya CCm yalianza pale walipoanza kugawa kadi kiholela badala ya mtindo ulikuwepo wa kutoa mafunzo ya miezi 3 na baadae kupewa mitihani mtindo huu ambao ulianzishwa na Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani umeendelea na utaenendelea kukigharimu chama tawala kwani ulibeba mamluki na watu walioingizwa kwa malengo maalumu(wanamtandao) na ndio iliyochangia CCM kufanya vibaya kwenye chaguzi za wabunge kwenye uchaguzi mkuu uliopita mkakatui uliotengenezwa mahsusi na aliyekuwa katibu mkuu Makamba.
Nawashauri pamoja na kampeni wanazoendesha cdm na kupata wanachama wangewafundisha wajue nini itakadi na sera za cdm ili wawe tayari kuzieneza na kuzitekeleza bila hivyo yatawakuta yaliyowakuta ccm sasa hivi wanaweza kujikuta wanapokea watu ambao wameingia kwa nia fulani ambayo si nzuri kwa chama chao
 
na jitihada zote za mbowe kukijenga chama asigombee?
Kwani mtu kuwa kijana ni dhambi au udhaifu?
Mbowe ana mchango mkubwa sana kuliko mtu mwingine yeyote chadema.
Ana haki ya kugombea kama wanachama wengine.
Acha kura za wanachama ndio ziamue.
Siyo lazima kila aliye fanya jitihada kukijenga chama chake finally apewe fursa ya kugombea URAIS. Mbona MZEE KAWAWA(MUNGU AMREHEMU) pamoja na kukitumikia cha kwa uadilifu mkubwa hakupata kuomba apendekezwe kugombea urais?
 
Zitto atasema chadema ni ya wakristo ili agombee yeye,same way JK alivyopata madaraka,nimeisema kwa njia nyingine na mod unayefuatilia mabandiko yangu,ifute na hii ukitaka.

Huwa nashindwa kuwaelewa mnaomtaja Zitto ns Urais. Mnataka agombee lini? 2015 au 2020? Na kwa Katiba ipi?
 
Binafsi nakubaliana na barua yako, na imesimama wima, lakini nigusie hapo kwenye siri nzito za Zitto na Makamba juu ya mkakati wa kuimaliza chadema, naamini hii sio siri kwakuwa kila mwanachadema hilo analitambua wazi, labda kigeni hapa ni mbinu mpya wanazobuni kufanikisha mpango huu maana mpaka sasa juhudi zao zimekwama chini ya usimamizi wa Jakaya Kikwete na ufadhiri wa Yusuf Manji wa Bilioni moja.
 
Achana na siasa chafu yaani mijitu mingine haimwogopi Mungu kwa kuleta unafki,umbea na majungu dhidi ya wenzao wewe unayejita honorable mp nahisi harufu ya makazi yako motoni
 
Barua imekaa vizuri. Mlio karibu nae mpelekeeni. Mbowe ni muelewa. Kuongoza vichwa lazima uwe kichwa, ila la Urais amwachie tu Mzee wa watu kwa sasa
 
Dr. Slaa ndio anakubalika sana pia hata kamanda Mbowe naye pia anafaa lakini the so called Zitto hafai koz ni mwanaCCM original na ni disaster kwa chama na Taifa.

Mwana ccm kama nape kweli tunatofautiana kwenye ufikili mwl wako alipata tabu xana.
 
Mh. Mbowe,
Kila mtanzania anafahamu kwamba unatamani sana kuwa rais. Kumbuka mwaka 2010 kabla ya CHADEMA kumsimamisha Dr. Slaa kuwa mgombea wa urais, vijana wachache sana walikiunga cchadema mkono. Lakini baada ya kumsimamisha Dr. Salaa, Tanzania ililipuka kwa shangwe na nderemo. Muda unavyokwenda ndivyo CHADEMA inavyozidi kupaa kwani Dr. Slaa anaaminika kwa machungu aliyonayo kwa taifa letu. Dr. Slaa ndiye Nyerere aliyebaki katika hii taifa

Nikiwa mwana CCM anayeiombea mema CHADEMA, na ambaye anajitayarisha kujiunga na ukombozi kabla ya 2015, nakusihi usijaribu kugombea urais 2015. Endeleeni kujenga chama, mwacheni Dr. Slaa agombee. Waambie mamluki kama Zitto na Shibuda wana CCM wenzangu watulie. Wewe bado kijana, tulia mwachie Dr. Slaa alikomboe taifa. Kwani yeye ndio mhimili wa upinzani hapa nchini. Mkifanya kosa kukurupuka na mambo ya urais kama mwana CCM Zitto, utashangaa CHADEMA itakavyo pukutika. Gombea Urais 2020 au 2025

Kuna kundi la vijana mahiri na wataalamu wa hali ya juu Ulaya na marekani ambao wanajipanga kuisaidia CHADEMA ikiwa Dr. Slaa atasimamishwa. Na watu kama Samwel Sitta wanaodahi kwamba CHADEMA haina watu wanaoweza kuongoza serikali, watashangaa mfuriko wa vijana toka Marekani na ulaya pamoja na waliopo nyumbani wakiongozwa na wewe pamoja na Dr. slaa watakavyoibadilisha sura ya Tanzania. Endeleza harakati bila kukiangalia kiti cha urais. waache wakina zitto waendelezo ndoto na tamaa zao za kibinafsi na za madaraka

NB: Kuna siri nzito nitawamwagieni humu siku chache zijazo. Ila kwa sasa, kuweni makini na January Makamba pamoja na Zitto. Kuna mpango maalum wa kuwatumia kukimaliza CHADEMA

Nikushukuru kwa barua.
Ninauhakika mh mbowe ni mtu anayependa $mabadiliko na siyo madaraka kama kibaraka zitto, mh mbowe hawezi kukurupuka katilka swala hili, nijuavyo mimi ama nionavyo mimi waziri mkuu wetu atakuwa mbowe na anafaa kwasasa katika nafasi hiyo.


Dr slaa ndiye chaguo la watanzania kwasasa na ndiye kimbilio la wengi kwasasa, wala usipate shida kuhusu zitto na genge lake ambalo soon linapotea kisiasa. January anachofanya kwasasa ni ahsante ya unaibu waziri wala mipango hana, uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana kuliko wapambe wake wanavyodhani.

Mbowe kwasasa aendelee kuisimamisha chadema kwani tunajua bila yeye chadema isingesimama kama ilivyosimama sasa, na kama kuna mtu ambaye ccm inamuombea mabaya ni yeye.
 
Usitufanye watoto wewe,sisi watu wazima na akili zetu usitake kututoa nje ya mada Slaa ndio kila so usitutake kuwafanya watu wachange mawazo yao,najuwa SlaA anawachachafya sana ndio maana hamlali so usituletee pumba zako hapa tuna msimamo na tunajuwa tunachofanya.....kama unampenda Mbowe mchague mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

haya ngoja tusubiri mporaji wa wake za watu alietelekeza familia aliongoze taifa.
 
Siyo lazima kila aliye fanya jitihada kukijenga chama chake finally apewe fursa ya kugombea URAIS. Mbona MZEE KAWAWA(MUNGU AMREHEMU) pamoja na kukitumikia cha kwa uadilifu mkubwa hakupata kuomba apendekezwe kugombea urais?

kawawa hakuwahi kuomba kugombea lakini mbowe amegombea mara mbili,hiyo ndio tofauti kubwa,mfano wako haukustahili kutumika hapa
 
Duuuu. Hakika unataka kutufanya hatuijui Marekani wala UK. Haya, tuambie hawa wataalam wanaojipanga kuja kuisadia Chadema wako kona zipi na wanafanya nini? Hivi umewahi kuhudhuria mikutano ya Chadema Marekani na UK? Kwa ufupi, Tanzania hakuna upinzani, ni njaa tupu. Dr Slaa ni dhaifu kuliko hata huyo Mbowe. Kwa kawaida, Mkatoliki yeyote anaekiuka kiapo cha upadri, huwa kama kichaa tu. mwacheni Mbowe

Aisee kweli wewe ni mchambuzi wa siasa 'mzuri'! Kweli hakuna upinzani na Slaa ni 'dhaifu', sasa washauri magamba waache kukosa usingizi maana hakuna upinzani na yule wanaye muona tishio ni dhaifu.
 
na jitihada zote za mbowe kukijenga chama asigombee?
Kwani mtu kuwa kijana ni dhambi au udhaifu?
Mbowe ana mchango mkubwa sana kuliko mtu mwingine yeyote chadema.
Ana haki ya kugombea kama wanachama wengine.
Acha kura za wanachama ndio ziamue.

kukijenga chama ndo alipwe kugombea? Mi nadhani tuliache kwanza, tuendelee kukijenga chama kata zote za tanzania
 
Mleta mada amewakurupusha na ninyi mmekurupuka.Mbowe hajatoa tamko lolote la kutaka kugombea wala Slaa hajaweka msimamo thabiti wa kutogombea."siongozi genge la wasaka madaraka"Naomba mnijuze huyu Zitto atakuwa na umri gani kufikia 2015?au katiba imeshabadilishwa kufuatia maoni yake na mlafi mwenzie Makamba?Ni muda wa kujenga chama si kuangalia nani awe nani ktk nini,huu urais wa kwenye mitandao unawavimbisha vichwa
 
Mbowe hawezi kuacha, tunwajua mnatumiwa na dr slaa kumkatisha mbowe tamaa ili asigombee, wajinga ndo wataunga mkono.
bila mbowe cdm isingefika hapa na dr slaa hashindi kura za maoni ng'o
 
Mbowe hajafaa kuwa rais. Kama anashindwa kuendesha ofisi yake tu ndogo ya gazeti la tanzania daima na ofisi nyingine moshi ambayo imemshinda hadi kaifunga kwa kuwa alikuwa halipi mishahara watu wakaacha. Kwa haya machache tu mbowe hafai hata kidogo kuwa rais. Na mengi sana ya mbowe ambayo yanaonyesha udhaifu wake wa kutoweza kuendesha mambo ila kwa sasa namhifadhi. Abadilike kwani hata ubunge siku sio nyingi viatu vitampwaya na ataweka matambara. Mbowe badilika mwachie slaa walau anaweza japo kuwa na yeye anasfa nyingi sana.
Naona umeminiwa thanks nyingi sana kwa kauli zako hizi za busara.
 
Mbunge Mheshimwa,
Nimeisoma barua yako kwa mheshimiwa Mbowe. Kitu pekee kilichonijia kichwani ni kwamba ndani ya CCM kuna obsession kubwa sana na Mbowe kuliko kiongozi mwingine yeyote wa Chadema. Ndiyo maana wanakimbilia kumbeza. Kama Mbowe si chochote na si lolote katika siasa za Tanzania sioni kwa nini ndani ya CCM watu wengi wanahara kwa sababu yake. Uamuzi wa kugombea au kutogombea utakuwa ni uamuzi wa ndani ya chama. Hauhitaji mtu wa nje, kama wewe mheshimiwa mbunge, kuutolea ushauri ingawa una haki ya kutoa maoni yako. Najua watu kama Januari wanatuita sisi wafuasi wa Chadema kuwa "brainwashed." Lakini najua hii ni kwa sababu ya arrogance yake ya kuamini kuwa CCM itatawala milele. Na sisi ndani ya Chadema tunajua mchango wa Freeman na ufasini wa kukifikisha chama hapa kilipo. Wakati utawadia watu ndani ya Chadema tutaamua ni nani anafaa kushika kijiti cha mbio za urais, lakini kabla ya hapo, tunashukuru na kuthamini mchango wa Freeman Mbowe katika ujenzi na uimarishaji wa chama.
 
Muda wa kuongelea urais si huu, chapeni kazi kwanza kwa kukujenga chama, msaliti atajionyesha mwenyewe mbele ya safari, yeyote aweza kuwa rais kupitia chama cha chadema
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom