Mheshimiwa mbunge, mimi sio Mbowe lakini wacha nikupe hekima. Chadema hakikujizolea umaarufu kupitia Mh Slaa, umekosea. Chama hiki kimekonga nyoyo za watanzania kwa kuwa kimekuwa kikijipambanua kutetea wanyonge na kutaka maliasili za Tanzania ziwanufaishe watanzania kama wewe.
Chadema ni chama na wala Slaa sio Chadema ni mwanachama kama wewe. Anao uzoefu wa kutosha kupanga vijana wetu makamanda na anayo busara na huruma kwa walalahoi wasiojua kesho serikali yao itaibuka na madudu hepi.
Lakini elewa kwamba Chadema haina utaratibu kama unaoutaka wewe, ni demokrasia ndio itachukua mkondo kusema nani asimame 2015. Hata Zitto akisimama binafsi sioni tatizo kwa kuwa hata wewe nina imani huna ushahidi kwamba nguli huyu ni mamluki. Najua hashiriki sana harakati za M4C lakini haitoshi kuropoka uzushi kama wako kwamba ni pandikizi, la CCM.
Sina hakika ni jeshi lipi utakalojiunga nalo kabla ya 2015 kwa kuwa nakuona hujui ulisemalo. Subiri siku nchi hii ikiwa hovyo usivyodhani then njoo humu uhare hivyo.
Uhuru una mipaka. Kila mtu akiamka asubuhi hupiga mswaki kuondoa harufu mbaya mdomoni kabla ya lolote. Nadhani uzi huu umeuandika baada ya usingizi mzito na kabla ya whitedent ama ni viroba at work.
Saidia chadema, achana na urais, sil wakati wake.
G Kassanga
Tabora.