Barua Kwa Freeman Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua Kwa Freeman Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Sep 1, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mh. Mbowe,

  Kila mtanzania anafahamu kwamba unatamani sana kuwa rais. Kumbuka mwaka 2010 kabla ya CHADEMA kumsimamisha Dr. Slaa kuwa mgombea wa urais, vijana wachache sana walikiunga cchadema mkono. Lakini baada ya kumsimamisha Dr. Salaa, Tanzania ililipuka kwa shangwe na nderemo. Muda unavyokwenda ndivyo CHADEMA inavyozidi kupaa kwani Dr. Slaa anaaminika kwa machungu aliyonayo kwa taifa letu. Dr. Slaa ndiye Nyerere aliyebaki katika hii taifa

  Nikiwa mwana CCM anayeiombea mema CHADEMA, na ambaye anajitayarisha kujiunga na ukombozi kabla ya 2015, nakusihi usijaribu kugombea urais 2015. Endeleeni kujenga chama, mwacheni Dr. Slaa agombee. Waambie mamluki kama Zitto na Shibuda wana CCM wenzangu watulie. Wewe bado kijana, tulia mwachie Dr. Slaa alikomboe taifa. Kwani yeye ndio mhimili wa upinzani hapa nchini. Mkifanya kosa kukurupuka na mambo ya urais kama mwana CCM Zitto, utashangaa CHADEMA itakavyo pukutika. Gombea Urais 2020 au 2025

  Kuna kundi la vijana mahiri na wataalamu wa hali ya juu Ulaya na marekani ambao wanajipanga kuisaidia CHADEMA ikiwa Dr. Slaa atasimamishwa. Na watu kama Samwel Sitta wanaodahi kwamba CHADEMA haina watu wanaoweza kuongoza serikali, watashangaa mfuriko wa vijana toka Marekani na ulaya pamoja na waliopo nyumbani wakiongozwa na wewe pamoja na Dr. slaa watakavyoibadilisha sura ya Tanzania. Endeleza harakati bila kukiangalia kiti cha urais. waache wakina zitto waendelezo ndoto na tamaa zao za kibinafsi na za madaraka

  NB: Kuna siri nzito nitawamwagieni humu siku chache zijazo. Ila kwa sasa, kuweni makini na January Makamba pamoja na Zitto. Kuna mpango maalum wa kuwatumia kukimaliza CHADEMA

   
 2. peri

  peri JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  na jitihada zote za mbowe kukijenga chama asigombee?
  Kwani mtu kuwa kijana ni dhambi au udhaifu?
  Mbowe ana mchango mkubwa sana kuliko mtu mwingine yeyote chadema.
  Ana haki ya kugombea kama wanachama wengine.
  Acha kura za wanachama ndio ziamue.
   
 3. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu uvae Gwanda hata Kesho...
   
 4. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mmmmmh............wenye maoni muandike tusome please
   
 5. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  slaa wetu raisi wetu
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda sana hii bahati nzuri, naujua msimamo wa Dr. Slaa kuhusu kugombea urais kwa 2015!.

  Japo mimi sina chama, nazi appreciate sana juhudi za Chadema kutupeleka kwenye ule ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania ile 2015!.

  Natofautia na wewe kwa hoja moja tuu, kwa vile Chadema ni chama cha kidemokrasia kwa maneno na matendo, lazima kiache milango yake wazi, kwa yoyote mwenye sifa, kugombea nafasi yoyote, atakaonekana is the best ndiye apeperushe bendera ya Chadema na sio kuanza mizengwe ya ki CCM CCM!.

  Japo mimi sina chama, mgombea wangu kwa CCM ni EL, kwa Chadema ni Zitto kwa sababu msimamo wa Dr, naujua!.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mbowe hapo hawezi kusikiliza. Kashainvest sana kwenye Urais. Slaa anategemea kuokota dodo chini ya mnazi.
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  kuna kaukweli hapa aisee
   
 9. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Samahani sana. Mh. Mbowe akifanya kosa kwa tamaa za madaraka, basi amekwisha na chama chake pia kimekwisha. Zitto na kundi fulani wanajipanga sana dhidi ya mbowe. yaani kila wiki wana kikao na viongozi wa CCM
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kila penye hoja za maana lazima ukurupuke kuja kuvuruga.CDM iachie wana CDM.Ninaloweza kukuhakikishia tutamsimamisha yeyote kugombea Urais,iwe ni shujaa Slaa ama Kamanda Mbowe au yeyote yule lakini katu asilani nakuapia CDM haitasimamisha Kibaraka yeyote wa CCM kugombea.All Shibuda type have been Banned.
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu tutobolee hiyo mipango inayofanywa na vibaraka wa ccm walioko CDM.
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama wananchi wanamsikiliza Slaa, basi watamsikiliza akiwaambia wamchague Mbowe au other CHADEMA candidate.
  Umemfananisha Slaa na Nyerere. Nyerere alisikilizwa na kumuokoa Mkapa na CCM mwaka 1995, Slaa naye anaweza kusikilizwa hata kama yeye siyo mgombea.
   
 13. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Chadema ni maarufu kuliko Slaa , kama Dr. Slaa angegombea kupitia UPDP angepata kura alizopata? kama mnajenga chama mnatakiwa muamini katika Demokrasia, Chama chenu ni Maarufu kuliko mtu binafsi acheni Demokrasia ichukue mkondo wake, Matokeo mliyopata 2010 ni matokeo ya kimkakati ya muda mrefu sio ubingwa au weledi wa kujieleza jukwaani pekee, msikipeleke chama chenu kikawa kama Sole Proprietor ikitegemea mtu mmoja kama vile NCCR au TLP, Statement za Sitta si uropokaji ni Technics za kisiasa na moja ya matokeo ya muda mfupi ni huu uzi uloanzishwa. Kukubalika/kutokukubalika kutaonekana kwenye uteuzi wa chama chake msianze kuleta mawazo ya kifalme, Yule ni binadam kama wengine chochote chaweza kutokea kabla ya 2015.
   
 14. M

  Mangare1 Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbowe hajafaa kuwa rais. Kama anashindwa kuendesha ofisi yake tu ndogo ya gazeti la tanzania daima na ofisi nyingine moshi ambayo imemshinda hadi kaifunga kwa kuwa alikuwa halipi mishahara watu wakaacha. Kwa haya machache tu mbowe hafai hata kidogo kuwa rais. Na mengi sana ya mbowe ambayo yanaonyesha udhaifu wake wa kutoweza kuendesha mambo ila kwa sasa namhifadhi. Abadilike kwani hata ubunge siku sio nyingi viatu vitampwaya na ataweka matambara. Mbowe badilika mwachie slaa walau anaweza japo kuwa na yeye anasfa nyingi sana.
   
 15. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa misingi ya demokrasia ndio.Ila kuutwaa madaraka zaidi na kwa ajili ya baadae, asithubutu. Mbowe bado mchanga sana. na udhaifu wake ni mkubwa mno. CCM wameshayaweka madhaifu yake pamoja na watamshugulikia. Slaa ndio tishio kwao, kila mwanya waliojaribu kaziba. Hawana jinsi ila kumkubali kama rais wao 2015... Vinginevyo Lowassa anakwend a magogoni
   
 16. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kuna watu huwa hawawezi kutoa comment bila kuandika "ingawa sina chama"!
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Watu wa namna hiyo ni wanafiki wakubwa..
   
 18. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa si useme hiyo mikakati ipi ya kikao? Angalia zisiwe udaku tu!! Halaf nahis wewe kma "PhiriKunjomba"
   
 19. data

  data JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,801
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  CHADEMA hawana mtu wa kumsimamisha kugombea URAISI... labda wawaonge MAJEMEDARI WA CCM...wahamie kwao.. Na hawawezi.
   
 20. Unkolonized

  Unkolonized Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno! But Dr. Slaa ndo kaifikisha CDM mahali ilipo coz ana msisimuko flan as if MTUME wa kuja kulikomboa Taifa hili! Mbowe was there there b4 Dr. Slaa but hakukuwa na msisimko kama alouleta Dr. Slaa 2010! Je, unaamini hilo?
   
Loading...