Kwenye kukigawa Chama hapo kina point. Kama hawatakata rufaa na Lema akawa amezuiwa kuna dalili za kukigawa Chama.Hapa hakuna dawa nyingine, zaidi ya kukata rufaa. Lazima tuone HAKI inatendeka. Afadhari jimbo libaliki wazi kwa mwaka moja(wote tukose kuwa na Mbunge) kuliko kukimbilia uchaguzi huki tukikigawa chama. Kura 56,000 alizopata Lema ni nyingi sana. Hatua ya kwanza iwe ni kulinda HAKI ya wapiga kura hao wengi.
Tafadhari sana ndugu zanguni, hapa kitu cha kwanza kabisa ni kukata RUFAA.
Time Limitation ya rufaa: Rufaa ya uchaguzi inatakiwa isikilizwe ndani ya mwaka moja. Mwaka huo mmoja utaisha kabla ya 2015. Lazima tuwe principled ktk kulinda na kutetea HAKI, kuliko kukimbilia uchaguzi.
Note well: Tukumbuke kuwa hii HUKUMU isipotenguliwa na mahakama ya juu, basi itakuwa PRECEDENT ambayo itatumikaa kung'oa wabunge wengi wa upinzani hapo baadaye.
Poleni sana, naona. Chadema mna mawazo. Mkate rufaa msikate yote tisa. Kumi ni kuwashawishi wananchi aw Arusha, mmechangia ni ni katika maendeleo ya Arusha tangu Lema achaguliwe Zanzibar ya fujo na mauajiq. Hata madiwani went hawafanyi kazi yeyote, mchaguliwe tena kwa shughuli gani fujo! Msifikri CCM inafanana makos a kila siku kisha ni nyi mfaidi,Kama mlivyofaidi Arumeru kutokana na makosa ya uteuzii. Ole wenu na kujeadili jiwe. People's itageuka ,kuwa popos.
Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.
Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.
Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?
Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?
Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.
CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.
Kwa kuongezea tu na kwa msisitizo mkubwa kwako Mh Dr.Slaa...kama unasoma huu ujumbe...please please......kesi hii ina mambo mengi kwani hata kama hamtakata rufaa na mkaamua kumsimamisha Lema...bado kutakuwa na mizenge tele ya delaying tactics.....USHAURI KWAKO DR.SLAA...TAFADHALI WAKUSIMAMISHE WEWE UGOMBEE UBUNGE ARUSHA.CHADEMA WASIMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA ZAIDI YA DR.SLAA.IKUMBUKWE KUWA ARUSHA INA MATATIZO MENGI YA MADIWANI AMBAYO HAYAJAPATIWA UFUMBUZI......PIA ARUSHA NI JIMBO KUBWA TZ.....NA NDIO MAANA CCM WANALITAKA...HASWA JK....HIVYO ASIMAME DR.SLAA MWENYEWE ARUSHA ACHUKUE JIMBO TAFADHALI...ATASAIDIA KUONDOA MIGOGORO ARUSHA KWA KIPINDI HIKI MPAKA 2015....Ndugu Slaa,
Kwanza niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwako binafsi na kwa chama chako cha CHADEMA kwa mafanikio mliyoyapata kwa kipindi kifupi. Natambua kazi mnayoifanya ni nzito na ya hatari maana wengi wanatamani kuwa kama ninyi lakini wanaogopa kutangulia ila nyie mmesema mnatangulia wengine watawakuta mbele ya safari. Kwa hilo hongera sana.
Bila kupoteza muda kutaja mafanikio mliyoyapata naomba nijikite moja kwa moja kwenye kiini cha barua hii.
Kabla sijasahau naomba chama kisikate rufaa kwa kesi ya Lema.
Naomba nikukumbushe tu kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 CCM hawakutaka si tu nyie mshinde bali msiongeze wabunge wa kuchaguliwa. Utakumbuka matamshi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba alipowaambia wanachama wa CCM kwenda kutafuta sababu yeyote ile wafungue kesi kupinga ushindi wa wabunge wa Chadema na chama kitagharamia kesi? Yanayotokea sasa ni utekelezaji tumjiandae kwa makubwa.
Utekelezaji wa hukumu ya Lema ni mwanzo tu ya mipango mingi ya CCM kuihujumu Chadema. Mpango ulikuwa trh 1-4 washinde Arumeru Mashariki halafu trh 5-4 ushindi wa Lema utenguliwe na sherehe kubwa yakupongezana ilikuwa ifanyike weekend hii mjini Arusha. Najua hilo limeshindikana.
Hukumu ya kupinga ushindi wa Lema si kwamba Jaji kajichanganya ni mtego wa makusudi ili nyie mjichanganye waendelee na plan B,C. Lengo lao ni kuikamata Arusha kwa hali yeyote kwa vile wanajua fika hawawezi kuikamata kwa kutumia sanduku la kura, kwa hiyo njia iliyobaki ni kutumia mahakama na pingamizi. Narudia tena msikate rufaa.
Lema amehukumiwa kwa kifungu 108 ‘Illegal Campaign' kinachomruhusu kugombea lakini kwenye majumuisho ya hukumu imeandikwa kahukumiwa kwa kifungu 114 "Illegal Practice" kinachomuzuia kugombea kwa miaka 5. Wanataka mkate rufaa au muombe ku review case na hapo itacheleweshwa mwisho mtaambiwa muda ni mfupi wa kuitisha uchaguzi.
CCM imeanza kuhaha baada ya kuona hamna mpango wa kukata rufaa, wanachosubiri ni Lema ateuliwe kugombea wamuwekee pingamizi, believe me or not lazima ataondolewa hata kama mtakuwa na hukumu mkononi.
Ndugu Slaa, CCM wameshafanya kosa wanajishauri endapo waingie kwenye uchaguzi ama la. Ushauri wangu ni kuwa, whatever the case, nendeni kwenye uchaguzi hata kama Lema hatogombea najua mtapata mgombea mwingine makini. Kama chama kitaona Lema asigombee, apewe kazi makao makuu ya kukiimarisha chama, akusaidie kuzunguka nchi nzima hasa katika kuimarisha matawi tayari kwa uchaguzi wa ndani na wa serikali za mitaa.
Nawatakia mafanikio mema katika ukombozi, najua kadritaabu zinavyozidi ndivyo ukombozi unavyokaribia.
Luteni.
Spanner unachosema kina msingi endapo haki itapatikana mahakamani....lakini hoja ya msingi hapa ni kuwa inaonekana haki imepindishwa mahakamani kwa hukumu hii na hivyo msingi wa kuirudisha kesi hii mahakamani unakosekana....tayari mahakama kuu imeshaonesha kuwanyima haki raia waliomchagua Lema sasa kwanini utegemee haki ipatikane huko huko mahakamani????msingi wa hoja hapa ni kurudia uchaguzi ili hukumu itolewe na wananchi wenyewe......Ieleweke wanaonyimwa haki hapa si Lema bali wananchi waliomchagua Lema....ni hawahawa wananchi watakaotoa hukumu ya kesi hii kwa njia ya kura....Hoja ya polisi kutangaza matokeo ni sawa tu na hoja ya rufaa kukataliwa....hivyo hapa ni kupima probability....kwamba wapi haki inaonekana itatendeka??????????BADO NASISISTIZA CDM WASIKATE RUFAA BALI WARUDIE UCHAGUZI KWA KUMSIMAMISHA MTU MAKINI AMBAYE NI DR.SLAA......HII ITAKATA MZIZI WA HILA ZA CCM ARUSHA....BELIEVE ME..........Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.
Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.
Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?
Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?
Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.
CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.