Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,972
- 22,933
Kwema huko binti yangu!
Tumekukumbuka sana binti yetu, mimi na mama yako tumekuwa tukikuombea sana upate mtu sahihi wa kukuoa. Jana ulipotutumia ujumbe kwamba umepata mchumba tulifurahi sana, tuna endelea kukusisitiza uishi maisha yampendezayo Mungu, tumekulea vizuri tangu utoto hadi umekua ukapata kazi huko jijini Dar unakoishi sasa na umepata na mchumba huko.
Misoji sisi wazazi tunakuombea kwa Mungu ufanikiwe na kutimiza malengo uliyojiwekea.Tunakupa ushauri ukusaidie unapojiandaa kuelekea katika ndoa takatifu siku zijazo.
Acha Kujifanya Mke Wakati Wa Uchumba! usiende kufua nguo za mchumba wako , wala kutandika kitanda ama kumuandalia chochote nyumbani kwake
Vaa mavazi ya kuustili vyema mwili wako mnapokuwa peke yenu, kamwe Usithubutu kufungua miguu yako kwa ajili yake!
Tambua wewe ni wa thamani sana hata shetani analijua hilo
Jithamini na kujiheshimu, Je, hutambui jinsi bidhaa inavyozidi kuwa adimu, ndivyo inavyothaminiwa zaidi? Binti mfalme, mpe mchumba wako sababu ya kukutafuta kama hazina iliyofichwa. Sema hapana kwa ngono hadi usiku wa harusi yako.
Usipuuze sms ama simu zake, - mwache aanzishe mazungumzo. Usikatae zawadi zake- ila usimuombe zawadi. Mweke nje ya nyumba yako na wewe ukae mbali na nyumba yake.
Namalizia kwa kusisitiza "Acha Kujifanya mke wakati wa uchumba"
Wasalaam baba yako.