Barua inayowatesa Mangula na Membe hii hapa!

Kevela atakua na matatizo ya akili kweli kwani hawezi kutoa tuhuma zake bila kuihusisha CDM? Lakini amenisaidia kujua siri ya uteuzi wa Mangula na siasa za majitaka na kikabila zinazoendelea mkoa mpya wa Njombe.
Nashindwa kuamini kama kweli barua hiyo iliandikwa na mhitimu wa shahada ya pili(MBA) ya chuo kikuu cha D'salaam!
 
kuna watu wajinga, wana quote maelezo marefu bila sababu ya msingi
 
Usitudanganye hapa!!1
1. Lwenge ni Mwizi alifukuzwa TANROAD!!!
2.Alikamatwa na PCCB kwa Rushwa na hata leo anathuma za Rushwa hapo

Sasa Kama unakula naye endelea!!!!!!!!!!!!!

Imekuaje akateuliwa kuwa naibu waziri kwa uchafu wote huu?
 
Imekuaje akateuliwa kuwa naibu waziri kwa uchafu wote huu?
Mbona Chenge ,Badwel, bado wapo Bungeni ????


Akiwa katika ziara jimboni, Mheshimiwa Lwenge alikuwa akitoa hotuba akidai kuwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anamuandaa yeye Lwenge kuwa Waziri kamili kwani Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dr Magufuli hafai na haelewani na Mheshimiwa Rais (Dr. Jakaya M. Kikwete) kwa kuwa Dr Magufuli ni mgonjwa na maamuzi yake si makini ndio maana anabomoabomoa nyumba za watu hovyo. Hayo aliyasema akiwa katika kata ya Saja. Huku akidai kuwa Yono.S. Kevela aliondolewa katika kura za maoni 2010 na kuteuliwa yeye mtu wa tatu(3), akinituhumu kuwa mimi Yono S.Kevela sikuwaletea wananchi wajimbo la Njombe magharibi maendeleo na akiwaambia watu kuwa mimi ni mgonjwa wa akili, Ukweli ni kwamba kura ambazo nilimzidi katika kura za maoni zilikuwa zaidi ya kura mia tano (500) dhidi yake Mh Lwenge. Na amekuwa akijisifu kwamba yeye aliteuliwa na NEC na siyo wananchi
 
Imekuaje akateuliwa kuwa naibu waziri kwa uchafu wote huu?
Wote hawa walipewa pesa na Mangula na Mh Lwenge ili wawapatie wajumbe awape na kumpigia Nepchard Msigwa. Bahati nzuri TAKUKURU inawashikilia na kuwahoji Zawadi Mgani kwa tuhuma ya rushwa Tsh 360,000/= zilikuwa zinagawiwa kwa baadhi ya wajumbe nje ya mkutano na kwenye vyoo nabar bila ya kuandikishwa sehemu yeyote.wakati wanatoa hiyo rushwa walikuwa wanaelekezwa kuwa wamchague Nepchardi Msigwa siyo Yono Stanley Kevela na tayari alikuwa kwenye mtandao wa Mh Lwenge na kunichafua kuwa sifai kuwa NEC Taifa, alikuwa akinichafua Zawadi Mgani. Zawadi Mgani alipewa kazi ya kugawa pesa ya posho kwa wajumbe, kazi ambayo yeye hakutakiwa kuifanya kwani yeye si Katibu wa CCM Kata, Ila yeye na mjomba wake Richard Ngwale Diwani wa Ilembula Ndio waliopanga kuwa Zawadi Mgani ndiye agawe pesa za posho mtandao wa mheshimiwa Lwenge wakanichafua na kupinga nisipate NEC –Taifa. Na akatumia nafasi hiyo kutoa rushwa. Yote haya yaliyotendeka yalikuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi, baadhi ya vifungu vya kanuni vilivyo kiukwa ni:
 
Duh, halafu kunawehu wengine wanasema watanzaniabhatujasoma! Aa wapi! Mu amewqsilisha ndiko la phd hapa bila jasho!
 
akidai kuwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anamuandaa yeye Lwenge kuwa Waziri kamili kwani Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dr Magufuli hafai na haelewani na Mheshimiwa Rais (Dr. Jakaya M. Kikwete) kwa kuwa Dr Magufuli ni mgonjwa na maamuzi yake si makini ndio maana anabomoabomoa nyumba za watu hovyo.

Jamani haya maneno 100% yametoka mdomoni mwa JK???
Mbona mambo?!
 
barua ndefu pamoja na kilichoandikwa kinajirudiarudia tu mara kwa mara. Wenye chama (mangula) wakimkuza sijui ataenda wapi?, kesi ya tumbili kumpelekea nyani unadhani utaambulia nin?
 
Hivi barua kwa Katibu mkuu ilienda softcopy au alituma hard copy na kutuma nakala ya softcopy kwa JF?
 
Kama kweli hiyo 'barua' ni andiko genuine la Yono S Kevela, basi ningeuomba uongozi wa UDSM umnyang'anye hiyo Masters yake aliyopata hapo Mlimani. Aibu kwa Masters' degree holder kuandika kama form one.
 
Fanya utafiti usiwe Mvivu!!!
Barua hiyo imetoka katika gazt la mwananchi story ipo front page
Acha ushabiki

Kwani gazeti la mwananchi haliwezi kuandika ujinga,kuwa mkubwa wewe!CHADEMA na mambo yenu ya ujambazi(rushwa)wapi na wapi,rushwa ccm ndo mahala pake,kama CHADEMA ni wababe na wana matusi,basi na Mangula na Msigwa ni CHADEMA,sasa chadema tumekua,tuna makada wakubwa ndani ya chama cha mAgamba,NAPE upo,wanachama wetu hao(Mangula&Msigwa).poa eeh!
 
Bila shaka huyu KING COBRA ndiye Bwana YONO S. KEVELA

Hivyo ameamua kuweka malalamiko yake hapa kwa sababu hata NAPE ni mwanachama wa JF, na bila shaka na J. Kikwete pia ni mwanachama hapa hivyo ujumbe utamfikia tu.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Last edited by a moderator:
Mhhh . . . ! Mbona mimi sielewi! Ina maana huyo Yono hajui kama CCM ni chama cha rushwa? UVCCM rushwa! WAZAZI rushwa! Kina mama wa CCM ( SOPHIA LION) nao rushwa! Sasa anafikiri atashughulikiwa? Itakuwa yeye rushwa yake haikutosha! Akomae na kusoma tu!
 
Bila shaka huyu KING COBRA ndiye Bwana YONO S. KEVELA

Hivyo ameamua kuweka malalamiko yake hapa kwa sababu hata NAPE ni mwanachama wa JF, na bila shaka na J. Kikwete pia ni mwanachama hapa hivyo ujumbe utamfikia tu.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
Wote hawa walipewa pesa na Mangula na Mh Lwenge ili wawapatie wajumbe awape na kumpigia Nepchard Msigwa.Bahati nzuri TAKUKURU inawashikilia na kuwahoji Zawadi Mgani kwa tuhuma ya rushwa Tsh 360,000/= zilikuwa zinagawiwa kwa baadhi ya wajumbe nje ya mkutano na kwenye vyoo nabar bila ya kuandikishwa sehemu yeyote.wakati wanatoa hiyo rushwa walikuwa wanaelekezwa kuwa wamchague Nepchardi Msigwa siyo Yono Stanley Kevela na tayari alikuwa kwenye mtandao wa Mh Lwenge na kunichafua kuwa sifai kuwa NEC Taifa, alikuwa akinichafua Zawadi Mgani.

Zawadi Mgani alipewa kazi ya kugawa pesa ya posho kwa wajumbe, kazi ambayo yeye hakutakiwa kuifanya kwani yeye si Katibu wa CCM Kata, Ila yeye na mjomba wake Richard Ngwale Diwani wa IlembulaNdio waliopanga kuwa Zawadi Mgani ndiye agawe pesa za posho mtandao wa mheshimiwa Lwenge wakanichafua na kupinga nisipate NEC –Taifa. Na akatumia nafasi hiyo kutoa rushwa.

Yote haya yaliyotendeka yalikuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi, baadhi ya vifungu vya kanuni vilivyo kiukwa ni
 
Back
Top Bottom