SI KWELI Barua hii ya Ibenge kufukuzwa Azam imekaaje?

SI KWELI Barua hii ya Ibenge kufukuzwa Azam imekaaje?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu hii vipi?
1788013691842.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook kumekuwapo na barua inayosambaa na kudaiwa kuwa imetolewa na klabu ya mpira wa miguu ya Azam kumtimua kocha wake mkuu, Florent Ibenge na benchi lake la ufundi.

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa barua hiyo si halisi bali ni ya kughushi. Barua hiyo imebainika kuwa na makosa ya kiundishi mengi.

Aidha barua hiyo imesamambaa Agosti 29, 2026 huku ikiwa inaonesha kuwa ilichapishwa na kutolewa Agosti 23, 2026. Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa taarifa hiyo ya kughushi imehaririwa kutoka kwenye barua ya Septemba 3, 2024 wakati klabu hiyo ilipomfuta kazi kocha wake Youssuph Dabo.

Hata hivyo hakuna taarifa kamahiyo katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Azam Football Club.
Back
Top Bottom