comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, amewasili nchini humo kuchukua hatamu za uongozi, kufuatia kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh
Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani.
Wanadiplomasia walimtaka Barrow arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi
Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.
Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.
BBC Swahili