Barrick yatangaza rasmi kifo cha Acacia!. Acacia yakubali rasmi kununuliwa baada ya Barrick kuongeza dau!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,
Hatimaye huu mtanange wa Acacia kununuliwa na Barrick, hatimaye umefika mwisho leo, kwa Barrick kutoa tangazo la kuinunua Acacia, na Acacia kutoa tango la kukubali kununuliwa na Barrick.

Tangazo la Barrick la Kifo cha Acacia ni Hili
PRESS RELEASES
Recommended Final Offer For Acacia Mining Plc By Barrick Gold Corporation – July 19, 2019

Tangazo la Acacia kukubali kununuliwa na Barrick ni hili

Hii maana yake ni
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya Tano kwa kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Kabudi, Hongera Magufuli, Hongera Watanzania, ila kwenye makinikia, bado kuna lakini!.
Leo tupongezane kwanza, lakini tuzijadili baada ya kusainiwa makubaliano yenyewe!.
Paskali
 
Kwanza kuna mambo tukubaliane!

1. It was not a hostile take over.
2. Hakukuwa na PUSU.

Ni biashara ya kawaida kabisa ambapo Acacia angeweza kukataa na kupersue options nyingine!

Management, bord of directors wamehusishwa kutoka mwanzo mpaka mwisho.

Nini kilikufanya uwaaminishe watu kuwa ni hostile takeover na sijui ni PUSU!
Where did you get these things?
 
Back
Top Bottom