Barrick Gold yakaribia kufikia malengo yake Tanzania

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,599
2,000
Barrick Gold yakaribia kufikia malengo yake Tanzania.jpg


Kampuni ya kimataifa ya uchimbaji madini ya Barrick Gold imetangaza kuwa imezalisha dhahabu karibu wakia 500,000 kutoka kwenye migodi mitatu iliyopo Kaskazini mwa Tanzania, mwaka jana.

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya Barrick kushirikiana moja kwa moja na serikali ya Tanzania katika uzalishaji wa dhahabu.

Ushirikiano huo ulianzishwa mwaka 2019 ili kutatua mgogoro wa ulipaji kodi wa kampuni hiyo.

Mwaka 2017, kampuni hiyo ambayo ni mmiliki wa kampuni ya Acacia ambayo iliingia kwenye mzozo na serikali ya Tanzania juu ya usafirishwaji wa mchanga wa madini au makinikia, na mzozo hhuo uikuja kutokana na ukwepaji kodi na kuminya haki za binadamu.

Tangu taifa hilo litoe tamko kuwa Acacia haitaruhusiwa kuendelea na shughuli zake nchini humo , Barrick Gold ilitatua changamoto hiyo kwa kuchukua hisa zote za mgodi wa Acacia wenye thamani ya dola bilioni 1.2 .

Mahakama kuu ya Uigereza ilipitisha mkataba huo mwaka 2019.

Hivyo kwa sasa Tanzania ikawa inamiliki 50% kupitia kampuni yake ya Twiga na riba 16% kutoka kwa kampuni zote zinazoendeshwa na Barrick.

Vilevile kampuni hiyo ilikubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo.

Katika taarifa yake Barrick Gold imesema migodi hiyo ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano ililipa gawio la dola milioni 250 mwezi Oktoba 2020

Barrick Gold yakaribia kufikia malengo yake nchini  Tanzania.jpg


Taasisi hiyo baadae iliripoti kuwa kiasi cha dola milioni 800 zilitolewa kwenye kodi, vibali ,miundombinu ,mishahara na malipo ya wasambazaji kwa mwaka jana.

Mwaka jana, Tanzania iliripoti kuwa kuna ongezeko la usafirishaji wa dhahabu kwa zaidi ya asilimia 50 na hivyo taifa kupata dola bilioni 2.7 mpaka mwezi Julai.

Hii ikiwa inaweka ongezeko linalokaribia dola bilioni moja ukilinganisha na mwaka 2019.

Ongezeko la usafirishaji wa dhahabu ya Tanzania nje ya nchi inalifanya taifa hilo kuwa na mapato makubwa ya fedha za kigeni, na kuchukua nafasi ya utalii.

Kipato kutoka kwa wasafiri kimeshuka kufikia asilimia 25.8 mpaka dola bilioni 1.9 mwaka jana, na kufanya utalii kushuka kutokana na marufuku ya kimataifa ya kusafiri , kwa mujibu wa benki kuu ya taifa hilo.

Katika kampeni za urais mwezi Septemba, Rais Magufuli alisema serikali imepata mafanikio makubwa katika sekta ya madini , kutoka kwenye uchimbaji mkubwa wa madini taifa hilo lilifanikiwa kupata dola milioni 56.8 kwa mwaka mpaka ilipofika Mei,2020. Magufuli, ambaye aliibuka kuwa mshindi wa uchaguzi mwezi Oktoba 2020 ,alisema kipato kimeongezeka mara mbili ukilinganisha na 2016.

Serikali ya Tanzania, inaonekana kuwa haikuwa innafuata fedha za madini bali kutatua mzozo uliokuepo kwa muda mrefu kati ya serikali na wachimbaji wageni.

Utawala wa Magufuli- ulitaka kuona ajira zinatolewa kwa wazawa na kumaliza mgogoro wa ardhi.

Rais wa Barrick na mkurugenzi mkuu Mark Bristow alisema, "…malalamiko yaliyokuepo zamani yameweza kutatuliwa na lililobaki ni suala la ardhi." Raia wa taifa hilo wameajiriwa kwa 96% , alisema mchimbaji.

chanzo. Barrick Gold yakaribia kufikia malengo yake Tanzania - BBC News Swahili
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,252
2,000
Thamani ya dhahabu imepanda kwenye msimu huu wa corona virus kwa hiyo kampuni za kuchimba dhahabu zinapata fedha nyingi. Basi kodi utakuwa nyingi na kila mwenye hisa ataongeza hela zake.

Kuongezeka kwa uzalishaji sijui imeenda vipi maana mgodi ni uleule hakuna miundombinu iliyoongezwa. Labda wamezalisha zaidi kwa vile kuna uhitaji mkubwa au ufatiliaji wa serikali na uhusika wa Twiga umemsaidia.

Mapato ya dhahabu yalizidi yale ya utalii kwa sababu ya corona watalii hamna. Uchumi ukirudi sawa tunatarajia thamani ya dhahabu kupungua, ya mafuta kupanda na baada ya miaka 2 usafiri wa anga utarejea kiasi chake. Hapa dhahabu itarudi wastani wa bei yake, mafuta bei iwe kawaida ila utalii upande kwa vile watu wako bored na walizuiliwa kusafiri muda mrefu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom