Barrick Gold mining license renewed for 15 years

Hivi majuzi Muhongo alisema umeme wa mgawo ni wa kupanga,akiwa na maana tuna umeme toshelezi!Na kwamba mgawo ni mahususi kwa watu flani wenye kunufaika kwa kuwauzia TANESCO mafuta...Sasa kama Barrick nao wanasema ni gharama kubwa kuendesha shughuli kwasababu umeme ni wa mgawo(blackouts),na hivyo inabidi watumie diesel(costs more),jambo ambalo linasababisha waseme ni ghali sana kuendesha shghuli zao,unadhani nani anaathirika zaidi ya Taifa kama kweli Muhongo yuko right?

Kwanza tukikubaliana nao tu kwamba umeme ni shida,ujuwe kuwa kwenye kunegotiate nao terms za mikataba sisi tayari tuko kwenye disadvantage,achilia mbali tamaa za ten percent!
Hawa mawaziri wanaposema tuna umeme toshelezi sijui wanamaanisha nini?
MW1000 kwa watu milioni 40 ambao wapo scattered is almost nothing.

Mkoa wa Mara, au tuseme buhemba kuna ration gani kati ya hizo 1000? Angebainisha hilo, source ya huo umeme ni nini?, reliability ? Angeainisha hivyo vitu kwanza labda angeeleweka.

ila nakubaliana naye kuwa Coal imetupwa ili mafuta yatumike kuwanufaisha baadhi ya watu/vigogo otherwise, sijawahi kuona watu wajinga kama nishati .... short term solution kwa long term problem!! ndiyo madhara yake hayo.
unatumia Cofta kutibu kifua kikuu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
huwa nashangaa wanao amini ku copromise na CCM,hawa ni kuwatoa kwa nguvu tu! naomba wananchi wapate uelewa juu ya Tanzania ijayo!
 
Tarehe 23 november ndugu MUHONGO akiwa ARUSHA alisema baada ya leseni ya TANZANITE 1 kuisha serikali kupitia kwake aliamua umiliki wa shea za mgodi huo uwe ni 50% kwa mwekezaji na serikali 50% kupitia STAMICO na kwamba hizo 50% za wananchi kupitia STAMICO zitapewa au kuuzwa kwa wanachi kupitia DSE..

Wengi walimpongeza kwa hatua hiyo na kama zoezi la kuuza shea hizo litafanyika kwa uwazi zaidi.nimeona kwenye uzi huu kuwa masharti ya mkataba wa umiliki wa mgodi wa NYAMONGO utaendelea kama ulivyokuwa. swali ni je share zimekaaje katika mgodi huo?zilikuwa ni 50%/50% kabla ya kuhuisha SML tena?.

Kama si hivyo basi kutakuwa na doublestandards ktk maamuzi ya serikali..kila mara nimekuwa niki quote "NOTHING ABOUT US WITHOUT US"Dhahabu ni zetu kwa ajili yetu na watoto wetu. Kama watanzania lazima tuhakikishe mikataba mibovu isirudiwe tena
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ten percent cut (10%) as they normally do, binafsi nadhani kama nchi tumekwama katika tope zito na haiwezekani kuchomoka katika tope hilo pasipo kubadili mfumo wa utawala uliopo.

Sasa hivi ni miaka yapata hamsini toka tumepata uhuru hospitali zetu hakuna madawa, dawa feki zinaingizwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa za kisheria dhidi ya walanguzi hao na wanazidi kupewa nafasi za kisiasa.

V
iongozi wetu wanaficha mabilioni ughaibuni waliyokwapua baada ya kulangua rasilimali zetu,wanasiasa wanahangaika na kutumia muda mwingi kusifia maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu(rasilimali watu), mikataba kama ile aliyokuwa akiingia chief Mangungo wa Msovelo tunaishuhudia kwa kiwango cha hali ya juu na wanaotuingiza katika mikataba hiyo wamesoma kweli kweli.
 
Inauma kwasababu kelele za watanzania zimezoeleka, tunapiga kelele weeee alafu tunanyamaza wanaume wanaendelea na kuinyonya nchi
Ndiyo maana nimesema something must be done!
Hawa viongozi tulio nao hawajaonja nguvu ya wananchi hata siku moja. Something must be done wananchi.

Hizi kelele tunazopiga wameshazizoe ndio maana wanasema huo ni upepo.
Wanafahamu kuwa Watanzania hawana utamaduni wa kuwaadabisha viongozi wao! Something must be done!

Tatizo la umeme limekuwepo kuanzia Kikwete akiwa waziri wa nishati. Alipoingia madarakani alikuta tatizo ni kubwa.
Kwa miaka sita Rais Kikwete hana suluhu ya muda mfupi au muda mrefu. Amekaa pembeni wezi wakiwapora Watanzania kwa kupitia wizara ya nishati na Tanesco,IPTL aliyosaini, Richmond aliyoshirikiana na PM lowassa na madudu mengine.

Madudu yote yaliyofanywa na akina Lowasa,Karamagi, msabaha akina Mboma na juzi akina Mhando, juzi kumefichuliwa ufisadi wa kutosha, serikali imekaa kimya kana kwamba haina Viongozi.

Rais Kikwete anafahamu fika kuwa mgao ni njia ya kuuza mafuta achilia mbali majenereta.
Anafahamu kuwa bila nishati ya uhakika hakuna mwekezaji anayeweza kuchukua risk ya investment.
Kila kukicha yupo New york akigonga kengele za DOW JONES eti anatafuta wawekezaji.

Kama kuna kiongozi anayelitia taifa hili umasikini licha ya ule uliopo, historia haitakamilika endapo jina la Kikwete halitatajwa.
Rais amekaa kimya nchi inaporwa, kana kwamba nchi haina uongozi! something must be done.

Huko migodoni ni wizi tu na kuwaachia wananchi mashimo na mercury ili wafe taratibu.
Hakuna kiongozi anayeshtuka. Kikwete analiangamiza taifa hili.

Ujanja wa kutumia tume za kuchunguza umekwisha, sasa hivi wanatumia bunge kama kichaka cha kurahisisha masuala ya kitaifa ili wapate nafasi ya kupora huku wakirithisha watoto wao uporaji kule Uswiss. Something must be done dudes.

Watanzania muda wa kulalamika umekwisha sasa, hivi ni muda wa kutenda, hii nchi ni yetu si yao.
We must stand and do something! something must be done.

Tutawaachia watoto wetu umasikini kutokana na utajiri wa kundi dogo sana. Something must be done!

Tusiposimama na kuwapa ujumbe mahususi na wenye funzo, basi wake zetu na dada zetu wataendelea kujifungulia juu ya baiskeli na matenga. Tutaendelea kufa bila matibabu huku wake zao na familia zao wakitibiwa Appolo.
Watoto wetu watakatwa vitovu kwa kutumia chupa za soda huku wake zao wakitibiwa chunusi South Africa.

Watoto wetu wataishia kukaa katika mawe tukiambiwa shule za kata, watoto wao watasoma ng'ambo ili warudi kurithi viti vya baba zao.

Umasikini wetu si rasilimali, ni umasikini wa akili zetu zinazoamini wanachosema hawa waporaji.
Ufakara wa akili zetu unaotutuma tuamini kuwa Kusimamia rasilimali zetu ni kuvunja amani na utulivu.

Wenye amani na utulivu ni Serikali na Wabunge, wewe na mimi hatuna amani tuna woga!
Ni woga wetu umetufikisha mahali tunapowalipa mshahara ili wafanye kazi za kuteteana kwa hoja za kipuuzi bungeni na kwingineko.
Ni woga wetu nunaotufikisha hapa, ni woga unaotudhalilisha kiasi hiki.

Woga waliouita amani na utulivu unatutokea puani kila uchao huku tukiangalia ndugu zetu wakikata roho bila matibabu, watoto wakiwa wezi kwa kukosa elimu, wengine wakifanya umalaya ili kujikimu kwa dhiki.

Katika nchi tajiri kama Tanzania watu wa kulaumiwa si genge la serikali au wapiga soga bungeni, ni sisi wananchi kwasababu tumeshindwa kujitetea, kutetea nafsi zetu, kulinda rasilimali zetu na tumewapa haki na hati miliki ya nchi yetu.
Sisi ndio wa kulaumiwa si wao. Unless we do something these gangstars will treat us like dogs!

Something must be done! Watanzania something must be done now!
muda wa kulalama umekwisha sasa ni muda wa kutoa ujumbe kwa hawa wezi na kundi liwalindalo.

Something must be done!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
What next? The way forward pleaseee...mie nishachoka na manunguniko plus lawama za kila siku za watz...niambieni tufanye nini sasa?
 
hawa mawaziri wanaposema tuna umeme toshelezi sijui wanamaanisha nini?
Mw1000 kwa watu milioni 40 ambao wapo scattered is almost nothing.

Mkoa wa mara, au tuseme buhemba kuna ration gani kati ya hizo 1000? Angebainisha hilo, source ya huo umeme ni nini?, reliability ? Angeainisha hivyo vitu kwanza labda angeeleweka.

Ila nakubaliana naye kuwa coal imetupwa ili mafuta yatumike kuwanufaisha baadhi ya watu/vigogo otherwise, sijawahi kuona watu wajinga kama nishati .... Short term solution kwa long term problem!! Ndiyo madhara yake hayo.
unatumia cofta kutibu kifua kikuu.

mkuu hapo nilipo-bold in red nimepapenda sanaaa na umenifanya niwaelewe vizuri kabisaaaa hawa viongozi wetu wa wizara na uzuzu walionao...wanafurahia utamu wa cofta huku nchi ikiingia kaburini....

Tanzania ni yetu sote..hawa viongozi hata wakiweka mabilioni uswis na kuuza nchi yetu bado wajomba na babu zao tutakuwa nao hapa tanzania ...

Na wengine wanajenga mahekali huko msoga as if watakuwa wanaishi pepo yao wakizungukwa na jehanamu ya ndugu wajomba wapwa na mashemeji masikini wa kutupa....

Nimesahau...na ule msikiti tutakuwa tunaswali wote..kila siku tutakuwa tunamuibia viatu mpaka akome.
 
Nchi inakwisha kwa sababu yetu wenyewe,fisi wamekabidhiwa bucha na sisi wenyewe sasa tunalia nyama yetu wengine mifupa yetu. Jamani kazi ipo sana tu kama tunahitaji maendeleo ya kweli. Watanzania tuna tabia za ajabu sana mfano kunamatukio mengi sana ya kustaajabisha yamefanyika na viongozi wa nchi hii lakini hakuna hatua yeyote tulio chukua. Hata tungeambiwa tz inaingia mkataba na barrick wa miaka 1000 tungefanya nini? Viongozi wetu wanajua msitu ni ule ule miti ni ile ile na nyani ni walewale, watanzania ni wale wale na akili zao ni zile zile kuliwa na waliwe
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Uzi waenye tija kwa nchi yetu kama huu huwezi waona wakina , nchemba, nape, na vijana wake wa lumumba, au tutentemeke....
Nchi imekwisha tunaingalia tu!!
Nini kifanyike??
 
Nchi imekwisha tunaingalia tu!!
Nini kifanyike??

Kwanza kabisa namshukuru EMT kwa kuinasa hii habari.

Nini kifanyike? Hizi hizi pesa watakuja kuzinunua kura za baadhi yetu. Tusijidanganye kwamba tusubiri mpaka 2015
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hebu niulize, tulitaka wanyimwe?
Kwa kutumia sheria na taratibu zipi??
 
Ina maana zoezi hili limefanyika kimya kimya bila ya waandishi wa habari kukaribishwa? Mbona hatujaliona kwenye tanzania media houses!

Umesahau habari nyeti kuhusu Tanzania huwa hazitolewi na local media?

Unakumbuka ile habari ya mkataba wa kutengeza vitambulisho zilipatikana wapi kwa mara ya kwanza?

Naomba kutofautiana na nyie

Renewal of Prospeting Licences,mining licences, Special Mining Licences sidhani kama ni issue hivyo
Ukiangalia takwimu renewals kwa zinazopolewa kwa mwezi ni mamia kwa mamia

Sasa hii ingekuwa na utofauti gani?? Ukizingatia mwekezaji anaruhusiwa kuendelea na shughuli zake kama hajakiuka taratibu na kama hajazuiliwa na serikali

Mie nadhani kama tunataka kubadilika kwenye madini lazima sera na sheria ziwe za mantiki hasa uwazi wa mikataba ili wananchi wajue magodi husika una manufaa gani kwao.

Kwa sheria ya TZ ni haki ya mmiliki wa SML kupewa renewal kama katimiza vigezo na masharti, NI HAKI YAKE
 
Sikubaliani moja kwa moja hapa
Kila mtanzania anaweza kupata database ya wamiliki wote wa vitalu ya uchimbaji na taarifa zao kwa Dola 100 tu, hapa simaanishi mgodi unachimba kiasi gani, bali umiliki wao wa vitalu ukoje.

Ishu ni je, taarifa hizi tunazielewa? Tuzitumieje?
Mkuu ni kweli usemacho,na ninakuhakikishia,kama si kwasababu ya shareholders(wanabandika habari hizi ili kulinda mahusiano na shareholders) na ndiyo maana hizi habari zinapatikana,otherwise tusingekaa tujuwe.

Moja ni kwasababu ya shareholders,na pili ni kwasababu watanzania sasa wana access ya habari za mitandaoni.Ambazo kiukweli sisi si walengwa,lakini imetokea kuwa tunapata access kwasababu information iko aimed to share holders.

Otherwise tusingejuwa chochote kwasababu access to information kwa Tanzania ni almost zero,na hii ni kwa mujibu wa globalintergrity.org!
 
NEno!!!!!!!!!!!
Hatuna nguvu katika negotiation sijui kwa nini?

Afu madaraka ya waziri wa nishati nayo yapunguzwe
Maana akiingia kichaa pale ndo huwa anatajirika kwa siku 3

Lazima liwe zoezi shirikishi kwenye hii mikataba

Hivi majuzi Muhongo alisema umeme wa mgawo ni wa kupanga,akiwa na maana tuna umeme toshelezi!Na kwamba mgawo ni mahususi kwa watu flani wenye kunufaika kwa kuwauzia TANESCO mafuta...Sasa kama Barrick nao wanasema ni gharama kubwa kuendesha shughuli kwasababu umeme ni wa mgawo(blackouts),na hivyo inabidi watumie diesel(costs more),jambo ambalo linasababisha waseme ni ghali sana kuendesha shghuli zao,unadhani nani anaathirika zaidi ya Taifa kama kweli Muhongo yuko right?

Kwanza tukikubaliana nao tu kwamba umeme ni shida,ujuwe kuwa kwenye kunegotiate nao terms za mikataba sisi tayari tuko kwenye disadvantage,achilia mbali tamaa za ten percent!
 
Kila mtanzania anaweza kupata database ya wamiliki wote wa vitalu ya uchimbaji na taarifa zao kwa Dola 100 tu,
Hahahahaha, duh! Tumefikia hapa? I'm not asking for too much. For all I know, If it was a CCM political news it would be on front pages of all newspapers.

Go figure why when it's monetary things info is always kept secret and probably one has to pay to obtain info as if he wants to venture into the business
 
NEno!!!!!!!!!!!
Hatuna nguvu katika negotiation sijui kwa nini?
Sijui kwanini una maana gani wakati ushaelezwa tatizo ni umeme. Mwekezaji ataingiza gharama za umeme which he'll incur as a reason for discount

Tuboreshe umeme, no more mikataba siyo tu kustimulate foreign investment bali pia kwa domestic uses
 
Ukiona hivyo, jua siamini katika sababu ya umeme tu.

Lazima kuna lubricants mahali fulani zinazotulegeza ama kwa kujua ama kutojua

Sijui kwanini una maana gani wakati ushaelezwa tatizo ni umeme. Mwekezaji ataingiza gharama za umeme which he'll incur as a reason for discount

Tuboreshe umeme, no more mikataba siyo tu kustimulate foreign investment bali pia kwa domestic uses
 
Ukiona hivyo, jua siamini katika sababu ya umeme tu.

Lazima kuna lubricants mahali fulani zinazotulegeza ama kwa kujua ama kutojua

Ningekuwa na uwezo ningewashauri wanabodi wote walau tuteue siku moja tujadili suala la umeme. Ni muhimu sana. Uchimbaji unategemea umeme leo wewe unaona umeme haina umuhimu kwenye kulilia discount
 
Back
Top Bottom