Kwani matatizo ya umeme Bongo yameanza leo au jana? Mbona tangu walipoingia nchini tangu mwaka 2000 hawakuona kama ni tatizo hadi miaka 12 baadaye!? Hawa naona wamestukia agizo la kulipa kodi ya 30% lililotolewa na Waziri mpya wa Madini na Nishati Sospeter Muhongo.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ng-companies-to-pay-30-pct-corporate-tax.html
yawezekana kabisa wameshaona mawe hayatoshi tena, sasa wanataka kukwepa kulipa mafao yetu na kodi zetu. mie binafsi sijaona faida ya owepo wao hapa zaidi ya hasara ya kutuulia ndugu zetu na then kutuachia mashimo matupu.Mkuu Nakubaliana na wewe lakini kwa kuongezea huenda mawe yameanza kuisha wanawuzia wachina hayo mapango na hiyo mivifaa Yao tu
Wamestukia kuwa 2015 mgodi utakuwa hauuziki. Hivyo wameamua kuwaingiza mkenge Wachina ili waikimbie nguvu ya umma mapema.
Tunayo STAMICO, na inalipa watu kila mwezi. Sijui wanafanya kazi gani.
Labda sikusomeka vizuri. Nilichokusudia kusema ni kuwa kwanini serikali yetu inashindwa kuitumia STAMICO kuchimba haya madini badala yake wanawapa wezi kwa kisingizio cha wawekezaji? Mara nyingi kisingizio kimekuwa uwezo mdogo wa mtaji, lakini ukiwa na mali hii unashindwaje kukopa ili kupata mtaji huo unaouhitaji?Ndugu, huwatendei haki STAMICO. Taarifa zilizopo ni kwamba kabla hata Barick hawajauziwa huo mgodi, tayari ilikuwepo kampuni ya Kahama Gold Mine na bodi yake ya wakurugenzi. Lakini kwa ufisadi mgodi ukauzwa kinyemela kwa mwekezaji "mjanja" ambaye naye aliuuza kwa Barick kwa bei ya kufa mtu? Watanzania wenzangu tusilaumu tulipoangukia, tuangalie kwanza ni wapi tulipojikwaa.
Kwani matatizo ya umeme Bongo yameanza leo au jana? Mbona tangu walipoingia nchini tangu mwaka 2000 hawakuona kama ni tatizo hadi miaka 12 baadaye!? Hawa naona wamestukia agizo la kulipa kodi ya 30% lililotolewa na Waziri mpya wa Madini na Nishati Sospeter Muhongo.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ng-companies-to-pay-30-pct-corporate-tax.html
Kama wazungu wanafunga virago kwa sababu ya Umeme na wanasema hawawezi kulipia wafanyakazi wao michango ya NSSF je hawa wachina walivyo mabahili umeme watatoa wapi na pia wanajulikana kuwa huwa hawalipi michango ya mafao.
Katika hali ya kawaida ingekuwa nchi zilizoendelea au zenye nia ya kuendelea waziri wa uwezekaji kama Mary Nagu angekuwa anaenda mbio ili hawa jamaa wasiondoke lakini kama sikosei Mary Nagu atakuwa bize kutafuta misafara ya mikutano ya nje ya nchi ili apate per diem.
Ripple effect ya hawa jamaa kuondoka ni kubwa mno...imagine watu wangapi watakosa ajira, tazama supply chain yao locally ikoje, serikali pia itakosa mapato
Lakini kwa sababu sisi hayo sio muhim kwetu HILI NALO LITAPITA
Wachina mpaka leo hawajaleta ripoti ya mgodi waliopewa wa Kiwira.
kazi kwenu