Barrick Gold kuuzwa...

wimbi la mbele

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
647
Reaction score
269
Kama wazungu wanafunga virago kwa sababu ya Umeme na wanasema hawawezi kulipia wafanyakazi wao michango ya NSSF je hawa wachina walivyo mabahili umeme watatoa wapi na pia wanajulikana kuwa huwa hawalipi michango ya mafao.

Katika hali ya kawaida ingekuwa nchi zilizoendelea au zenye nia ya kuendelea waziri wa uwezekaji kama Mary Nagu angekuwa anaenda mbio ili hawa jamaa wasiondoke lakini kama sikosei Mary Nagu atakuwa bize kutafuta misafara ya mikutano ya nje ya nchi ili apate per diem.

Ripple effect ya hawa jamaa kuondoka ni kubwa mno...imagine watu wangapi watakosa ajira, tazama supply chain yao locally ikoje, serikali pia itakosa mapato

Lakini kwa sababu sisi hayo sio muhim kwetu HILI NALO LITAPITA

Wachina mpaka leo hawajaleta ripoti ya mgodi waliopewa wa Kiwira.

kazi kwenu
 
Mkuu Nakubaliana na wewe lakini kwa kuongezea huenda mawe yameanza kuisha wanawuzia wachina hayo mapango na hiyo mivifaa Yao tu
 
Mkuu Wachina hawa wa leo si sawa na wale wa mwaka 47, ninaamini lazima watafanya tathmini ya kina kuhakikisha hawauziwi mapango.

Mkuu Nakubaliana na wewe lakini kwa kuongezea huenda mawe yameanza kuisha wanawuzia wachina hayo mapango na hiyo mivifaa Yao tu
 
Au huko chini ya ardhi wamekwisha maliza hazina!?
 
Mary Nagu jimboni kwake wanaoga mara moja kwa wiki, ndoo moja ya maji ni 1500 halafu kuyapata mbinde sijui wamefanya nini yeye na Sumaye.
 
Upepo wa M4C unawaogopesha wanajua mwisho wa kutuibia umefika.
 
Lilipotokea agizo hilo (kutokana na kuwa walikuwa wanasamehewa kodi kwa miaka mitano) niliwahi kutoa hoja kuwa wawekezaji waliopo watakuwa wanauziana rasilimali zetu au kubadilisha majina ya kampuni muda mchache kabla ya kumaliza hiyo miaka ya msamaha wa kodi.

Hivi ndivyo wanavyotaka kufanya hawa Barrick na usishangae kuona bado wakiwa na hisa kwenye kampuni mpya itakayowarithi.

Hata hivyo ningefurahi kama wangefunga virago na kuondoka kabisa bila kuuza migodi.

Faida toka kwa wawekezaji wa madini nchini ni sawa sawa na 100-100x100= kwa upande wetu au 100x100-100 kwa upande wao.
 
Si waende zao watuachie wenyewe hiyo migodi?
 

TRA hawawezi kufanya kitu kama hakuna sheria inayotaka wakusanye kodi, sheria zetu ni dhaifu sana (kama ilivyo serikali) na mara nyingi wawekezaji wamezitumia kupiga madili ya kuzimu na kuondoka bila kulipa kodi yoyote

SAMAX walitengeneza mamilioni kwa kuuza mgodi wa Golden Pride kwa RESOLUTE miaka ya 90 na hata waliouuza mgodi wa Buli walipiga mihela ya kufa mtu na hawakulipa hata senti kwa serikali isipokuwa kifuta jasho kwa watendaji wa serikali waliokuwa wanawasaidia kupitisha sheria zinazowalinda
 
Hilo ndio neno! Hawa CCM wanatuibia kiuuwazi. Mhongo ni CDM huyooo!
 
watakuwa wamemaliza kila kitu ardhini wanataka kuuza mitambo yao tu,wanatudanganya eti umeme,au walikuwa hawalipii bili zao,tanesco wameshaanza mchakato wanahofia? tanesco wakagueni hao jamaa kabla hawajaondoka inawezekana walikuwa wanachakachua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…