Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Mnamo March 21, 2017 ICSID ilitoa maamuzi/ hukumu kwa kuipa ushindi kampuni ya Antofagasta plc na Barrick Gold Corporation katika shauri maarufu linalojulikana kwa jina la Reko Diq Arbitration Proceedings TORONTO .
Katika taarifa yake Barrick Gold Corporation (NYSE:ABX)(TSX:ABX) (“Barrick” or the “Company”) imeeleza kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya kibiashara ( Arbitration tribunal of the World Bank’s International Center for Settlement of Investment Disputes (“ICSID”) siku ya Tarehe 20 Machi,2017 ilitoa maamuzi kuhusu usuluhishi wa kampuni tanzu ya Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) iliyoundwa kwa Muungano kati ya Antofagasta plc na Barrick, dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan.
Mlalamikaji ambaye ni Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) alifungua shauri husika kutokana na Serikali ya Pakistan kutenda kinyume na sheria kwa kukataa kutoa leseni ya madini ili kuwezesha uendelezaji wa Mradi wa Reko Diq mwaka 2011. TCC ililalamikia kitendo cha Utawala wa jimbo la Balochistan kukataa kutoa kibali husika huku kampuni hiyo ikiwa imekwisha wekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya utafiti na upembuzi yakinifu wa mradi husika.
Mradi wa Reko Diq , unapatikana katika jimbo maarufu la Balochistan, na ulitegemewa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani bilioni 3 kama fedha za uwekezaji wa awali wa mradi husika . Reko Diq ni miongoni mwa eneo lenye utajiri mkubwa wa copper na dhahabu duniani ambalo bado halitaendelezwa, na utajiri wake unakadiriwa kuwa na uhai wa zaidi ya miaka 50.
Katika siku hiyo ya Maamuzi, ICSID tribunal ilikataa hoja za utetezi upande wa Serikali ya Pakistan , na kuthibitisha kwamba Pakistan ilikiuka vipengele mbalimbali vya sheria za Uwekezaji kati yake na Australia ambapo kampuni ya TCC imesajiliwa.
Hatua ya pili kuhusu fidia ilipangwa kuanza kusikilizwa Machi,22 ambapo Mahakama itapokea hoja za Maandishi kutoka pande zote na kuamua juu ya kiwango cha fidia kitakachopaswa kulipwa na Serikali ya Pakistan kwenda kwa kampuni ya TCC, huku hukumu ikipangwa kutolewa Mwaka 2018.
Wataalamu wa Uchumi na masuala ya madini wanakadiria kwamba Serikali ya Pakistan inaweza kuwajibika kulipa kiasi kikubwa zaidi cha fedha kutokana na ukiukwaji wa wazi wa Mikataba ya Uwekezaji.
ICSID Issues Decision In Favor Of Antofagasta, Barrick In Reko Diq Case.
Pakistan’s $500bn gold mine kept under wraps | The National