Barclays TZ...The hopeless,nimewanyooshea mikono!

kwani ulilazimishwa ulitoa rushwa ili kufungua account au ulitaka kutumai ile filosofi ya penye udhia penyeza lupia.

Hiyo tabia ya kupenyeza lupia ndiyo iliyochangia pia kukua kwa rushwa hapa nchini. Wakati wa 'vita ya uhujumu" wahindi (nataja kabila kama ambavyo ningesema wachaga- sina maana ya ubaguzi) walitumia sana hiyo lupia ili kujilinda wao na mali zao. Kuanzia hapo rushwa ikawa tatizo la kudumu nchini ambalo limekuwa likikua hadi kufikia kiwango cha tujisenti.

Usipenyeze lupia penye udhia, bali paache pajiozee. tafuta benki nyingine, zipo nyingi tu mjini.
 
sielewi hapo yaani benk ya kibiashara inapiga danadana watu kufungua acount! inasomeka kweli hiyo! Sasa waamekuja kufanya nini Bongo? Jamaa hapa ananiambia labda kupendezesha mji na hivo vibanda vyao vya blue
 
Mkuu benki ziko nyingi na zingine wala hazichukui muda kiasi hicho kufungua ama kufunga account. Au una agenda iliyofichika ambayo nao Barclays wameishtukia na wanaifanyia kazi? Watchout!
Bank zote zimeorodhesha masharti yake yote ya kujiunga kwenye karatasi kutegemeana na ni aina gani ya account unataka kufungua.
Zamani zamani wewe unajua una ishu sio Barkclays tuu, benki yoyote itakushtukia na siajabu hiyo cheque ikakudodea.
1. Unalipwaje kwa Cheque wakati huna account?.
2. Eti ni ya ki NGO, hii ndio account ngumu kufungua kuliko zote, lazima upeleke hati ya usajili maana NGO hazilipi kodi.
3. Hayo uliyajua, ndio mana ukataka kupenyeza rupia.
4. Inaonekana hiyo pesa imetoka nje kama imezidi!! Sh.10,000,000 benki yoyote haipokei cheki hiyo bila kupitia BOT kufanya authenticity ya ziliko toka hizo fedha.
5. Naamini aliyewalipa kabla haandika cheque, aliwaomba bank code ili afanye direct transifer, kwa vile huna account, na shida yako ni pesa, ukamconvince aandike cheque.
Tunaomba ukifanikiwa popote kufungua account na kudeposit hiyo hela na ikaclear tujulishe ili nasi tupitishie hiyo benki fedha zetu maana itakuwa ni laundry !.
 
Back
Top Bottom