Barcelona watavaa jezi zenye logo ya OVO ya msanii Drake kwenye El-Clasico

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Kuelekea mchezo mkubwa katika soka la vilabu Spain na Europe kwa ujumla imetangazwa rasmi kuwa FC Barcelona watavaa jezi zenye logo ya OVO ambayo ni kampuni ya muziki inayomilikiwa na mkali kutoka Toronto, Canada 'Drake' ikiwa ni katika kusheherekea mafanikio ya Drake kufikisha streams Bilioni 50 katika mtandao wa kusikilizia muziki wa Spotify ambao ni wadhamini wa FC Barcelona.

Hivyo basi logo ya Spotify haitakuwepo kwenye jezi katika mechi ya El-Clasico na badala yake itawekwa logo ya OVO.

Katika historia hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza Barcelona kuvaa jezi zenye logo ya msanii badala ya mdhamini wao.

Pia katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo (warm-up) wachezaji watavaa jezi maalumu ambazo nyuma zitakuwa na jina la 'DRAKE' ikiwa na namba 50 kusheherekea 50 billion streams za Drake kupitia Spotify.

Drake ndiyo anakuwa msanii wa kwanza katika mtandao wa kusikilizia muziki wa Spotify kufikisha streams Bilioni 50.

Fun facts:

'Drake Curse'
Drake ni msanii anayeaminika katika mitandao ya kijamii kuacha laana kwa timu au wanamichezo pale wanapokutana na kupiga picha naye. Kwani kila mwanamichezo anayekutana na Drake timu yake hupoteza mchezo unaofuata. Hivyo katika utani watu wanaamini Real Madrid wataifunga Barcelona kwasababu ya laana ya Drake.

April 15, 2019 admin wa AS Roma English alichapisha tweet ya utani kupitia mtandao wa Twitter akiwatania wachezaji wa timu yake ya Roma kuwa "All Roma players banned from taking photos with Drake until the end of the season"

Akiwa na maana kuwa wachezaji wote wa AS Roma wamezuiliwa kupiga picha na Drake mpaka mwisho wa msimu. Hii ni baada ya mastaa kama Pogba, Aguero, Aubameyang, Sancho, Kurzawa, Serena Williams na McGregor kupiga picha na Drake na timu zao kufanya vibaya katika michezo iliyofuata.
20221014_123325.jpg
 
Mechi itapigwa lini
Kuelekea mchezo mkubwa katika soka la vilabu Spain na Europe kwa ujumla imetangazwa rasmi kuwa FC Barcelona watavaa jezi zenye logo ya OVO ambayo ni kampuni ya muziki inayomilikiwa na mkali kutoka Toronto, Canada 'Drake' ikiwa ni katika kusheherekea mafanikio ya Drake kufikisha streams Bilioni 50 katika mtandao wa kusikilizia muziki wa Spotify ambao ni wadhamini wa FC Barcelona.

Hivyo basi logo ya Spotify haitakuwepo kwenye jezi katika mechi ya El-Clasico na badala yake itawekwa logo ya OVO.

Katika historia hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza Barcelona kuvaa jezi zenye logo ya msanii badala ya mdhamini wao.

Pia katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo (warm-up) wachezaji watavaa jezi maalumu ambazo nyuma zitakuwa na jina la 'DRAKE' ikiwa na namba 50 kusheherekea 50 billion streams za Drake kupitia Spotify.

Drake ndiyo anakuwa msanii wa kwanza katika mtandao wa kusikilizia muziki wa Spotify kufikisha streams Bilioni 50.

Fun facts:

'Drake Curse'
Drake ni msanii anayeaminika katika mitandao ya kijamii kuacha laana kwa timu au wanamichezo pale wanapokutana na kupiga picha naye. Kwani kila mwanamichezo anayekutana na Drake timu yake hupoteza mchezo unaofuata. Hivyo katika utani watu wanaamini Real Madrid wataifunga Barcelona kwasababu ya laana ya Drake.

April 15, 2019 admin wa AS Roma English alichapisha tweet ya utani kupitia mtandao wa Twitter akiwatania wachezaji wa timu yake ya Roma kuwa "All Roma players banned from taking photos with Drake until the end of the season"

Akiwa na maana kuwa wachezaji wote wa AS Roma wamezuiliwa kupiga picha na Drake mpaka mwisho wa msimu. Hii ni baada ya mastaa kama Pogba, Aguero, Aubameyang, Sancho, Kurzawa, Serena Williams na McGregor kupiga picha na Drake na timu zao kufanya vibaya katika michezo iliyofuata.View attachment 2386812
 
Back
Top Bottom