Kuna habari kuwa kwa takribani miaka miwili sasa baraza la mitihani kuna hakukaliki kwa wafanyakazi wake aidha kuondolewa ama kujiondoa wenyewe kufuatia ubabe uliopo pale wa katibu wake Mtendaji Dr Joyce Ndalichako. habari za ndani zinasema kuwa mama huyu amekuwa na mtazamo wake kivyake badala ya mtazamo wa kitaasisi. Kila kukicha ni kubadili watendaji bila kujali maslahi ya watahiniwa. Inasemekana kuwa aliweza kubadili kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa wa kidato cha sita 2007 na kusababisha wanafunzi wengi kufeli licha ya wataalamu wake kushauri. Wanajf wenye habari hizo vipi? Taasisi hiyo inaelekea pabaya