Baraza la Mitihani, NECTA, Siasa inauwa elimu

Baraza la Mitihani, NECTA, Siasa inauwa elimu

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,047
Reaction score
2,239
Nimempokea kijana wangu aliyekuwa anamalizia mitihani yake ya fomu siksi na swali langu la kwanza kama kawaida ya mzazi ikawa ni juu ya hali ya mitihani. Jibu la kijana ni kwamba mitihani ilikuwa ya kawaida. Baada ya mazungumzo ya muda kidogo, kijana amefunguka na kunihakikishia kwamba atashinda maana maswali mengi yalijulikana kabla ya muda.

Mimi ni baba, imebidi niulize aliipata wapi? Je, ni waalimu wanawasidia vijana wao? Jibu ni kwamba maswali yote walikuwa wakiyapokea kwa njia ya ”whatsapp” toka Dar es Salaam. Kwa hakika kabisa kijana kawataja wanafunzi wa shule ya Tusiime kwamba ndo yalikokuwa yakitokea. Somo la jiografia ametaja kwamba hilo waliletewa picha halisi kabisa ya mtihani ingawa mengine ilikuwa ni swali moja moja. Nakumbuka shule hii mwaka jana imepongezwa kwa ufaulu mzuri, sasa kumbe mambo yenyewe ndo yalivyo.

Lawama zangu ni siasa iliyoingizwa NECTA na miaka miwili tu tangu Ndalichako kuondoka, sasa mitihani inazidi kuwa ni njugu barabarani!
Ndalichako alikuwa na mipango ya kuondokana na tatizo hili sasa naona liko palepale na hisia yangu litakuzwa na ushindani wa shule za private zikishindana kuvuta wateja. Je, tutafika?
 
Wivu huo.Maswali kutoka kwa wanafunzi wa Tusiime kvp?Ina mwanao alikuwa akitumiwa maswali na wanafunzi wote wa Tusıime au hapo shuleni kwao wenzake nao pia wana marafiki Tusiime?Mtihani wa NECTA format yake ilivyo inawawezesha walimu na wanafunzi makini kuprobe maswali ya mtihani na hilo si kosa na ndıyo maana mwanao amekuambia mengne hayakuwa halisi.
 
Kwanza ww unajua necta au unasikia propaganda tu. Watu wanaoijua necta watafute wakwambie. Necta haifanyi kazi unayowaza ww, na shule umeishia kidato cha ngapi ww mzazi? Usichukue maneno ya mtaani ukaleta watu wachangie
 
Ukweli utabaki palepale NDALICHAKO alikuwa ni kisiki,kwa Tz ya sasa hivi ya watu wa kupiga dili wanapo pata fursa mtu wa aina ya Ndalichako ni nadra kumpata :A S 100:
 
Walimuondoa Ndalichako kwa sababu Mtoto wa Mkuuu alifeli
Waislamu walilalamika anawapunja marks.
Yule mama tokea ameondoka hawa wahitimu wamekuwa viazi sana.
Elimu na siasa havitakiwi ingiliana. Wangeacha hata kama wanafunzi wote wakifeli imradi hawajafanya kile kinachotakiwa basi waendelee feli tu sema ikitokea hivyo wazazi wanalia lia, wanasiasa wanalia lia
 
MchunguZI

pole sana kwa kuwa hujui ulisemalo wala ulitendalo. Umedanganywa na kijana wako kwa kuwa kuvuja paper la NECTA Siku hizi ni ndoto za mchana. Pengine umetumwa, hata Kama umetumwa, umetumia hoja dhaifu. Pole!!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini watu hawaji na inquiry minds? kwa nin watu wanakuja na kukanusha tu wakati wao wanaishi majumban kwao na huyu anaishi nyumban kwake? hapo ndipo unagundua wengi hapo zamani walifaulu kwa ukanjanja tu na ndo maana hoja kama hii wameijia kwa hasira sana na hawa nai wanafunz waliofaulu kuanzia mwaka jana kuendelea na weng waliojib hoja hizi ndo waliofanikiwa na mitihani hii iliyo leak waswas wao ni kuwa kelele zikizid itafutwa otherwise watu wenye akili wangetaka mtoa hoja athibitishe na si kupinga. division 5 at work........ hii nchi inaharibika kwa kuzalisha mijitu isiyo na akili na hii ndo mikanjanja kwenye kila fani.
 
kwan mwanao ndo kamalza 4m6 peke yake? utakuwa unataka kuichafua shule ya tusiime hakuna mtihan uliovuja ka unaona ni siasa waambie baraz wafute matokeo ya mwanao hapo utakua mzalendo
 
Madiliko katika masuala yote yanayohusiana na mitihani tokea aondoke mama Ndalichako yamekuwa dhahiri,na yanaongezeka kila siku.Nadhani kuna tatizo la kukosa umakini na hasa katika wizara ya Elimu.

Nipo Mbeya kwa sasa na nimeshuhudia vituko vya ajabu vilivyofanywa na wizara ya Elimu.Baada ya kuanza BRN,wizara ilianza kutunga mitihani ya terminal kwa kidato cha nne inayofanywa nchi nzima na wanafunzi wa kidato cha nne.Mwaka huu ilianza jumatatu 18/05/2015 mpaka ijumaa 22/05/2015 ikihusisha mitihani minne,Mathematics,Kiswahili,English na Biology.Mitihani yote ilikuwa na makosa ya ajabu,mfano:Basic Mathematics,theluthi moja ya maswali yote yalikosewa,michoro yote miwili iliyotakiwa kuwepo haikuchorwa,instruction hazikukamilika,mfano unaambiwa tumia pie = bila kuandikwa thamani yake.Hakukuwa na mtiririko mzuri wa uandishi wa namba za maswali,mfano swali la 2 lilitokea mala 17.Kwa ujumla zaidi ya nusu ya maswali yalikuwa hayafanyike.Wazazi wamelalamika mno,inakera sana mtoto wako anakesha akisoma halafu anakutana na mitihani iliyokosewa namna hiyo.Tafsiri ya wanafunzi ya BRN ni mzaha,kukosa umakini na vituko.Tuombe Mungu mzaha huu usije ukaingia kwenye mitihani ya NECTA,ikitokea hivyo taswira ya Tanzania kimataifa itaharibika vibaya mno.

Naomba wahusika waache kabisa kuleta mzaha kwenye Elimu,naamini angekuwepo Ndalichako asingeruhusu ujinga huu ufanyike.Naomba wadau watafute mitihani hiyo waone vituko vya karne.Watanzania tuache kabisa kuleta siasa kwenye Elimu.Wote tuunganike tuwaeleze wahusika kwa sauti isiyo na mzaha hata kidogo kuwa,"Uzembe wenu ni mauti yetu"
 
Wewe mzazi umechemka na mwanao muongo kwanza ww Huna mtoto umetumwa tu.

Pia huyu mzazi simwelewi!! Anadhani Ndalichako kuondoka NECTA ndo mitihani imeanza kuvuja... Rudi kaka Mzazi ukafanye utafiti wa uvujaji wa mitihani!! Tofauti na hapo utakuwa na wivu na shule Tusiime na pia uongozi uliopo wa NECTA
 
Wewe mzazi umechemka na mwanao muongo kwanza ww Huna mtoto umetumwa tu.

Aombe mwanae afutiwe matokeo kama hana fitina!

pole sana kwa kuwa hujui ulisemalo wala ulitendalo. Umedanganywa na kijana wako kwa kuwa kuvuja paper la NECTA Siku hizi ni ndoto za mchana. Pengine umetumwa, hata Kama umetumwa, umetumia hoja dhaifu. Pole!!!

kwan mwanao ndo kamalza 4m6 peke yake? utakuwa unataka kuichafua shule ya tusiime hakuna mtihan uliovuja ka unaona ni siasa waambie baraz wafute matokeo ya mwanao hapo utakua mzalendo

Mzazi kama mwanafunzi!

Imenibidi niwakusanye ili niwaandikie kwa pamoja baada ya kusoma mawazo yenu wote ni ya wale wanaosubiri kufufuka.
Nilichoandika ni kile kilichotokea kwa mwanangu, Mulitaka niandike ambayo sikuyaona?

Nimewahi kuandika hapa kwamba siku hizi hata chizi, mwizi, nk. anapata ushabiki JF. Wengine wakisikia jina linalofanana na kabila lake tu, Wanatetea hata kama linamhusu mtu mwizi, hata kama hawana faida na wizi huo. Wengin e wakisikia linamuhusu mtu mwenye dini moja nayeye pia wanatetea ili tu kuwakomoa wa dini nyingine. Wapo wale wa chama kimoja nao wanateteana bila manufaa au mafanikio yoyote.

Ninyi wote mulioandika sioni wa kujadiliana naye maana Binafsi NECTA naijua kuliko ninyi. Wengi wenu uelewa mdogo haulingani na elimu yenu na hayo ni matokeo hayo hayo ya wizi wa mitihani. Munapata vyeti bila elimu. Katika familia yangu hakuna hilo na sifurahii wizi wa mitihani.

Shule hizi zoote zinazotangazwa kila mwaka kwa ubora tena kwa kupishana wako ktk juhudi za wizi wa mitihani kila mwaka. Ni biashara. Kwa uzembe wenu mukiona matokeo mazuri munadhani wataoto wenu au ndugu zenu wanafaa, lakini mumezungumza nao kuona kama ufahamu upo? huenda hamtagundua maana inategemea ufahamu wenu pia.

Subiri utajionea matokeo.
 
Pia huyu mzazi simwelewi!! Anadhani Ndalichako kuondoka NECTA ndo mitihani imeanza kuvuja... Rudi kaka Mzazi ukafanye utafiti wa uvujaji wa mitihani!! Tofauti na hapo utakuwa na wivu na shule Tusiime na pia uongozi uliopo wa NECTA

Kama ni mnayama wewe ni ngiri maana hata hukufikiri unajibu nini. Kwanza nani kasema mimi ni kaka? Au ni hizo hisia na mbu kila wakati unawaza kunyonya tu!

Unanituma nikafanye utafiti gani? au hujui maana ya utafiti? yaani kuona mtihani ulivyovuja miaka hii nahitaji utafiti! Mawazo kama haya niliyasikia Bunge la katiba, nikadhani ni wachache kumbe muko wnegi! Fooool!
 
Kama ni mnayama wewe ni ngiri maana hata hukufikiri unajibu nini. Kwanza nani kasema mimi ni kaka? Au ni hizo hisia na mbu kila wakati unawaza kunyonya tu!

Unanituma nikafanye utafiti gani? au hujui maana ya utafiti? yaani kuona mtihani ulivyovuja miaka hii nahitaji utafiti! Mawazo kama haya niliyasikia Bunge la katiba, nikadhani ni wachache kumbe muko wnegi! Fooool!

Kwahaya maneno yako Dada unathibitisha ni sifuri kuliko hata mwanao aliyekuwa anategemea maswali toka Tusiime!! Huna hoja unaanza matusi tu!! ----- kweli kweli Mzazi!!
 
wewe utakuwa una ukabila kwa sababu tusiime ni ya wahaya. kesho utaisema kaizilege ilimradi tu umechafua.
 
Back
Top Bottom