Baraza la Mitihani (NECTA) latangaza Matokeo ya Kidato cha sita 2017

Naombeni matokeo ya Tabora Girls

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Hivi baada ya kuongoza huwa wanapotelea wapi?
Umewafuatilia? Unasema tu! If you are not an academician , you can never now the whereabouts of these good students. Mosha yuko University of Cape Town! She is performing wonders there
\

Imaculate Mosha
Research Assistant at University of Cape Town

Cape Town Area, South Africa
Computer Software
Current
  1. University of Cape Town,
  2. DataProphet,
  3. Women in Computer Science , UCT
Previous
  1. University of Cape Town,
  2. j5 International Limited,
  3. UCT Women in Computer Science
Education
  1. University of Cape Town
 

Attachments

  • upload_2017-7-15_13-55-27.jpeg
    upload_2017-7-15_13-55-27.jpeg
    7.9 KB · Views: 57
S.0132/0673
Div 2 ya point 11,D tatu,C moja na S moja
S.0132/0834
Div 1 ya point 8, C Mbili,B Moja na E Moja
Hawa ndugu zako nimewapenda hasa huyo wa div 1 kapiga B ya Adv/Maths
msaada plz hii S.0947/0571
 
Shule zilizoongoza


Katika matokeo hayo, Shule ya Wasichana ya Feza Girls ya Dar es Salaam imeibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys (Pwani) iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.


Shule nyingine ni Marian Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza Boys (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.


Shule zilizoshika mkia

Shule zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja). Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya) na Mlima Mbeya (Mbeya).
Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent(Tabora).


Waliofutiwa matokeo
Kadhalika taarifa ya Necta imeeleza kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.
Taarifa ya Dk Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.
Pamoja na hao kumi, watahiniwa wengine 15 hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya mitihani hiyo.


‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.
 
Back
Top Bottom