Baraza la Mitihani (NECTA) latangaza Matokeo ya Kidato cha sita 2017

MrMondo

Member
Feb 23, 2015
94
58
Hivi punde waziri wa elimu sayansi na teknolojia anarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi wa tano mapema mwaka huu.

Chanzo cha habari hii ni www.necta.go.tz

UPDATE:

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.

Kupata matokeo, http://41.188.136.77/matokeo/

tembelea http://41.188.136.77/matokeo
=======

Kwa ufupi
  • Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
  • Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
  • Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Zanzibar
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.

Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.

Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;

“Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”

Ufaulu wa masomo
Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.

Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.

CHANZO: Mwananchi
 
Kwa mujibu wa habari ambazo zipo hapa ITV ni kuwa wameitwa kwa ajili ya upokeaji na utangazaji wa matokeo hapa Zanzibar. Safari hii katibu mtendaji wao ndugu Msonde kaamua kuyatangazia hapa Zanzibar, stay tuned

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
b1571424044eddcdb681496b113a1e06.jpg


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom