BARAZA la Maaskofu limeomba radhi kwa kitendo cha kukojolewa Kitabu Kitukufu cha Korani.

wewe unadhania kuomba msamaha ndiko kutafuta chuki ya muislamu kwa mkristo? Ndio maana wamarekani hawakuomba radhi kwa wamisri kwa ile filamu ya kukashifu dini yao. nakusifu kwa kufanya jambo la maana ila umelifanya kwa watu walio kula kiapo cha chuki kwako maisha yao yote.
 
wanaomba radhi ya nini? mbona hakuna masheikh au viongozi kutoka bakwata ambao waliwaomba radhi wakristo wakati makanisa yalivyochomwa moto zanzibar...hakuna cha kuomba radhi wala nini..wote tunajua tatizo sio wakristo tatizo ni waislalm so serikali ikae nao hao waleta vurugu iwaulize ni nini wanataka..kwa sababu za ya wivu wa kimaendeleo na kielimu dhidi ya wakristo sioni sababu nyingine yoyote

Wana wivu wa kike hao eti serikali inatubeba ni juhudi zetu ona mavyuo yalivyojaa endeleeni kulalamika tu necta,necta huku hamna mikakati yoyote ya kuanzisha shule zaidi ya kuchoma makanisa. TUMSIFU YESU KRISTU.
 
BARAZA la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) limeomba radhi kwa kitendo cha kukojolewa Kitabu Kitukufu cha Korani.
Pia limeiomba Serikali kushirikisha mabaraza yote ya kidini kuunda tume huru itakayosimamia na kuishauri juu ya uendeshaji taasisi na jumuiya za kidini nchini.
Halikadhalika limeitaka Serikali kubana wahusika wa uvunjwaji wa makanisa na kurejesha mali zilizoibwa na kulipa fidia za uharibifu wa kuchoma makanisa 10 yaliyoko Tanzania Bara.

Tamko hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Askofu Dk Mwigulu Kilimba likitokana na mkutano wa siku mbili wa maaskofu na wachungaji zaidi ya 1,000 waliokutana kujadili vurugu na ghasia za kuchomwa moto makanisa, Biblia kuchanwa na kupigwa kwa watumishi wa Mungu hivi karibuni.

Alisema vurugu hizo zilitokana na kitendo cha mtoto kukojolea Korani Mbagala jijini Dar es Salaam, kitendo kilichowahuzunisha na kuwafadhaisha.

“Baraza linaomba radhi kutokana na kitendo hicho, kwani kama mmoja asingemshawishi mwenziwe, yaliyotokea yasingetokea,” alisema Dk Kilimba na kuongeza kuwa kitendo cha kukojolea Korani hakijawafurahisha.

Alisema baada ya kitendo hicho, vurugu zilizosababisha uvunjifu wa amani zilitokea na Baraza linaiomba Serikali irejee misingi ya Katiba kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia isiyo na dini, ili kusaidia kuondoa hisia za kundi moja la dini kuona watawala wako upande wa dini fulani.

Kwa mujibu wa Dk Kilimba, Baraza limeiomba Serikali kushirikisha mabaraza yote ya kidini nchini na kuunda Tume Huru itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuishauri Serikali juu ya uendeshwaji wa shughuli za taasisi na jumuiya za kidini.

“Jambo hili litasaidia kubainisha mipaka ya kiutendaji kwa shughuli za kidini na mamlaka ya nchi, hivyo kuondoa dhana ya kutaka kuingiza udini kwenye siasa,” alisema Dk Kilimba na kuwaomba waumini kuendelea kudumisha hali ya utulivu na amani.

Aliiomba Serikali itambue kuwa macho na wapenda amani nchini wanasubiri kuona hatua zitakazochukuliwa kwa watuhumiwa wa matukio ya uvunjwaji wa makanisa Zanzibar na Tanzania Bara.

Siku za karibuni nchi imekuwa katika vurugu za kidini ambapo wafuasi wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakifanya maandamano na kushambulia makanisa huku wakiyachoma moto na kupora mali zilizomo na pia baadhi ya magari yakipondwa mawe na kuharibiwa.

Sehemu ya vurugu hizo ilichangiwa na mtoto mwenye umri wa miaka 14 kukojolea Kitabu cha Korani kutokana na ubishani na mtoto mwenziwe aliyemtishia kuwa akifanya kitendo hicho atageuka panya au nyoka.

Siwaelewi, mnaomba radhi kwa vile mmefanya /mmemtuma afanye hivyo. Nashukuru hakuna maaskofu wakatoliki! Unaomba radhi ya nini! After all, askofu haoi!!!!
 
hawa maaskofu ndio wanaowatuma waumini wao wakojolee kitabu kitakatifu cha quran, hizi ni akili mbovu huwezi kueneza dini kwa kudhalilisha kitabu cha dini nyingine foolishness.

Duh.. Yaani wewe ndo hopeless kabisa.. Suala la kukojolewa Quran lilianzia kwenye ubishi uliozuka baina ya watoto wawili.. Hilo suala la kutumwa na Maaskofu limetokea wapi..? Hivi huna ndugu wa dini tofauti na wewe..? Au jirani wa dini tofauti na wewe..? Au rafiki wa dini tofauti na wewe..? Au boci au mfanyakazi wako ambae ni tofauti na wewe..? Stop bein selfish..!
 
Je Serikali kushirikisha mabaraza yote ya kidini kuunda tume huru itakayosimamia na kuishauri juu ya uendeshaji taasisi na jumuiya za kidini nchini?
 
...“Baraza linaomba radhi kutokana na kitendo hicho, kwani kama mmoja asingemshawishi mwenziwe, yaliyotokea yasingetokea,” alisema Dk Kilimba na kuongeza kuwa kitendo cha kukojolea Korani hakijawafurahisha'...


Hapa mimi sijaelewa, ina maana radhi ipi inaombwa-kwani huyu mtoto alitumwa na kanisa akakojolee Quran Au kanisa lilifanya uzembe gani hadi kusababisha hili tukio?
 
Siwaelewi, mnaomba radhi kwa vile mmefanya /mmemtuma afanye hivyo. Nashukuru hakuna maaskofu wakatoliki! Unaomba radhi ya nini! After all, askofu haoi!!!!
Askofu haoi?
Chunguza maandiko, acha kulishwa kama kifaranga tafiti kwa akili zako uone ukweli ulivyo.
Angalia-'The papal encyclicals 1958-1981, page204
Pope Paul VI, in his encyclical 'Sacerdotalis Caelibatus(Priestly Celibacy, 1967), endorsed celibacy as a requirement for the clergy, but he admitted that ''The New Testament which preserves the teaching of christ and the Apostles... does not openly demand celibacy of sacred ministers...Jesus Himself did not make it a prerequisite in His choice of the Twelve, nor did the Apostles for those who presided over the first Christian communities.''--The Papal Encyclicals 1958-1981.
Refer 1 Corinthias 9:5,John 1:42, Mark 1:29-31 (mother in law of Peter)
1 Timothy 3:2 (a bishop to be married once/ to be a husband of one wife.
1 Timothy 4:1-3 (doctrine from the devils;...they will say marriage is forbidden.
 
Hongera sana Baraza la Maaskofu kwa kuomba Radhi , inadhirisha kudumisha upendo na amani kwa gharama yoyote hata ikibidi kuomba radhi pale ambapo hata hatuna makosa . hizo ndizo gharama za Upendo na amani .
Ninadhani uislam una muongozo, je , Ni aya gani ndani ya Quran inayowaelekeza waislam kuchoma Na kuharibu makanisa pale mtu Mwenye jina la Kikrito anapowakosea?
Inabidi kuelewa vizuri misingi ya Imani zetu maana mtu mwenye kumwamini Mungu Ni mwenye Subira ,mvumilivu, asieonyesha Uwezo (kwani uwezo Ni wa Mungu pekee) Mwenye kuonyesha daima Upendo Kwa watu wote Kwa kua wameubwa Na Mungu.....
 
Askofu haoi?
Chunguza maandiko, acha kulishwa kama kifaranga tafiti kwa akili zako uone ukweli ulivyo.
Angalia-'The papal encyclicals 1958-1981, page204
Pope Paul VI, in his encyclical 'Sacerdotalis Caelibatus(Priestly Celibacy, 1967), endorsed celibacy as a requirement for the clergy, but he admitted that ''The New Testament which preserves the teaching of christ and the Apostles... does not openly demand celibacy of sacred ministers...Jesus Himself did not make it a prerequisite in His choice of the Twelve, nor did the Apostles for those who presided over the first Christian communities.''--The Papal Encyclicals 1958-1981.
Refer 1 Corinthias 9:5,John 1:42, Mark 1:29-31 (mother in law of Peter)
1 Timothy 3:2 (a bishop to be married once/ to be a husband of one wife.
1 Timothy 4:1-3 (doctrine from the devils;...they will say marriage is forbidden.

Tuko wote, maaskofu wa Kikatoliki hawaoi! Basi zaidi ya hapo ni yako na timoty. We do not know what the old writings meant by a Bishop. Tunaona katika biblia watu wanaishi miaka elfu moja na zaidi......., kuna mtu anaishi miaka elfu moja karne hizi. hatujui miaka walikuwa wanaanisha nini! Hivyo hivyo hatujui maaskofu wanaooa walikuwa wanamaanisha nini> This is quite debatable!
 
serikali ya kikwete na ccm haiwezi kufanya lolote la maana kwa sababu iko kwa maslahi y a kifamilia zaidi.

Hao waislam wanachukua hatua gani kwa mtoto aliyemshawishi mwenzake akojolee hicho kitabu? Je angebadilika nyau yule mtoto waislam bado wangechoma makanisa au huo unyau ungetosha kufuta kosa la mikojo? Hasira za watoto kudanganyana zinaendaje makanisani kama si njama na hila za kutafuta mlango wa kufanya chuki walizonazo juu ya ukristo? Kwani wamethibitishaje kuwa yule mtoto alitumwa na kanisa kukojolea? Wanathibitishaje kwamba yule mtoto mshawishi hakutumwa na wao ili wapate mlango wa kuanzishia fujo?



dah,kama nakuona vile hapo ulipo...!!
Well..,kila kitu kiko wazi,na kila kilichofanyika kimeacha mesegi,
kujiufunza sasa kutokana na makosa
tusianze nyoosheana vidole hapa
kila mtu anakithamini na kukipenda kile kinachompa amani
hilo lieleweke wazi kabisa
 
Mkuu angalia tarehe ya thread. Siku magazeti yaliporipoti maaskofu kuombba radhi, kesho yake askofu Kilimba alikanusha vikali kuwa wameomba radhi. Alisema wazi kuwa hawawezi kuwaomba radhi wakorofi waliowachomea makanisa na wezi wa mali za kanisa. Maaskofu walichosema ni kuwa wamesikitishwa na michezo ya kitoto iliyopelekea kukojolewa kwa korani. Tena alishauri serikali ijitahidi kubuni ajira ili kuwasaidia baadhi ya watu ambao wameanza kubuni visa ili wafanye uporaji. Alishutumu magazeti kwa kuandika habari za uongo.

kwa ufafanuzi huu mpya nimeridhika kwasababu kanisa litaombaje radhi kwa matendo ya wahuni? aliyekojolea kuran ni muhuni mkristo na waliochoma makanisa na kupora ni wahuni wa kislamu!
 
we huwajui waislam, wao hawana tatizo hata kidogo. Yaani ni watu wa kawaida kabisa, ishu ni kitabu chao! Yaani kwa mujibu wa koran mtu yeyote asiye muislam hana dini (kafiri/mpagani) na hastahili kuishi. Na mwanzoni huko uarabuni, dini ilienezwa kwa upanga/jambia. Wasio waislam walikuwa wanauawa. Sasa hivi hilo haliwezekani lakini dhambi hiyo bado inaandama vizazi vyao, wanatamani kumwaga damu. Namna ya kuokoa vizazi vijavyo ni kui-edit koran tu, kwa sababu vichwa ngumu wanameza mistari kama ilivyo.



tui-edit kama mlivofanya nyie sio??
Unayoyasema kwanza si kweli,ni mshabiki na mzandiki pia upeo wa fikra ni kama ule wa philipo mulugo
amin imani yako na wengine waamin imani yao
kama moto upo na pepo ipo basi usiwe na shaka sisi waislam tutaenda motoni nyie mtaenda peponi na kupata uzima wa milele,,muhimu ni kua na subira tuh katika haya maisha ya mpito
 
mnajua nyinyi mnatakiwa muwe na akili ya ziada japo kidogo. hivi vitendo vya kuidhalilisha qur'an vimeanza leo? matukio mangapi yalilipotiwa ya kudhalilishwa qur'an na serikali ambayo inasema haina dini ikayafumbia macho ikiwemo na viongozi wenu wa kikristo? sasa imefika pahala waislam wamechoshwa na huu upumbavu mnaoufanya badala yake na wao wameamuwa kuharibu miongoni mwa vitu vyenu vya kiimani ili nanyi mjisikie ni kwa kiasi gani hili jambo linavyoumiza. Mtenda akitendewa huisi ameonewa ila akitenda yeye yupo sawasawa! sasa leo imejidhihirisha wazi kabisa kuwa serikali ya Tanzania ina dini nayo ni ukristo!!



WORD UP...!!
:A S thumbs_down:
 
kwa ufafanuzi huu mpya nimeridhika kwasababu kanisa litaombaje radhi kwa matendo ya wahuni? Aliyekojolea kuran ni muhuni mkristo na waliochoma makanisa na kupora ni wahuni wa kislamu!


emeona eeh
wanapandikza chuki tuh na kujifanya wao ndio wana busara na wepesi kuomba radhi
hawana lolote
 
Jeuri na viburi vya maaskofu katika nchi hii haviwezi kuwafanya waombe radhi. Kama wangekuwa ni waungwana basi angalau wangekemea matukio ya mara kwa mara yanayofanywa na wafuasi wao ya kuukashifu uislamu na matukufu yake. Hawawezi kukemea kwa kuwa hayo ndio matunda ya mafunzo kwa watoto wao. wanapenda kusikia matukufu ya waislamu yakikashifiwa. Badala yake wanawafundisha watoto wao kwamba qurani ni kitabu cha majini na mashetani. Imani ni kitu kingine rafiki.Wakati wewe unaona uislamu na vitabu vyake na misingi yake ni utukufu basi hata mchungaji au mkristu anaona bibilia yake na vifaa vyake ,makanisa au nyumba za ibada ni vitu vitukufu kabisa.Kama kukemea waislamu mngeanza kukemea wale wote wanaodhalilisha ukristu ili haki itendeke.Imani ya kiislamu na kikristu ziko tofauti sana na kila moja ikiona vifaa vyake,vitabu vyake,mitume wake na nyumba zao za ibada ni tukufu! Sote tuheshimiane na kuogopa kudhalilisha dini nyingine kwa mtazamo wowote ule.
 
Huyo mchungaji aliyekanusha kuomba radhi ndio amenifurahisha.Niliishaanza kupost hapa kuwaona hao maaskofu ni wapuuzi.Unaombaje msamaha kwa mambo ya watoto?Mtoto anapokosea huwa anaadhibiwa kumuonyesha kwamba alichokifanya sio kizuri na asirudie siku nyingine.Sasa majitu mazima yana misbehave kwa mambo waliyofanya watoto,huku ni kukosa kazi na busara.
Dini zenyewe hizi za kuletewa ,watu wengine ndio wanajifanya wao ni wasafi kuliko hata hao mitume.Kiukweli ningekuwa na madaraka ningewatandika sana hawa watu mpaka washike adabu.Huyo mtoto aliyekojolea wameishamuathiri kisaikolojia , kwa liliotokea.Kiuhalisia watoto huwa ni wadadisi,na kilichotokea kwao walikua wanadadisi hayo mnayowafundisha.Na kama mnawafundisha uongo matokeo yake ndio hayo yanayowafanya watu wafiche aibu ya uongo wao kwa kwenda kuwaharibia wengine mali.
hili suala naliita ni la kijinga na wala sio la kitoto.Kwani watoto huwa wana reason.
 
Back
Top Bottom