BARAZA la Maaskofu limeomba radhi kwa kitendo cha kukojolewa Kitabu Kitukufu cha Korani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BARAZA la Maaskofu limeomba radhi kwa kitendo cha kukojolewa Kitabu Kitukufu cha Korani.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by R.B, Oct 27, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  BARAZA la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) limeomba radhi kwa kitendo cha kukojolewa Kitabu Kitukufu cha Korani.
  Pia limeiomba Serikali kushirikisha mabaraza yote ya kidini kuunda tume huru itakayosimamia na kuishauri juu ya uendeshaji taasisi na jumuiya za kidini nchini.
  Halikadhalika limeitaka Serikali kubana wahusika wa uvunjwaji wa makanisa na kurejesha mali zilizoibwa na kulipa fidia za uharibifu wa kuchoma makanisa 10 yaliyoko Tanzania Bara.

  Tamko hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Askofu Dk Mwigulu Kilimba likitokana na mkutano wa siku mbili wa maaskofu na wachungaji zaidi ya 1,000 waliokutana kujadili vurugu na ghasia za kuchomwa moto makanisa, Biblia kuchanwa na kupigwa kwa watumishi wa Mungu hivi karibuni.

  Alisema vurugu hizo zilitokana na kitendo cha mtoto kukojolea Korani Mbagala jijini Dar es Salaam, kitendo kilichowahuzunisha na kuwafadhaisha.

  “Baraza linaomba radhi kutokana na kitendo hicho, kwani kama mmoja asingemshawishi mwenziwe, yaliyotokea yasingetokea,” alisema Dk Kilimba na kuongeza kuwa kitendo cha kukojolea Korani hakijawafurahisha.

  Alisema baada ya kitendo hicho, vurugu zilizosababisha uvunjifu wa amani zilitokea na Baraza linaiomba Serikali irejee misingi ya Katiba kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia isiyo na dini, ili kusaidia kuondoa hisia za kundi moja la dini kuona watawala wako upande wa dini fulani.

  Kwa mujibu wa Dk Kilimba, Baraza limeiomba Serikali kushirikisha mabaraza yote ya kidini nchini na kuunda Tume Huru itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuishauri Serikali juu ya uendeshwaji wa shughuli za taasisi na jumuiya za kidini.

  “Jambo hili litasaidia kubainisha mipaka ya kiutendaji kwa shughuli za kidini na mamlaka ya nchi, hivyo kuondoa dhana ya kutaka kuingiza udini kwenye siasa,” alisema Dk Kilimba na kuwaomba waumini kuendelea kudumisha hali ya utulivu na amani.

  Aliiomba Serikali itambue kuwa macho na wapenda amani nchini wanasubiri kuona hatua zitakazochukuliwa kwa watuhumiwa wa matukio ya uvunjwaji wa makanisa Zanzibar na Tanzania Bara.

  Siku za karibuni nchi imekuwa katika vurugu za kidini ambapo wafuasi wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakifanya maandamano na kushambulia makanisa huku wakiyachoma moto na kupora mali zilizomo na pia baadhi ya magari yakipondwa mawe na kuharibiwa.

  Sehemu ya vurugu hizo ilichangiwa na mtoto mwenye umri wa miaka 14 kukojolea Kitabu cha Korani kutokana na ubishani na mtoto mwenziwe aliyemtishia kuwa akifanya kitendo hicho atageuka panya au nyoka.
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  hilo la kuwa baraza la pamoja la ku-monitor taasisi na jumuia za kidini naliunga mkono kwa 100%. hii inatokana na serikali kushindwa kudhibiti jumuia/tasisi/vikundi vya kidini ambavyo baadhi vimegeuka tatizo kwa amani na utulivu nchi. vipo kwa dini zote mbili kubwa nchini ndio maana maaskofu wanashauri baraza lijumuishe wawakilishi wa dini zote.
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,082
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red; ndipo hasa kisa na mkasa vilipo juu ya kadhia ya Mbagala. Chanzo cha vurugu nini na nani? Hongereni maaskofu.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,082
  Trophy Points: 280
  Tunakoelekea baadhi ya taasisi za kidini ni hatari kwa usalama wa taifa kuliko ukimwi, ujambazi, ufisadi, au vita baina yetu na adui wa nje.
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Aliyeshawishi Quran kukojolewa na aliyeshawishika akakojolea Quran WOTE ni wakosaji. It takes two to Tango.

  Lakini wale "WAHUNI" waliokwenda kuchoma na kuiba makanisani ni WAKOSAJI zaidi kuliko hao watoto.
   
 6. T

  Tabby JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,894
  Likes Received: 5,521
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Kikwete na ccm haiwezi kufanya lolote la maana kwa sababu iko kwa maslahi y a kifamilia zaidi.

  Hao waislam wanachukua hatua gani kwa mtoto aliyemshawishi mwenzake akojolee hicho kitabu? JE ANGEBADILIKA NYAU YULE MTOTO WAISLAM BADO WANGECHOMA MAKANISA AU HUO UNYAU UNGETOSHA KUFUTA KOSA LA MIKOJO? HASIRA ZA WATOTO KUDANGANYANA ZINAENDAJE MAKANISANI KAMA SI NJAMA NA HILA ZA KUTAFUTA MLANGO WA KUFANYA CHUKI WALIZONAZO JUU YA UKRISTO? KWANI WAMETHIBITISHAJE KUWA YULE MTOTO ALITUMWA NA KANISA KUKOJOLEA? WANATHIBITISHAJE KWAMBA YULE MTOTO MSHAWISHI HAKUTUMWA NA WAO ILI WAPATE MLANGO WA KUANZISHIA FUJO?
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Akizungumza na WAPO radio leo asubuhi askofu Mwakilimba amekanusha vikali madai yaliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa baraza la maaskofu limeomba radhi. Alisema kuwa wao walionyesha kusikitishwa tu na michezo ya kitoto iliyopelekea kukojolewa kwa kuran na watoto hao. Alisisitiza kuwa kamwe hawatawaomba radhi watu waliochoma makanisa. Amedai kuwa vyombo vya habari vimeandika upotoshaji na kuwa tamko halisi linapatikana mtandaoni.
  Mtazamo wangu: ndugu zetu waislamu wanatakiwa kujitokeza hadharani na kujitenga na waislamu wenye msimamo usiofaa ili kurejesha mahusiano mema.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wanaomba radhi ya nini? mbona hakuna masheikh au viongozi kutoka bakwata ambao waliwaomba radhi wakristo wakati makanisa yalivyochomwa moto zanzibar...hakuna cha kuomba radhi wala nini..wote tunajua tatizo sio wakristo tatizo ni waislalm so serikali ikae nao hao waleta vurugu iwaulize ni nini wanataka..kwa sababu za ya wivu wa kimaendeleo na kielimu dhidi ya wakristo sioni sababu nyingine yoyote
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  safi sana yaani huyo padri alikua kama vile kwenye akili yangu
   
 10. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Safi sana viongozi wetu! mna busara na hekima sana.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kukosa ustaarabu kwa wengine kusikulazimishe na wewe kukosa ustaarabu. Usikubali kuwa reduced to somebody else's level. Ni uungwana kuomba radhi kwa niaba ya unaowaongoza, inaitwa uwajibikaji!
   
 12. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kuomba radhi ni kitendo cha kiungwana
   
 13. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa maaskofu ndio wanaowatuma waumini wao wakojolee kitabu kitakatifu cha quran, hizi ni akili mbovu huwezi kueneza dini kwa kudhalilisha kitabu cha dini nyingine foolishness.
   
 14. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,160
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  ahahahahaaa, daah! togola gamale!Nashauri waombe radhi tena kwa niaba ya yule kijana wa kipemba aliye kojolea, kunyea, na kumvalisha mbwa tasbihi yenye ndevu!
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Na yule aliyeripotiwa jana kukojolea q'uran na kumvalisha mbwa tasbihi huko zanzibar anachukuliwa hatua gani? Au kwa sababu ni muislamu hakuna tatizo?!
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sio kukosa ustaarabu...mtoto mdogo alikojolea quran, kwanza hakuna cost yoyote hapo waislam imewaingia plus aliyekojolea ni mtoto mdogo na sio mtu mzima..vitu vingapi watoto wetu wanafanya na tunajua wamefanya kwa sababu ya utoto wao na tunawasamehe? makanisa yamechomwa na watu wazima na sio watoto ambao hawana akili...ni watu wazima ambao walipanga kwenda kuchoma na kuharibu mali za kanisa ambazo ni gharama ya mamillion...ukiangalia hata in terms of cost pekee ilibidi wakristo waombwe msamaha...mtu mzima angekojolea hiyo quran kidogo ningeelewa bt watoto ni watoto you cant treat them like adults bt its amazing some muslim adults behave like kids at times...
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kabla ya kuunda hilo baraza, kwanza rais amuondoe Wassira na afute hiyo wizara. Hatuwezi kuwa na office mbili kwa kazi ile ile. Tumeshaona Wassira hawezi kusimamia mahusiano ya jamii na wala hana ubunifu wowote kwenye hiyo wizara. Tuanze upya.
   
 18. m

  mfumo JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Jeuri na viburi vya maaskofu katika nchi hii haviwezi kuwafanya waombe radhi. Kama wangekuwa ni waungwana basi angalau wangekemea matukio ya mara kwa mara yanayofanywa na wafuasi wao ya kuukashifu uislamu na matukufu yake. Hawawezi kukemea kwa kuwa hayo ndio matunda ya mafunzo kwa watoto wao. wanapenda kusikia matukufu ya waislamu yakikashifiwa. Badala yake wanawafundisha watoto wao kwamba qurani ni kitabu cha majini na mashetani.

   
 19. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Maaskofu 1000 waliokaa kwa siku mbili itakuwa wamejua nani mkosa.Sasa hawa Kova na Mussa wanasema nini?.Na wao nao lazima waombe radhi baada ya kuwaacha huru masheikh zetu.Wao wabaki na ujinga na ukafiri wao.
   
 20. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Baraza la maaskofu PCT; siyo la Baraza la Makanisa yote ya Pentekoste nchini.Tena nina mashaka na tamko lao,kwa serikali kuunda tume huru kama siyo kutafuta vyanzo vya posho au ulaji mwingine toka ikulu !
   
Loading...