Baraza la Maaskofu Katoliki watoa tamko kulaani mauaji Kibiti na shambulio kwa Tundu Lissu

Hivi akumbuki bunge na police lilipiga marufuku kuzungumzi hii issue ya kibiti tena mwigulu mpaka akatishia kuwakamata wakina lema waisaidie police sasa watu wangezungumzaje wakati mlisema iwe siri,azori yuko wapi,
Muwe na pasaka njema
 
Huwezi kushindana na maaskofu wa TEC na KKKT; cha msingi si kulumbana nao ila aangalie highlights kwenye waraka zote mbili. Lazima kuna kitu hakipo sawa ila Mkuu hataki ku accept na kurekebisha usukani wa roli letu kabla halijaingia kwenye korongo.
 
Hawezi shindana viongozi wa dini kwani leo walinzi walikuwa wengi kuliko rai wa kawaida na hisi huyu halali pale kivukoni kwani hajiamini kabisa
 
Teh jiwe bana huwa linanichekesha sana kuna sehemu kasema kwanini serikali haikununua hizi ndege miaka 100 iliyopita na Tanzania ilikuwepo

Miaka 100 iliyopita Tanzania ipi ilikuwepo ?

Hapo kwenye waraka wa Maaskofu jiwe kasema hazikilizi yoyote na hayamfanyi chochote huo waraka

Anasema Watanzania bila kujali dini ,kabila wala chama tuwe pamoja wakati huo viongozi wa upinzani wako ndani na wamenyimwa dhamana order ikitoka kwake.

Kumuelewa huyu jamaa inabidi uwe mwendawazimu
 
Kibiti watu wakataka iwe ajenda bungeni mkadai hakuna tishio la usalama tz, waandishi wa habari waliokuwa wanaifuatilia mkawapiga mkwara. Leo mnaona iwe ajenda kwa sababu mmesemwa vibaya. Ukiona kusifiwa kwingi jua kunakukosolewa jirani kunasogelea.
 
Kile alichokisema Mheshimiwa Rais wetu jana kwenye ibada ya misa ya pasaka nadhani kilikuwa kinatosha kuwa jibu kwa nyaraka hizi za maaskofu. Maana alimtuma paroko amfikishie salamu zake kwa maaskofu juu ya kuhubiri amani na maendeleo.

Sasa hiki cha leo kinaonyesha alichosema jana hakuwa amedhamiria ila kutimiza wajibu tu kwa kuwa alikuwa ndani ya jengo la kanisa sasa inabidi apretend kama mkristo safi sasa ametoka yupo nje ya kanisa anasema sasa yaliyoujaza moyo wake. Huu sio ukristo

Bwana amjalie hekima Rais wetu
 
Sasa alitaka Maaskofu wawaandikie waraka Majambazi ya Kibiti au ,wastaafu Mpigeni Gavana huyu Bwana Mkubwa miaka mitatu bado mingi sana atatuumiza huyu
Umeuliza swali zuri sana. Huu waraka angeandikiwa nani? Wauaji huwa wanaandikiwa nyaraka?
 
Mzee wa kutoka nje ya reli kama kawaida yake.

Yaani kama kuna kitu amenyimwa huyu jamaa ni kuwa mtu wa subira.

Yaan kwake kuropoka ni jambo la kawaida sana

Sasa mauaji ya kibiti na kupokea pangaboi vnahusiana nini ?

Ok. Kwa kuwa wakat wa kibiti hakukuwa na waraka so watu waendelee kukaa kimya kuangalia nchi inavyozid kupoteza mwelekeo chini ya utawala wake wa ovyo ovyo.
 
Huwezi kushindana na maaskofu wa TEC na KKKT; cha msingi si kulumbana nao ila aangalie highlights kwenye waraka zote mbili. Lazima kuna kitu hakipo sawa ila Mkuu hataki ku accept na kurekebisha usukani wa roli letu kabla halijaingia kwenye korongo.

Hao Maaskofu wako wangapi??? Maaskofu wenye mtizamo tofauti wako wangapi? Wauumini wanaounga mkono huowaraka wako wangapi? Wasiounga mkono huo waraka wako wangapi? Maaskofu wamekosea mno kutoa ule waraka..wameleta mgawanyiko miongoni mwao na miongoni mwa waumini na ndani ya jamii
 
Ndio maana nimeshauri hawa viongozi wa serikali wanyamaze au watafute meza ya mazungumzo na kada mbalimbali.

Sasa kama ni kweli raisi kayasema hayo,basi hii nchi inahitaji raisi mwenye upeo wa kuona mbali.
Baba askofu Chengula ameshauri watanzania kuwa makini tunapochagua viongozi ili kuepuka hasara ya kitaifa kama hiii inayoendelea kutupata hadi sasa.
 
Back
Top Bottom