Baraza kivuli la CHADEMA ndani ya bunge ni batili halina sura ya muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza kivuli la CHADEMA ndani ya bunge ni batili halina sura ya muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vitendo, Nov 16, 2010.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  16/11/2010

  YAH: BARAZA KIVULI LA CHADEMA NDANI YA BUNGE NI
  BATILI HALINA SURA YA MUUNGANO
  Ndugu
  Waandishi wa habari,

  Napenda kuwaeleza kwamba sura ya baraza kivuli lililoundwa na Chadema ndani ya Bunge la Jamhuri wa Muungano ni batili.

  Limekuwa batili kwa sababu ya kukosa sura ya muundo wa muungano. Shulghuli zote za Bunge la Muungano ni sharti zijenge sura ya Muungano vinginevyo baraza kivuli la Chadema ni baraza kivuli la Tanzania Bara.

  Kwa mantiki hiyo bado kuna nafasi kwa vyama vilivyo baki ambavyo havikuingizwa kwenye baraza kivuli la Chadema kuunda baraza kivuli mbadala litakalokuwa na sura ya muungano.

  Kwa kuwa CUF ndio chama kilichokidhi sifa ya kimungano. Ni vema CUF ikatoa kiongozi wa upinzani bungeni.

  Nachukua nafasi hii kumuomba Mhe: Spika wa Bunge tukufu kutoa maelekezo kuchagua baraza kivuli litakalokuwa na sura ya muungano.

  Ndimi,

  ---------------------------------
  Kom Fahmi Nasoro Dovutwa
  Mwenyekiti-UPDP-(T)
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Duh! Kuna watu wanaijua shari. Aliona kasahaulika anakumbushia
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe si ulitangaza kuunga mkono CCM? Mbona unazungumzia upinzani kwa hoja hafifu? Hakuna sura za muungano pale kuna sheria na kanuni.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Muungano upi?...ambao zanzibar wameuvunja?........mbona muungano hakuna?...mwandishi uko sayari gani au pande zipi za tanganyika?...we unaamini kikwete ni rais wa muungano ambao haupo?...............mnapoteza muda kuzungumzia muungano wakati zanzibar imeshajitenga.....
   
 5. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwani baraza kivuli lililopita lilikuwa na sura ya muungano? Au CUF walijisevia wenyewe tu. Kama ni hivyo kelele za nini wacha CHADEMA nao wapete
   
 6. K

  Kudadadeki Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hauna U- komredi wowote Kaka, you are just another crap from Msanga, Kisarawe.
   
 7. OME123

  OME123 JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,441
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Dovutwa gani huyu yule mamaluki wa ccm au yupi,hauna akili mbuzi weeeeeeeeee
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sitashangaa Spika wa CCM kubadilisha kanuni za bunge ili kukidhi matakwa haya.

  kuna issue nyingi zinatakiwa kujadiliwa mfano zanzibar mtu anakuwa mbunge kwa kupata kura 6,000 Tanzania bara kuna wabunge wamepata ubunge kwa kura 18,000. sijui ndugu Kom Fahmi Nasoro Dovutwa anapendekeza nini kwa spika juu ya hili.

  Je ni sawa uki refelct wapiga kura kusema mbunge mmoja wa tanzania bara ni sawa na wabunge watatu wa Visiwani?
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Weka pressure kwenye kubadili katiba na sio kuwapinga Chadema. Pia, hilo ni tatizo la Wazanzibari kutowachagua Chadema na nafikiri ndio demokrasia yenyewe hiyo!!!!!!
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanza angetoa taarifa ya kukataa serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar kwani imeundwa na vyama viwili tu na hali kuna vyama 19 nchi hii(nirekebishwe kama sipo sahihi).
   
 11. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sijui kwa nini watu wameamua kuwasema chadema sana hapa kwa baraza lao hili,mbona CUF wakati ule wakiwa na kina Lwakatare waliwahi kukaataa kuunda kambi ya upinzani na wenzao wengine? na tena Tambwe hiza amewahi kuohojiwa wakati huo na star tv juu ya msimamo huo wa CUF na aliongea mengi ikiwamo haki yao ya kuunda baraza hilo kwakuwa wao ndio wenye wabunge wengi na wametumiza masharti. Sasa leo kwa nini inaonekana chadema wa kwanza kufanya hivyo?
   
 12. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Fahami Dovutwa uchaguzi umeisha usahau tena vijisenti walivyokuwa wanakupa sisiem wakati wa kurudi kijiweni umewadia.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Of all the people Dovutwa ndo anaandika hayo!
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  hivi uchina na ukubwa wake wanaviti vingapi UN ?
   
 15. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wewe Dovutwa unaweza kuwa sahihi au sio sahihi, ili kuondoa huu utata tupe kifungu cha sheria kinachosema baraza lazima liwe na waziri kutoka Zanzibar.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duuuu muungano upi??? huuu ulioshikwa na Gundi!?? unaohitaji katiba mpya kuufufua??
  mnanichanganya jamani hv kwani hajui kuwa muungano umeshakufa???
  TUUOKOE MUUNGANO WETU KWA KUTENGENEZA KATIBA YETU!
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  hahahahaa!
  Hiyo inamtosha. siongezi neno.
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Orait...kumbe macho yangu bado yanaweza kusoma vizuri.........unamaanisha meeeee, meeeee!
   
 19. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa yako kwa mujibu wa kura za Rais wa Muungano Kikwete hakuchaguliwana wanapiga kura wa Zanzibar. Hivi basi yeye sio rais wa Muungano bali wa Tanzania Bara. Of course hii ni kama kura za Bara nazo zilikuwa sahihi.
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Je katika uchaguzi wa mwaka 2005 wabunge wa CUF walikuwa wanauwiano wa sura ya Muungano? au kwa vile ni CHADEMA mnataka kupindisha mambo?
   
Loading...