Baraza kivuli la CHADEMA ndani ya bunge ni batili halina sura ya muungano

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
16/11/2010

YAH: BARAZA KIVULI LA CHADEMA NDANI YA BUNGE NI
BATILI HALINA SURA YA MUUNGANO
Ndugu
Waandishi wa habari,

Napenda kuwaeleza kwamba sura ya baraza kivuli lililoundwa na Chadema ndani ya Bunge la Jamhuri wa Muungano ni batili.

Limekuwa batili kwa sababu ya kukosa sura ya muundo wa muungano. Shulghuli zote za Bunge la Muungano ni sharti zijenge sura ya Muungano vinginevyo baraza kivuli la Chadema ni baraza kivuli la Tanzania Bara.

Kwa mantiki hiyo bado kuna nafasi kwa vyama vilivyo baki ambavyo havikuingizwa kwenye baraza kivuli la Chadema kuunda baraza kivuli mbadala litakalokuwa na sura ya muungano.

Kwa kuwa CUF ndio chama kilichokidhi sifa ya kimungano. Ni vema CUF ikatoa kiongozi wa upinzani bungeni.

Nachukua nafasi hii kumuomba Mhe: Spika wa Bunge tukufu kutoa maelekezo kuchagua baraza kivuli litakalokuwa na sura ya muungano.

Ndimi,

---------------------------------
Kom Fahmi Nasoro Dovutwa
Mwenyekiti-UPDP-(T)

Wewe naamini akili yako haipo sawa hata waliokupigia kura pia ni wehu, ulishaamua kuunga mkono ccm leo unataka kujadili mambo ya upinzani wewe zuzu nini? Tuache na upinzani wetu nyau wewe.
 
Wakuu hivi mfano Dr. Slaa angekuwa ndiye raisi kwa sasa (which was very likely) na CHADEMA ingekuwa na majority ya wabunge (Lakini wote kutoka Tanzania bara) je wangelazimika kuteua watu kutoka Zanzibar kuwa mawaziri just for the case ya kuweka serikali yenye sura ya muungano? Katiba inazungumzia lolote kuhusu hili? Na je ni mawaziri wangapi wanatakiwa kutoka bara na wangapi kutoka Zanzbar?

All in all hilio pia linaonyesha ni namna gani mapungufu ya muungano wetu yalivyo. Na with the current state of affairs kuna uwezekano wa Mzanzibari kuwa raisi wa muungano miaka ijayo? Maana it's likely too Salim ndiye alikuwa wa mwisho kuwa na karata hiyo.
Chadema iliunga mkono mgombea wa CUF Zanzibar Seif Sharrif Hamad, hivyo nina hakika CUF wangepewa ushindi wao halali na kuongoza visiwani kisha bara napo Dr.Slaa angewapa CUF uongozi wa Jamhuri ya Tanzania kuendea kuundwa kwa serikali tatu. Ndicho wananchi wa Zanzibar wanakitaka na ndicho Chadema wanatakiwa kukitangaza kila siku kwa Wazanzibar ili kesho wananchi hao waikubali Chadema visiwani..
Hizi habari za uhasama na chuki zinajengwa na watu wasiojua siasa na jinsi ya kuwavuta wananchi wapiga kura.
 
Mkuu Nikupateje ahsante kwa kunukuu vifungu ili watu waache kukurupuka bali wasome na waandike vitu vyenye uhakika. Wengi tunaenda kwa mkumbo kwamba kwakuwa wengi wanaona/wanasema hivyo basi ni sahihi. Kukurupuka tu na kuropoka ndo kunaharibu nchi yetu, tangia grassroots hadi viongozi wa juu.
 
Back
Top Bottom