Elections 2010 Baraza jipya la mawaziri

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,558
Kwa kulingana na ilani ya ccm, baraza la mawaziri wa Tanzania litakuwa na mawaziri wasiopungua 47, na kwakuwa huwa wana tabia ya kulipa fadhila, haitatushangaza kusikia hata Mama Salma Kikwete kuwa waziri mojawapo kutokana na kampeni alizokuwa amefanya,
hata Ridhiwani Kikwete naye kupewa nafasi kwa jinsi alivyoendesha kampeni zake.

Baraza litakuwa kama ifuatavyo:

1. Mizengo Pinda/Edward Lowassa - Waziri Mkuu
2. Bernad Membe- Mambo ya Nje
3. Ridhiwan/Masha - Mambo ya Ndani
4. Juma Nkhami/ Mkuchika - Habari na Michezo
5. John Magufuli/Lameck Airo - Uvuvi

Endelezeni..................................
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,228
Tumia angalao ubongo wako kidogo. Nini sifa za mtu kuwa waziri? Ridhiwan/Masha wanaweza kuwa mawaziri? Kwa vigezo gani?
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,558
Tumia angalao ubongo wako kidogo. Nini sifa za mtu kuwa waziri? Ridhiwan/Masha wanaweza kuwa mawaziri? Kwa vigezo gani?

Unafikiri ccm wanaangalia vigezo? Wanaangalia ulichangia kiasi gani kwenye chama. Ndiyo maana wabunge wengi wa ccm wamepita strd 7, mfano Lameck Airo, Livingstone Lusinde, Stephen Ngonyani (maji marefu), Deo Sanga (jah people) nk.
Fikiria kama wabunge wote ni darasa la saba unategemea kuteua mawaziri wa namna gani?
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,558
Nimemsahau jamaa moja ambaye naye atapata promotion ya kuwa waziri. anaitwa GENIUSBRAIN. Hongera mwenzetu.
 
Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,125
Walau Riwadhi na Masha hawezi kuwa mawaziri kwani kikatiba waziri lazima hawe amechaguliwa kwenye jimbo. Au.....
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,228
Unafikiri ccm wanaangalia vigezo? Wanaangalia ulichangia kiasi gani kwenye chama. Ndiyo maana wabunge wengi wa ccm wamepita strd 7, mfano Lameck Airo, Livingstone Lusinde, Stephen Ngonyani (maji marefu), Deo Sanga (jah people) nk.
Fikiria kama wabunge wote ni darasa la saba unategemea kuteua mawaziri wa namna gani?

Wewe unaangalia elimu y darasani? Ok, Mbowe na Sungu elimu yao level gani? Acheni ushabiki. Kuwa waziri lazima uwe mbunge. Sasa huyu salama na ridhiwani ni wabunge?
 
Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,125
Lowassa akichaguliwa Waziri Mkuu watu tutaingia barabarani. Hapo lazima atakufa mtu. Hiyo itakuwa kuwafanya Watanzania mbumbu sana. Ikiwa hivyo atakuwa anaandaliwa kuwa Rais 2015
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,144
3,189
Walau Riwadhi na Masha hawezi kuwa mawaziri kwani kikatiba waziri lazima hawe amechaguliwa kwenye jimbo. Au.....

Siyo kweli kwamba lazima awe amechaguliwa. Kwani Mwangunga au Sophia Simba walikuwa wamechaguliwa katika majimbo gani?
 
Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
1,642
Tumia angalao ubongo wako kidogo. Nini sifa za mtu kuwa waziri? Ridhiwan/Masha wanaweza kuwa mawaziri? Kwa vigezo gani?

Nadhani emt yuko sawa. Kwani Meghji, Mahiza etc. walipataje uwaziri? Katiba si inasema anaweza akateua wabunge 10 akitaka?
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
306
Unafikiri ccm wanaangalia vigezo? Wanaangalia ulichangia kiasi gani kwenye chama. Ndiyo maana wabunge wengi wa ccm wamepita strd 7, mfano Lameck Airo, Livingstone Lusinde, Stephen Ngonyani (maji marefu), Deo Sanga (jah people) nk.
Fikiria kama wabunge wote ni darasa la saba unategemea kuteua mawaziri wa namna gani?

Wewe pilipili usiyo ila inakuwashia nini ? Hili ni baraza la mawaziri wa wanaotoka na ccm wewe panga lako la chadema, au ndio unomba cheo kwa JK hivyo pole pole. Mbona mgombea mwenza wa Slaa alikuwa darasa la saba?. Kweli nchii hii ni ya kuwa na M/Rais wa darasa la 7, kweli mmewadharau kweli watanzania, Mungu awasamehe bure.
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,228
Nadhani emt yuko sawa. Kwani Meghji, Mahiza etc. walipataje uwaziri? Katiba si inasema anaweza akateua wabunge 10 akitaka?

Anaweza kuteua lakini tayari kafanya hivyo? Au tunadakia mambo tuu? Tusubiri basi tuone kama atateua mkewe na mtoto wake kuwa wabunge halafu awape pia na uwaziri.
 
DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,309
294
Unafikiri ccm wanaangalia vigezo? Wanaangalia ulichangia kiasi gani kwenye chama. Ndiyo maana wabunge wengi wa ccm wamepita strd 7, mfano Lameck Airo, Livingstone Lusinde, Stephen Ngonyani (maji marefu), Deo Sanga (jah people) nk.
Fikiria kama wabunge wote ni darasa la saba unategemea kuteua mawaziri wa namna gani?

Dah! Kweli nyani haoni kundule.... Umemsahau mgombea mwenza wa Dr. Slaa, Wilbrod Peter (PHD) ni darasa la saba? Be careful not to throw stones when you live in a glaa house!!!
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,228
Wewe pilipili usiyo ila inakuwashia nini ? Hili ni baraza la mawaziri wa wanaotoka na ccm wewe panga lako la chadema, au ndio unomba cheo kwa JK hivyo pole pole. Mbona mgombea mwenza wa Slaa alikuwa darasa la saba?. Kweli nchii hii ni ya kuwa na M/Rais wa darasa la 7, kweli mmewadharau kweli watanzania, Mungu awasamehe bure.

GeniusBrain heri umemwambia. Mgombea mwenza alikuwa darasa la saba which means kama slaa angeshinda tungekuwa na makamu wa rais ambaye hajaenda shule. Kwangu sioni ubaya wowote lakini Mungi anaona ubaya wa wabunge kuwa na elimu ya darasa la saba. Kwani hao mafisadi wana elimu gani? Inabidi tuwe objective sometimes. Tuko too subjective.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom