Baraza Jipya la Mawaziri matarajio ya wananchi na Taifa kwa Ujumla.

Kibori

Member
Jul 21, 2009
72
10
Kwanza kabisa, Mawaziri watakaofukuzwa kwa usifadi uliofanyaki katika wizara zao, ni maoni ya wananchi kwamba watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo ili pia mawaziri watendewe haki inayostahili kwani wakiachwa wananchi wataendelea kuwahukumu pengine pasi sawa au ukweli kamilifu. Taifa lijenge hulka ya kuwapeleka Mahakamani wale wanaoshindwa kusimamia ofisi za umma ipasavyo ili pia ukweli ujulikana kwa uhakika.

Baada ya utangulizi huo haya ni mapendekezo ya baraza jipya la mawaziri rais anategemewa kufanya uteuzi stahiki kama ifuatavyo.


Wizara ya Fedha - Abdallah Kigoda

Wizara Africa ya Mashariki -Bernald Membe

Wizara ya Maliasili na Utalii- James Lembeli


Wizara ya Nishati na Madini- Kafumu


Niabu Wizara ya Nishati na Madini- January Makamba

Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa- Asha Rose Migiro

Wizara ya Viwanda - Prof. Tibaijuka

Naibu Waziri Viwanda - Filikunjombe

Wizara ya Sheria - Dr. Harison Mwakiembe

Wizara TAMISEMI- Mzee Samweli Sita

Wizara ya Ardhi- Mzee Magufuli

Wizara ya Uchukuzi - Ole Meedeye

Wizara Miundo mbinu - Selina Kombani

Wizara ya Afya- Agrey Mwanri



Utafiti unaendelea kupata maoni ya watu.....


Karibuni kwa Maoni Jamani
 
Tatizo la msingi ni kutokuwa na system inayowawajibisha wababaishaji na mafisadi kwa kisingizio cha siasa, kama criminal offenses za uizi na corruptions zingekuwa zinakuwa dealt accordingly tusingejali sana nani yuko wapi. Hivo hiyo false hope za kutaja list ya watu bila kudili na mzizi wa tatizo is just another waste of time.
 
Acha mambo hayo, umewapima hao kwa lipi au kwa upendezaji wa majina yao?
 
Kafumu kuwa waziri wa nishati na madini ni hatari ndiye aliyetoa vibali vinavyotusumbua leo hii bad idea kuwa waziri
 
Da Tibaijuka Utalii, Mwakyembe Trans, Goodluck EA, 6 Land, Membe Viwanda, Rose Int,
 
mawaziri wetu wasiwe wabunge...maana mfumo wa sasa hivi watu wengi wanakimbilia ubunge sio kuwasaidia wananchi wa majimbo yao bali ni kwa kua wengine wanakua tayari wameshaahidiwa kupewa uwaziri. Mbunge awe ni mbunge anasimamia shughuli za serikali na Rais achague mawaziri ambao sio wabunge but watapitishwa na bunge
 
Kwa ujumla CCM hakuna kitu wote wezi tu! Kafumu kaupata ubunge kwa wizi, zao la dhambi na matunda yake ni dhambi tu!
 
Sawa ndugu unamuacha celina kombani ktk baraza la mawaziri kwa lipi alilotusaidia watz? Nipe hoja kunjufu ya jakaya kumbakisha huyu mama na kumtosa mponda? Maana ni heri ya mponda kuliko celina......hapo umeniuzi sana...magufuli mwacheni apumzike homa zinahitaji mapumziko
 
mawaziri wetu wasiwe wabunge...maana mfumo wa sasa hivi watu wengi wanakimbilia ubunge sio kuwasaidia wananchi wa majimbo yao bali ni kwa kua wengine wanakua tayari wameshaahidiwa kupewa uwaziri. Mbunge awe ni mbunge anasimamia shughuli za serikali na Rais achague mawaziri ambao sio wabunge but watapitishwa na bunge
Hiyo sera ni ya CDM - CCM hawawezi kuitumia wanajua itakavyowabana kweye deal zao za kiwiziwizi
 
Msitegemee kitu positive kutoka kwa JK. Vigezo anavyotumia JK ktk teuzi zake ni; 1. Dini ya mtu 2. Urafiki 3. Undugu 4. Geographical location 5. Uwe mtu wa "yes man".
 
Msitegemee kitu positive kutoka kwa JK. Vigezo anavyotumia JK ktk teuzi zake ni; 1. Dini ya mtu 2. Urafiki 3. Undugu 4. Geographical location 5. Uwe mtu wa "yes man".

Mnyisanzu hapo umesema kweli. Ndiyo maana atakamtoa Maige atamweka Lembeli on the basis of geographical location rather than merit. Mpaka tutakapopata katiba bora na viongozi bora ndipo tutakapoelewa kwa nini Tanzania ilidumaa kwa miaka 50 mpaka na kuwa na amani, maliasili nyingi na watu wengi.
 
Hata kama atabadili Baraza, hii ni x ya ngapi? X chache kuona yai safi ndani ya kapu ambalo mayai yalivunjika. Yote siyo masafi hata aliyeshika kapu naye atakuwa ananuka!


Kubwa zaidi, wabadhilifu watafanywaje?
 
Back
Top Bottom