Umenena ipasavyo!...Leo hii taifa hili haliheshimiwi tena; hata majirani zetu ambao walikuwa wanachukulia maneno yetu kwa uzito hawafanyi hivyo tena. Hatukurogwa ila ni kutokana na maamuzi yetu sisi wenyewe.
Ni kweli tumechagua wenyewe kutoheshimiwa maana hadi hivi sasa sijasikia hatua zozote zilizochukuliwa na Foreign Affairs ministry kwenye suala hili, inaonekana wanaona hayo marusi ni stahili yetuZamani zile mataifa makubwa yalikuwa yanasikiliza sana maneno yanayotoka Tanzania na kuyachukulia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo maana kwa nyakati tofauti, mawaziri wa nje wa nchi kubwa kama Henry Kissinger na Edward Heath walimfuata Nyerere, tena Butiama kukiwa hakuna lami. Leo hii sidhani kama kweli wanaweza kufanya hivyo. China iliingia kwenye security council ya Umoja wa mataifa kwa sehemu kubwa kutokana na msukumo wa Tanzania ambayo wakati huo ilikuwa inajengewa reli ya Uhuru. Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya uchumi kwa afrika ya Kusini na Rhodesia yalitokana na mskumu wa Tanzania wakati huo ikiwa mwenyekiti wa Frontline States. Isralei yenyewe ikiwa na kumbukumbu nzuri, itakumbuka kuwa iliwahi kulaaniwa na Umoja wa Mataifa kutokana na msukumo wa Tanzania kama sehemu ya kupinga Ubaguzi wa Rangi huko Afrika ya Kusini na Rhodesia, Ukoloni wa Kireno huko Mzambiki na Angola na Ubaguzi wa Zionism uliokuwa unafanywa na Wayahudi dhidi ya wapalestina.
Leo hii taifa hili haliheshimiwi tena; hata majirani zetu ambao walikuwa wanachukulia maneno yetu kwa uzito hawafanyi hivyo tena. Hatukurogwa ila ni kutokana na maamuzi yetu sisi wenyewe.
Haya ndio maneno yanayowafanya viongozi wetu wajione na wao ni viongozi kumbe ni vilaza. Tumezoea kusikia maneno matamu kutoka kwa Mwakilishi wa Jumuiya Ya Ulaya kwa kuwa anafanya unafiki huo kwa maslahi ya waliomtuma atusifie kutwa kucha ili wao waendelee kupewa migodi yetu."Tanzania is the largest country in East Africa, rich in natural resources, with a population of some 46 million peace seeking people and a gross domestic product of more than 58 billion dollars.
Acha kupotosha mkuu kasome tena! Hajailinganisha Tanzania na Tripolitania.... Amewalinganisha na wale wababe wa Ulaya kaona hamjai hata kwenye kikombe!! Uongo?!Ila inauma sana! Tanzania kulinganishwa Tripolitania! Kajimbo ndani ya Libya! Au Mauritania. Ila nadhani Ehud Barak atakuwa MDINI! Kwa hiyo,hiyo suffix ....NIA..... anadhani ni nchi za Kiislamu! Asijifanye kateleza! Rungu alilonalo Membe akalitoe stoo amtandike laivu kama alivyomtandika balozi wa Libya!