Barak unfazed by criticism from Tanzania

huyu barak aache dharau za kijinga kwani hata wao hawana msaada wowote kwetu.huwezi ukalinganisha umuhimu wa US,UK,SCANDINAVIAN COUNTRIES,CHINA kwa Tanzania ukilinganisha na Israel hivyo kama vipi watupotee tu na hatuwahitaji.Ngoja tuanze kuwaita Iran waje wavune Uraniaum ndo watajua umuhimu wetu kwao.

kweli eudi aache kashfa.

hivi siku kiongozi wa tanzania wa ngazi sawa na eudi akisimama na kuikana "holocaust" huyo eudi na taifa lake
watanyamaza na kusema kwamba hawajali kwa sababu kiongozi huyo ni wa nchi "irrelevant"? eudi amepotoka.

je kama myhem anavyosema, tanzania ikiwaalika wairani waje "kuvuna" uranium tuliyonayo, kweli huyo eudi
atakaa kimya kwa vile tanzania ni "irrelevant"? kweli eudi amepotoka.

eudi amepotoka zaidi katika nyanja ya kidiplomasia, kwani kiongozi wa ngazi yake anatakiwa awe makini
katika lugha anayotumia na mifano anayoitoa kuhusiana na nchi nyingine. nasema eudi amepotoka.

katu siwezi kufurahia nchi yangu kudharauliwa hata kama nina "issues" na watawala wa nchi yangu. eudi, amepotoka, amepotoka, amepotoka .... dah!
 
You can be respected yet be irrelevant. Does it take a platoon of brainiacs in the country to having to figure this out??!! Tumejifedhehesha siye wenyewe kutaka ufafanuzi wa kauli yake ya awali!!
 
Zamani zile mataifa makubwa yalikuwa yanasikiliza sana maneno yanayotoka Tanzania na kuyachukulia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo maana kwa nyakati tofauti, mawaziri wa nje wa nchi kubwa kama Henry Kissinger na Edward Heath walimfuata Nyerere, tena Butiama kukiwa hakuna lami. Leo hii sidhani kama kweli wanaweza kufanya hivyo. China iliingia kwenye security council ya Umoja wa mataifa kwa sehemu kubwa kutokana na msukumo wa Tanzania ambayo wakati huo ilikuwa inajengewa reli ya Uhuru. Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya uchumi kwa afrika ya Kusini na Rhodesia yalitokana na mskumu wa Tanzania wakati huo ikiwa mwenyekiti wa Frontline States. Isralei yenyewe ikiwa na kumbukumbu nzuri, itakumbuka kuwa iliwahi kulaaniwa na Umoja wa Mataifa kutokana na msukumo wa Tanzania kama sehemu ya kupinga Ubaguzi wa Rangi huko Afrika ya Kusini na Rhodesia, Ukoloni wa Kireno huko Mzambiki na Angola na Ubaguzi wa Zionism uliokuwa unafanywa na Wayahudi dhidi ya wapalestina.


Leo hii taifa hili haliheshimiwi tena; hata majirani zetu ambao walikuwa wanachukulia maneno yetu kwa uzito hawafanyi hivyo tena. Hatukurogwa ila ni kutokana na maamuzi yetu sisi wenyewe.

I love this"
 
halafu waziri membe anajigamba kwamba tunaheshimika sana nje! Ukweli heshima tulikuwa nayo enzi zile sio sasa wakati huu ambapo hata viongozi wakuu wa afrika mashariki wamesusia sherehe za uhuru wa miaka 50. Hata libya nao wameamua kutupuuza labda mkapa muhamar gadhafi atakaporudi tena!

wazee tunaheshimika nje kwa kuwa ombaomba duniani. Ni wazi hatuna viongozi makini. Resources zetu wanagawa na sasa tunahaibishwa na israel. Ni aibu kwa membe na jk wake. Ndiyo maana mimi napendekeza jk apumnzike hata sasa, kwani ameshatimiza ndoto yake ya kuwa rais amemaliza. Aachie ngazi tutafute mwenye vision aijenge mpya tanzania.

Nafahamu kuna watu watasema ohoo katiba hairuhusu na ni uhaini kumtaka rais ajiuzulu kabla ya wkt wake; hapa suala si katiba wala uhaini, suala hapa ni kwamba unaendelea kuwa rais kwa ktaka kuwafanyia nini watanzania? Mimi nawaambia ipo siku mtakuja sema; kufikia mwaka 2015 tanzania itakuwa na hali mbaya sana kiuchumi na reputation ya nchi yetu duniani. Ukweli uko wazi kwamba hatuna rais anayefahamu ni kwanini yeye ni rais. Nitamwona mzalendo sana na mwenye kuipenda nchi yake kama ataamua kuwasidia watanzania ili wapate mtu atakayewasaidia kuvusha uchumi wetu. Hali itazidi kuwa mbaya sana, kwani mapema mwakani bei ya umeme nayo inapanda, je wawekezaji itakuwaje? Je nini hatima ya wazalishaji wadogowadogo? Je sekta binafsi ikiwa hoi unategemea nini kwenye uchumi wa nchi? Je bei ya bidhaa itakuwaje wkt gharama ya uzalishaji itakuwa imepanda?

Ni hakika tunapoelekea hali ni mbaya zaidi kwa watanzania waliowengi.
 
Hawa jamaa ingekuwa enzi zile za "masikini jeuri" balozi wa Israel nchini Tanzania kwa sasa angekuwa uwanja wa ndege akirudi nyumbani....

Pia hata yule Muhubiri wa injiri ambaye upamba mandhari ya pale anapohubiria kwa bendera ya Israel nadhani angekuwa ameisha acha kuitumia bendera hiyo.
 
Halafu hawa hawa Waisrael ndio baadhi ya Watanzania wanawapapatikia kuwa ni "taifa la mungu". bs.

Mheshimiwa Kiranga, mtu akisema ukweli, haimwondolei status au nasaba yake. Anabakia kuwa alivyo hata kama alichokisema hakipokelewi au haikeleweki. Nchi yetu imekosa mwelekeo, hatujielewi sisi ni nani na lengo/dira kama taifa ni nini. Tumekuwa kama mbuzi waliofunguliwa wenda malishoni kila mtu atimka kivyake na kwa mwelekeo autakao. Nafasi yetu kwenye international arena imeshachuja, we no longer hold water and nobody takes us serious!
 
Mheshimiwa Kiranga, mtu akisema ukweli, haimwondolei status au nasaba yake. Anabakia kuwa alivyo hata kama alichokisema hakipokelewi au haikeleweki. Nchi yetu imekosa mwelekeo, hatujielewi sisi ni nani na lengo/dira kama taifa ni nini.

Ukweli unauma! Lol
 
hii kitu imeniuma utafikiri mimi ndio rais wa nchi..ndio hatulingani na england lakini ningekuwa rais ningemrudisha balozi wangu
 
Mheshimiwa Kiranga, mtu akisema ukweli, haimwondolei status au nasaba yake. Anabakia kuwa alivyo hata kama alichokisema hakipokelewi au haikeleweki. Nchi yetu imekosa mwelekeo, hatujielewi sisi ni nani na lengo/dira kama taifa ni nini. Tumekuwa kama mbuzi waliofunguliwa wenda malishoni kila mtu atimka kivyake na kwa mwelekeo autakao. Nafasi yetu kwenye international arena imeshachuja, we no longer hold water and nobody takes us serious!

Sijasema kwamba hajasema ukweli, nasema kuna Watanzania wengine wana wa idolize WaIsraeli hawa hawa.

Kuna ukweli mwingine una cost diplomatically needlessly. Huyu waziri hakuhitaji kutaja nchi ili kusema kwamba kuna nchi duniani ambazo hazina umunimu kama wa Uingereza na Ujerumani, kwa kutaka mbwembwe akataka kutaja nchi zinazo rhyme na Uingereza katika Hebrew.

Hii diplomatic brouhaha nzima imetokana na kutaka kutuonyesha yeye MC! Stupid cow.
 
kuanzia leo mimi nipo upande wa palestina na mkiendelea kusema kuwa ati israeli ni taifa la mungu basi mimi nawaambia kuwa mungu ha exist
 
Heheheee unakumbuka kumbe eeh?

Halafu mbona umeadimika sana? Boksi nini?

Nipo kila siku hapa kama lurker...
Ila hata wewe unakumbukumbu sana, mara nyingi posti zako hukumbushia mambo ya zamani kwahiyo nilipoliona bandiko lako nikacheka sana. Boksi kama kawa mkuu.
 
kuanzia leo mimi nipo upande wa palestina na mkiendelea kusema kuwa ati israeli ni taifa la mungu basi mimi nawaambia kuwa mungu ha exist

Sio wewe tu, longtime nchi yetu ipo upande wa Palestina lakini bado hatuna impact yoyote ya kubadili reality on ground, so hawahitaji ata kujua tupo upande gani kwani hatuna uwezo wa kubadilisha chochote...
 
Sio wewe tu, longtime nchi yetu ipo upande wa Palestina lakini bado hatuna impact yoyote ya kubadili reality on ground, so hawahitaji ata kujua tupo upande gani kwani hatuna uwezo wa kubadilisha chochote...

kwa hili lililotokea inabidi tujionyeshe kabisa msimamo wetu......badala ya kuwalamba matakkko hawa wamarekani na waingereza na jk naye aache kuomba omba ndio maana ametiwa ddole na waisraeli wanajua kuwa nchi yetu haina kitu kwani ingekuwa na kitu tusingeuwa omba omba .
 
hii kitu imeniuma utafikiri mimi ndio rais wa nchi..ndio hatulingani na england lakini ningekuwa rais ningemrudisha balozi wangu

Utawezaje kurudisha balozi wako toka Israel wakati unategemea Israel wakupe msaada kwa kilimo cha umwagiliaji kwenye nchi yako mwenyewe?

Pia unategemea Israel wakupe magari mawili matatu kwa bei ya kutupa kwa jeshi lako ili uonyeshe raia wako pale uwanja wa taifa kuwa jeshi liko ngangari kupasua mawe kwa vichwa kama Van damme na swazinigga ( Schwarzenegger) lakini yakitokea mafuriko jamaa wanaingia mitini na kuwaachia wavuvi wa Ferry...
:)..
 
Back
Top Bottom