Barak unfazed by criticism from Tanzania

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
ShowImage.ashx

Photo by: Ariel Harmoni / Defense Ministry[h=1][/h]By GIL HOFFMAN
12/27/2011 19:21

[h=2]Refuses to apologize to African country after it protests being called "irrelevant."[/h]

Defense Minister Ehud Barak has declined to apologize to Tanzania, despite a letter from the African country protesting a Barak statement that its representatives in Israel found offensive, a Barak associate said Tuesday.

In an interview with Israel Radio's Ayala Hasson last Thursday, Barak criticized theForeign Ministry for warning that adopting the Palestinian position on how to advance diplomatic talks would make England, France, and Germany irrelevant.

http://www.jpost.com/Features/FrontLines/Article.aspx?id=250635
"Germany, France and England are not Tanzania, Mauritania or Tripolitania [a region in Libya]," said Barak, noting places whose names rhyme with England in Hebrew. "These are very important, very relevant countries and we don't have an interest in increasing tensions with them or making them bitter enemies."

Tanzania's honorary consul in Israel, Kasbian Nuriel Chirich, wrote a letter to ForeignMinister Avigdor Lieberman condemning Barak's remarks and inviting a representative of Israel to visit his country.

In this effort to praise theimportance of key countries in Europe, he chose to put down Tanzania and compare it to a country that doesn't even exist," Chirich wrote. "Tanzania is the largest country in East Africa, rich in natural resources, with a population of some 46 million peace seeking people and a gross domestic product of more than 58 billion dollars.

Chirich noted that Israel andTanzania have had diplomatic, security, and economic relations since Tanzania's independence and that Prime Minister Binyamin Netanyahu has recently met African leaders in an effort to deepen ties with the continent amid the strengthening of Islamic extremism there.

"Tanzania is an important country that Israel should not ignore," Chirich wrote.

Barak's associates said he did not intend to express regret for his statements aboutTanzania, which they said Barak had made on multiple occasions.

"Maintaining relations with England, Germany, and France is indeed more urgent for Israel than with Tanzania, which has less influence from Israel's standpoint," a source close to Barak said.

Ndio ukweli wenyewe. Zamani zile tulijiheshimu na tukaheshimika zamani hizi ule u 'maskini jeuri' hatuna tena....
 
"Umatonya" wa viongozi wetu utatugarimu sana! Ila binafsi natamani Matusi yanapaswa yatoke kila upande pengine tutazinduka na kuchukua hatua!
Mungu Ibariki Tanzania, wabariki na watu wake wafunguke akili, macho na mioyo!
 
Zamani zile mataifa makubwa yalikuwa yanasikiliza sana maneno yanayotoka Tanzania na kuyachukulia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo maana kwa nyakati tofauti, mawaziri wa nje wa nchi kubwa kama Henry Kissinger na Edward Heath walimfuata Nyerere, tena Butiama kukiwa hakuna lami. Leo hii sidhani kama kweli wanaweza kufanya hivyo. China iliingia kwenye security council ya Umoja wa mataifa kwa sehemu kubwa kutokana na msukumo wa Tanzania ambayo wakati huo ilikuwa inajengewa reli ya Uhuru. Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya uchumi kwa afrika ya Kusini na Rhodesia yalitokana na mskumu wa Tanzania wakati huo ikiwa mwenyekiti wa Frontline States. Isralei yenyewe ikiwa na kumbukumbu nzuri, itakumbuka kuwa iliwahi kulaaniwa na Umoja wa Mataifa kutokana na msukumo wa Tanzania kama sehemu ya kupinga Ubaguzi wa Rangi huko Afrika ya Kusini na Rhodesia, Ukoloni wa Kireno huko Mzambiki na Angola na Ubaguzi wa Zionism uliokuwa unafanywa na Wayahudi dhidi ya wapalestina.

Leo hii taifa hili haliheshimiwi tena; hata majirani zetu ambao walikuwa wanachukulia maneno yetu kwa uzito hawafanyi hivyo tena. Hatukurogwa ila ni kutokana na maamuzi yetu sisi wenyewe.
 
Hii fedheha ya mara ya pili tumeitafuta, kwa sababu ilikuwa wazi kuwa Tanzania ni irrelevant kwa Israel unapolinganisha na England na France.

Tumewapa chance ya kutuambia kwa mara ya pili tu
 
Yule Mzee wetu mwenye busara alisema.. Heshima inaletwa kwa kufanya kazi na kuwa na msimamo thabiti na sio kuomba omba misaada na kuwa lege lege!!...

Hawa jamaa ingekuwa enzi zile za "masikini jeuri" balozi wa Israel nchini Tanzania kwa sasa angekuwa uwanja wa ndege akirudi nyumbani....
 
Taifa hili limejishusha lenyewe, tuna watawala (siyo viongozi) wasiojua taifa linahitaji nini, wala hawajui wafanye nini. Tumeshauza uhuru wetu, ushawishi tuliokuwa nao hatujui ulipotelea wapi na hakuna dalili kuwa tunaweza kurudi ktk nafasi tuliyokuwa nayo. Hatuna wa kumlaumu, tujilaumu wenyewe.
 
Ehudi kasema ukweli tu!kwani Tanzania ni England?Sasa tunaumia nini?yeye anaiona Tanzania haifai wengine waiona yafaa.
 
Tunasubiri statement ya Membe. Tunategemea KAULI KALI sawa sawa na alivyomkaripia na kumwagiza Balozi wa Libya kupandisha bendera ya Gadafi haraka badala ya ile ya Serikali ya "waasi".

Mlizoea kuonea vidagaae? Papa hilo sasa, chezeni nalo. Humu ndani napo: Zanizbar ni nchi, Zanzibar sio nchi. Kumbe wenzetu wanatuona mabwege tu - TANZANIA is IRRELEVANT.
 
Zamani zile mataifa makubwa yalikuwa yanasikiliza sana maneno yanayotoka Tanzania na kuyachukulia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo maana kwa nyakati tofauti, mawaziri wa nje wa nchi kubwa kama Henry Kissinger na Edward Heath walimfuata Nyerere, tena Butiama kukiwa hakuna lami. Leo hii sidhani kama kweli wanaweza kufanya hivyo. China iliingia kwenye security council ya Umoja wa mataifa kwa sehemu kubwa kutokana na msukumo wa Tanzania ambayo wakati huo ilikuwa inajengewa reli ya Uhuru. Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya uchumi kwa afrika ya Kusini na Rhodesia yalitokana na mskumu wa Tanzania wakati huo ikiwa mwenyekiti wa Frontline States. Isralei yenyewe ikiwa na kumbukumbu nzuri, itakumbuka kuwa iliwahi kulaaniwa na Umoja wa Mataifa kutokana na msukumo wa Tanzania kama sehemu ya kupinga Ubaguzi wa Rangi huko Afrika ya Kusini na Rhodesia, Ukoloni wa Kireno huko Mzambiki na Angola na Ubaguzi wa Zionism uliokuwa unafanywa na Wayahudi dhidi ya wapalestina.

Leo hii taifa hili haliheshimiwi tena; hata majirani zetu ambao walikuwa wanachukulia maneno yetu kwa uzito hawafanyi hivyo tena. Hatukurogwa ila ni kutokana na maamuzi yetu sisi wenyewe.
Ni kweli tumechagua wenyewe kutoheshimiwa maana hadi hivi sasa sijasikia hatua zozote zilizochukuliwa na Foreign Affairs ministry kwenye suala hili, inaonekana wanaona hayo marusi ni stahili yetu
 
huyu barak aache dharau za kijinga kwani hata wao hawana msaada wowote kwetu.huwezi ukalinganisha umuhimu wa US,UK,SCANDINAVIAN COUNTRIES,CHINA kwa Tanzania ukilinganisha na Israel hivyo kama vipi watupotee tu na hatuwahitaji.Ngoja tuanze kuwaita Iran waje wavune Uraniaum ndo watajua umuhimu wetu kwao.
 
Ila inauma sana! Tanzania kulinganishwa Tripolitania! Kajimbo ndani ya Libya! Au Mauritania. Ila nadhani Ehud Barak atakuwa MDINI! Kwa hiyo,hiyo suffix ....NIA..... anadhani ni nchi za Kiislamu! Asijifanye kateleza! Rungu alilonalo Membe akalitoe stoo amtandike laivu kama alivyomtandika balozi wa Libya!
 
kiukweli nchi zilizotajwa na Ehud ukiziangalia hazilingani hatakidogo kiuchumi, kiuzalendo, kiushawishi na kimaendeleo ya kisayansi sisi tupo nyuma sana sasa tukitaka tusidhalilishwe tena tujipange upya. Lakini kwa sasa ukweli ndio huo kwamba sisi kwa England,France&Germany ni kama sisimizi kwa Tembo( kiuchumi) sio kwa kuangalia eneo la ardhi au idadi ya watu.
 
Halafu Waziri Membe anajigamba kwamba tunaheshimika sana nje! Ukweli heshima tulikuwa nayo enzi zile sio sasa wakati huu ambapo hata Viongozi wakuu wa Afrika Mashariki wamesusia Sherehe za Uhuru wa miaka 50. Hata Libya nao wameamua kutupuuza labda mkapa Muhamar Gadhafi atakaporudi tena!
 
Hivi kwa nini sisi hatupendi kusikia ukweli?

Kwa nini tukiambiwa ukweli tunasema tumetukanwa?
"Tanzania is the largest country in East Africa, rich in natural resources, with a population of some 46 million peace seeking people and a gross domestic product of more than 58 billion dollars.
Haya ndio maneno yanayowafanya viongozi wetu wajione na wao ni viongozi kumbe ni vilaza. Tumezoea kusikia maneno matamu kutoka kwa Mwakilishi wa Jumuiya Ya Ulaya kwa kuwa anafanya unafiki huo kwa maslahi ya waliomtuma atusifie kutwa kucha ili wao waendelee kupewa migodi yetu.

Barak kasema kweli, nyie kama mna mlaani endeleeni mimi simo. Tim Clarke amezoea kutusifia kwa maslahi ya EU hatusemi, anayekamua jipu letu ndio tunamchukia
 
Ila inauma sana! Tanzania kulinganishwa Tripolitania! Kajimbo ndani ya Libya! Au Mauritania. Ila nadhani Ehud Barak atakuwa MDINI! Kwa hiyo,hiyo suffix ....NIA..... anadhani ni nchi za Kiislamu! Asijifanye kateleza! Rungu alilonalo Membe akalitoe stoo amtandike laivu kama alivyomtandika balozi wa Libya!
Acha kupotosha mkuu kasome tena! Hajailinganisha Tanzania na Tripolitania.... Amewalinganisha na wale wababe wa Ulaya kaona hamjai hata kwenye kikombe!! Uongo?!
 
Back
Top Bottom