Barabara ya vivuli vya kifo

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,448
2,289
'Shades of Death Road' yaani barabara ya vivuli vya kifo au babarara yenye vivuli vya kifo. Ni barabara inayopita msituni huko Warren New Jersey US, msitu huu unaitwa Jenny Jump Forest, barabara sio ndefu sana, ina urefu wa km 11 tuu.

Hii ni moja kati ya barabara za hatari zaidi kupita katika maeneo haya, iwe mchana na usiku pia. Huonekana vivuli vikitokea juu na kuvamia watu na kuwakata makoromeo.

Mara nyingi pia ajali nyingi hutokea katika eneo hili, wengine husema hushuhudia maiti zikiwa zimening'inizwa mitini kando ya barabara NK.

Zamani barabara hii ilikuwa ikitumiwa na majambazi ambao walikuwa wakijificha msituni, wanavamia watu wanaopita, wanawauwa na kuwapora vitu walivyonavyo.

Hali hii iliwaogopesha sana watu, baadae wananchi waliwakamata, wakawauwa majambazi hao na kuitundika miili yao juu ya miti kando ya barabara ili iwe fundisho kwa wengine.

Kati ya mwaka 1920 hadi 1930 kulikuwa na mauaji matatu ya kikatili yaliyofanywa kando ya barabara hii.

Moja ilikuwa ni wizi ambapo mtu aligongwa na gari kichwani na kuporwa sarafu za dhahabu, pili ni mwanamke aliyemkata kichwa mumewe na kumzika kichwa na mwili pande tofauti za barabara, na tatu ni mkazi wa eneo hilo Bill Cummins, aliyepigwa risasi na kuzikwa kwenye matope. Uchunguzi wa kesi hizi zote haukuwahi kufanikiwa kamwe.

Hakuna majibu sahihi kama majambazi hawa waliouliwa kikatili wana uhusiano wowote na vivuli hivyo?, au mizimu yao inalipa kisasi?. Miaka ya 1850 barabara hii ikikuwa inaitwa Cat Hollow au Cat Swamp, hii ni kwa sababu kulikuwa na mapaka ya ajabu yaliyokuwa yakiishi mstuni humo!, yalikuwa yanawashambulia wasafiri mara kwa mara na njiani.

Hii ni barabara inayokatiza msituni, msitu huu unaitwa Jenny Jump Forest. Kwanini uitwe kwa jina la mtu, Jenny?

Wakati matukio haya yote ya uporaji yakitokea, kuna mwanamke alikuwa anaitwa Jenny, huyu pia alikuwa ni mmoja wa wahanga waliouliwa na kuporwa vitu vyake katika msitu huu wakati akipita barabarani. Inaelezwa kuwa mzimu wa Jenny bado upo ndani ya msitu huu na ndio maana unaitwa Jenny jump forest.

Source FM facts
IMG_20200108_192838_920.JPG
 
Back
Top Bottom