Barabara ya kifo - World's most dangerous road - Bolivia

Kweli bolivia hiyo ni barabar ya kifo nawavulia kofia, Hapa kwetu zilikuwepo mpaka sasa Kutoka kiwira Mbeya hadi Mbalizi kupitia Igogwe Hospital bado ipo, Makongorosi chunya bado ipo, Morning site Morogoro sehemu bado ipo kuelekea Bondwa kileleni mlima wa morogogo. sehemu moja upareni-Ugweno ipo lakini wa TZ hakuna anaefikiria jinsi ya kuiboresha mpaka sasa miaka 50 ya Uhuru. Milima ya bolivia ni ya bonde la ufa katika milima ya Andes. Mbinu mya wanatoboa milima. kama ilivyo China, Switzaland ,nk
 
Hapa kwetu Tanzania kuna barabara inayofanana na hiyo? Duh, kweli hii hatari.

Mombo - Lushoto, Gonja miamba, Sekenke ya zamani, na kitonga ni baadhi ya barabara zinazofanana kwa mbali na hiyo ila bado hazijaifikia kwa kutisha kwake.

Regards
Chacha
 
it is true this is a death road but i dont understand if a correct minded person can drive on that.Why has it been established overthere instaead somewhere else.Does it mean there was anywhere to introduce the new road.
 
Hii barbara ingewekwa kuwa moja ya maajabu ya dunia. nadhani hata mainjnia walioibuni hii barabara ni kiboko
 
Yaani mie nikifika huko nateremka kwenye basi kwanza kuchimba dawa ili nione mkojo unapodondokea
 
Wakuu wangu hapa kwtu pia ipo. ukienda lushoto kutokea mombo mambo ni hayo hayo. tufanye utalii wa ndani jamani.
kaka kwa hii baranara ya Lushoto ni cha mtoto huenda kidogo naweza kufananisha na ile ya Malawi ukitokea Tanzania kupitia Karonga kwenda Mzuzu ,hapo napo gari likidondoka tu ni moja kwa moja hadi kina cha Lake Nyasa
 
Wakuu wangu hapa kwtu pia ipo. ukienda lushoto kutokea mombo mambo ni hayo hayo. tufanye utalii wa ndani jamani.
kaka kwa hii baranara ya Lushoto ni cha mtoto huenda kidogo naweza kufananisha na ile ya Malawi ukitokea Tanzania kupitia Karonga kwenda Mzuzu ,hapo napo gari likidondoka tu ni moja kwa moja hadi kina cha Lake Nyasa
 
Mi nilidhani barabara yetu ya kupanda Ugweno nayo inatisha kumbe kuna nyingine ni noma especially hiyo ya bolivia. Dah!!

Kupanda hiyo ya bolivia lazima uwe umegonga msuba kidogo au vodka shots!
 
madereva wote wa bongo wanaosababisha ajali waende wakajifunzie udereva upya huko!
 
lushoto mombo napo ukipanda yale mabasi yaendayo huko,njiani unashilia roho mkononi
 

Du! duniani kuna mambo, tembea uone.
Nimeendesha gari Kitonga, Sekenke niliposhinda usiku kucha, Barabara ya Songea Tunduru, Tabora - Chunya - Mbeya kupitia Makongorosi, Lukumburu ya Songea kabla ya lami kujengwa, Njombe - Ludewa, Lakini hii ya Bolivia ni mwisho wa dunia na ni kuzimu ya ahera. Kumaliza mlima salama uwe unateremka au unapanda ni mwujiza wa Mungu. Binafsi ningehamia sehemu nyingine. Ndio maana hawa waspanish wanauwezo wa kuvumilia hali ngumu majuu kuliko waafrika, kumbe hali ndo hii, balaa tupu!
 

weee ukome kabisa mwanangu ..wenzako warusi hapo wanaona kama ni very interesting hao hapo ni kama watalii ... na usijaribu hata siku moja kufananisha barabara za urusi na za bongo hata siku mmoja wale barabara zao ni nzuri sana ...hao hapo ni watu wanafanya tours ..
 
hiyo barabara ya bolivia hunipeleki hata siku moja hata kwa panfga au mkuki bora nitembee kwa mguu... hata baiskeli hapo siendeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…