JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524
Kwa wale tunaoishi karibu na bonde la ufa -Rift valley, hili halitushangazi,kwani haipiti mwezi bila tetemeko la ardhi kutokea.Lakini ni dalili kwamba bara la Afrika linameguka ,tena kwa kasi.
Kwa mujibu wa utafiti unaofanywa na Dr James Hammond katika eneo lililopewa jina la Afar Triangle ambako ardhi imeanza kuzama na kuanza kutengeneza umbo linaloonekana kama maandalizi ya kuibuka kwa bahari itakayolitenganisha na kulipasua bara la Afrika katika mapande mawili. ni dhahiri kuwa muumba wa mbingu na ardhi bado hajamaliza uumbaji.
Kwa mujibu wa utafiti huu pande moja (plate) litazibeba nchi za Afrika mashariki..Tanzania,Kenya,Ethiopia,Somalia ,Uganda ,Rwanda ,Burundi na sehemu ya Msumbiji. Mpasuko huu utapita na kufuata maziwa makuu ya Tanganyika,Nyasa,Kivu,Edward na Albert.
Ingawaje mpasuko huu ni wa milimita chache kwa mwaka lakini mtafiti huyu anasema kasi hii ya kupasuka ni kubwa kuliko sehemu yoyote duniani.
Ila kawatoa hofu waafrika ..kwani mipasuko kama hii huchukua mamilioni ya miaka mpaka kukamlika. Lakini mwenyezi mungu huwa hana ahadi na yeyote. Akitaka litimie basi litatimia hata sasa.. hakuna wa kuzuia.
Giant crack in Africa formed in just days
Scientists are sounding the alarm: the mysterious cracks appear across the planet