Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,725
- 830,789
Ni aina ya bao kwenye soka ambalo hakuna anayetegea kama litafungwa, huja kiaina yake kimtindo na bila kipa kujiandaa au wale walinzi. Mpira hutikisa nyavu na hadhira kulipuka kwa shangwe na kelele za goooooo....!!!!
Hiki ndio kilichotokea wiki iliyopita Pale EL alipokutana uso kwa uso na Magufuli. Wengi hawakutarajia kile alichokifanya Lowassa, kwa tabasamu toka rohoni alimsabahi Magufuli bila chembe ya kinyongo! Katu Magufuli hakulitegemea hili na yeye bila kuficha hisia zake za ndani kabisa akakiita kitendo kile kama ni muujiza.
Ilikuwa ni 'brief moment' iliyoleta impact kubwa sana kisiasa hasa kwa upande wa Lowassa! Kwa kasi ya ajabu ikawa ni mjadala kila mahali lakini kote huko kete ikimwangukia Lowassa. Hamasa ya kumpongeza EL kwa kuonyesha uuungwana mkubwa kiasi kile umeikumba CCM hata kufikia nacho kutoa tamko rasmi la kumpongeza.
Kisiasa hili ni bao la kisigino na si la mkono