VOICE OF MTWARA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 3,137
- 2,267
Nawaleta kwenu wanamuziki hawa wa dansi Banza stone "mwalimu wa waalimu" na Ally Choki mzee wa farasi ili tujue nani ni zaidi ya mwenzake kimuziki. haya tuendelee wadau
Banza Stone hana mpinzani kwa kizazi chake, tatizo hajawahi na hatakaa awahi kujitambua. Choki kinachombeba ni kuithamini kazi yake kwani anaelewa na anatambua hayo ndo maisha yake. Period.
Ali Choki huyo juu na sababu ziko wazi:
- Ametunga nyimbo nyingi kuliko Banza
- Ameonyesha kalama ya uongozi kwa bendi alizofanyia kazi na sasa yuko anamiliki bendi yake
- Ni mtu anayekubalika katika jamii hata nje ya muziki kimatendo
Banza Stone: kwa nyimbo chache alizotoa zilivuma, mfano Mtaji wa Maskini ni moja ya wimbo ninaoupenda mpaka sasa..lakini maisha yanahitaji muendelezo kwani hauli siku moja tu bali unaendelea kuhitaji kula. Mwenzake yuko kwenye muziki mpaka sasa.
Nadhani hukumuelewa Bigbro. Mida mingine mafanikio ya kimaisha yanaweza kuja kutokana na bahati, kujitambua na nidhamu katika kazi na sio akili au kipaji. Banza ana kipaji lakini hajitambui na hana nidhamu na kazi yake ndio maana Choki ana mafanikio kimaisha maana anajitambua na ana nidhamu. Unataka kunambia Haruna Boban au Nidhar Khalfan wana kipaji sana cha mpira kwa kigezo kuwa wamecheza mpaka Swede na Canada na wanamiliki magari ukiwaringanisha na Saidi Nassoro Mwamba "KIZOTA" ambaye mpaka anakufa alikuwa anaishi kwa hawara na hakuwa hata na baiskeli?
nadhani sasa tumefikia makubariano kuwa unaweza kuwa na kipaji kizuri kuliko mwenzio lakini akakupita mafanikio kwa kutojitambua kwako au kutojitunza. Tukirejea kwenyekichwa cha habari kuwa nani ni mkali jibu ni kuwa Banza ni mkali lakini hana mafanikio kama Choki. adios amigoNi kweli kabisa!
Lakini kipaji kinahitaji kutumiwa vema kwa manufaa ya mhusika na jamii yake, kinahitaji kulindwa na kustawishwa. Hapa ndipo wengi uwa tunakwama. Wapo wengi wenye vipaji wanakufa navyo bila hata kujijua. Mwisho wa siku jamii kama jamii tunaangalia matokeo sio kilichoko ndani!