Bank ya CRDB inachosha, Usiamini huduma yao

Bank ya CRDB inachosha, Usiamini huduma yao

CRDB imepanuka sana, ina services nyingi lakini ukiangalia kwa makini hawajawekeza equally kwenye raslimali watu, malalamiko haya sasa yamezidi na yote haya utakuta ni incompetence ya staff wao.
tatizo ni kupeana ajira kwa kujuana kindugu performance zero
 
CRDB badala ya kuboresha huduma zao mbovu...Wanafungua vibranch uchwara vyao kama uyoga wanaviita Microfinance.....hivi vimicrofinance vitakufa kama vile vya Barclays vilivyokufa
Hakika
 
Hiyo ni Bank ya maendeleo vijijini sielewi kwa nini wanang'ang'ana mijini wajikite ktk kilimo ili kieleweke !
Ivi CRDB BANK ipo chini ya serikali au ni Taasisi ya serikali au Taasisi ya binafsi. Na jee ina umiliki gani na wazungu
 
serikali wametoa pesa zao sasa hivi wamefilisika
Haha masiala Aya. Tushituane mapema watu tuanze kutoa pesa tuzikimbize NMB. Maana ishakuwa ishu tena kama ilivyo tukuta kule NBC bank
 
Oooh! Mimi niliumbuka ndani ya ndege nilikuwa nanunua saa duty free. Mhudumu alipoingiza kadi katika machine akanijibu "Sorry Sir, your issuing bank is unavailable. Ikabidi nifungue wallet nitumie Dollar kuficha fedheha.
Mkuu mengineyo sio ya kulaumu bank...hiyo ndege ilikuwa kwenye altitude gani? Maana kuanzia ft 2000 hivi tegemea kupata hilo jibu as network inakuwa hamna
 
Kosa hapa si CRDB ....kamdai card issuer wako yeye ataangalia kwa Visa/master card/citrus au whoever ambaye ndo service provider wako na utapata refund yako bila shida. Ilishanitokea mie wakati nasoma niliporud chuo abroad nikaenda kwa my bank na nimepata hela yangu kiurahisi...only tu ukumbuke tarehe ya transaction. ..
Yamenikuta nimefika TZ nikatumia Debit Visa card ya nje kwenye ATM ya CRDB Mbezi mwisho. Nikiwa katika harakati za kutoa pesa nikiwa nafuata maelekezo ya ATM ilifikia pahala ATM ikaniambia subiri pesa, nikasikia machine ikihesabu several times kisha ilipomaliza ikasema transaction cancelled chukua kadi yako na pesa haikutoka. Nilipokwenda kwenye internet kuangalia salio nikakuta zile pesa zimeshachukuliwa kutoka kwenye account yangu. Hadi naondoka home kurudi kazini sijarudishiwa hizo pesa hadi leo.
 
Mkuu mengineyo sio ya kulaumu bank...hiyo ndege ilikuwa kwenye altitude gani? Maana kuanzia ft 2000 hivi tegemea kupata hilo jibu as network inakuwa hamna
Braza najua unatetea kibarua. ..unadhan hao wahudumu wa ndege n.a. hawakujua Hilo kabla ya kuruhusu atumie card kufanya transaction...kwe mapungufu muwe mnakubali basi
 
Mimi nilitaka kufungua account NBC mbona niliamua kuachana na huo mpango. Wana masharti ya kijinga sana. Una barua na kitambulisho cha mwajiri bado wanataka barua cjui ya mwenyekiti wa mtaa na masharti mengine yasiyo na kichwa wala miguu. Kwa ufupi NBC hovyo kabisa.
 
Kwa iyo Mishahara iliyokuwa inapitia katika CRDB BANK inarudishwa tena kupitia NMB bank [emoji542]. Maana Taasisi nyingi malipo yake yalikuwa NMB bank wakayapeleka CRDB BANK [emoji542]. Sasa wamerudisha tena nmb bank [emoji542]. Duh hii nchi hatari sana
 
crdb ikifika wikiend inabidi uzunguke ATM machine 10 hadi 15 ndo ukute moja yenye pesa na network.
 
crdb ikifika wikiend inabidi uzunguke ATM machine 10 hadi 15 ndo ukute moja yenye pesa na network.
Nashindwa kuelewa hapa. Kama kadi yako ni ya Visa, kwa nini usiende kwenye ATM ya benki ingine ambayo inapokea Visa, badala ya kutafuta ATM ya CRDB?
 
Nashindwa kuelewa hapa. Kama kadi yako ni ya Visa, kwa nini usiende kwenye ATM ya benki ingine ambayo inapokea Visa, badala ya kutafuta ATM ya CRDB?

Mkuu kama crdb ATM inakwambia haina network ( ambalo ndo tatizo kuu wikiend)...ukienda kwenye ATM machine zingine za visa inakwambia haitambui your card issuer, jaribu ujionee.
 
Back
Top Bottom