Bank ya CRDB inachosha, Usiamini huduma yao

Bank ya CRDB inachosha, Usiamini huduma yao

CRDB BANK jaman ni janga sana ktk huduma zao kwa mfano tawi la goigi na tegeta kibaoni hatare utakwazika.tangu 27 mwezi huu mpk wa leo no service kabisa hata uende siku gani. Mm nami nahama sina namna natafta pesa kwa shida n tabu nyingi sana na kutumia pia niteseke ni BIG NO
 
nilipoteza ATM yangu nikapeleka data zangu zote ili wa renew then wakasema watanipigia simu, lkn cha kushangaza mwez wa takribani wa 4 huu nothing.

Nilichukulia dirishan amount yangu iliyobaki nimetelekeza account wala sijui nitaitumia lini tena. waki tengeneza hiyo ATM card wataitumia wenyewe.
 
Equity Bank ipi tena unayoisifia? Equity tawi la Kariakoo, niliomba cheque book ya company account, ni zaidi ya mwaka sijapata.. Unaweza vipi ku operate a company account without a chq book...Kuna wakati tulijadili way forward ya kuimprove banking services Tanzania na wazo moja wapo lilikuwa ni kwa Serikali kuanzisha Bankers Ombudsman!
 
Yamenikuta nimefika TZ nikatumia Debit Visa card ya nje kwenye ATM ya CRDB Mbezi mwisho. Nikiwa katika harakati za kutoa pesa nikiwa nafuata maelekezo ya ATM ilifikia pahala ATM ikaniambia subiri pesa, nikasikia machine ikihesabu several times kisha ilipomaliza ikasema transaction cancelled chukua kadi yako na pesa haikutoka. Nilipokwenda kwenye internet kuangalia salio nikakuta zile pesa zimeshachukuliwa kutoka kwenye account yangu. Hadi naondoka home kurudi kazini sijarudishiwa hizo pesa hadi leo.
Mwanalumango, hio si chochote. Mimi kuna wakati niliingiza kadi katika ATM transaction ikakataliwa na kadi ikatoka bila kuwepo ile chip. Nikawauliza wahudumu wakasema mtambo umenasa ile chip kwa bahati mbaya itabidi utengenezewe nyingine lakini mpaka uwe na fomu ya Polisi kueleza kuharibika kwa kadi yako. Can you imagine?
 
kuna NBC mbagala branch pale kichefuchefu kuna teller mmoja,ukienda pale andaa kupoteza saa nzima unasubiri kudeposit,nilitaka kuhama niingie CRDB kumbe kimeo na huko
 
Mkuu NyaniMzee,

Umesema kweli kabisa, yaani ikifika tu Saa 12 Jioni ni tabu kwelikweli. Utakuja ATM hazina pesa na ukijaribu SIMBANKING wanakuambia wanaboresha mitambo. Kila siku hadithi ni hiyo hiyo.

Halafu wanakiburi ile mbaya, ukiwapigia hata wakati wa kazi wanakuambia tatizo litaisha baada ya muda mfupi, huo muda mfupi unaweza kuwa masaa zaidi ya mawili unasubiri.
 
Mwanalumango, hio si chochote. Mimi kuna wakati niliingiza kadi katika ATM transaction ikakataliwa na kadi ikatoka bila kuwepo ile chip. Nikawauliza wahudumu wakasema mtambo umenasa ile chip kwa bahati mbaya itabidi utengenezewe nyingine lakini mpaka uwe na fomu ya Polisi kueleza kuharibika kwa kadi yako. Can you imagine?
Daa hiyo kali sana, pole kaka, sasa kama ingekuwa ni kadi yangu ingekuwa hatari sana maana ninasafiri all over bila cash nikitegemea kadi tu kila ninapokwenda.
 
kuna NBC mbagala branch pale kichefuchefu kuna teller mmoja,ukienda pale andaa kupoteza saa nzima unasubiri kudeposit,nilitaka kuhama niingie CRDB kumbe kimeo na huko

Aisee kuna siku nilikaa pale baadae akatoka sijui ndio meneja yule eti hakuna sistyem twende nbc taifa (Duce ) saa 1:30 mnawaacha watu wamesimama kwenye foleni? Bira exime
 
Daa hiyo kali sana, pole kaka, sasa kama ingekuwa ni kadi yangu ingekuwa hatari sana maana ninasafiri all over bila cash nikitegemea kadi tu kila ninapokwenda.
Oooh! Mimi niliumbuka ndani ya ndege nilikuwa nanunua saa duty free. Mhudumu alipoingiza kadi katika machine akanijibu "Sorry Sir, your issuing bank is unavailable. Ikabidi nifungue wallet nitumie Dollar kuficha fedheha.
 
Equity Bank ndiyo mpango mzima.
Hamna vile vidada shebeduzi wala wabana pua, kazi kazi mtindo mmoja huduma zote faster, kiukweli wako vizuri.

CRDB usijaribu weekend kutafuta hela through ATM utajuta.
Bank zetu bado sana sijui tatizo ni nini jamani watanzania
Hii bank ni nzuri changamoto yake ni kwenye card zao. nadhani wanazitengeneza kwa material hafifu sana. ukiingiza kwenye ATM haina shida ila ukiingiza kwenye machine za kulipia zinginezo inakataa wanakwambia imechubuka...watu wengi wamesema tatizo ni ubora wa card kwa hiyo huwezi kulipia bila kutoa cash.
 
Asante kwa taarifa hii hope wataisoma na wataifanyia kazi
 
Oooh! Mimi niliumbuka ndani ya ndege nilikuwa nanunua saa duty free. Mhudumu alipoingiza kadi katika machine akanijibu "Sorry Sir, your issuing bank is unavailable. Ikabidi nifungue wallet nitumie Dollar kuficha fedheha.
Ungekuwa na madafu je?
 
Ungekuwa na madafu je?
ningeiacha tu nifanyeje sasa. Wanatutia aibu sana hawa CRDB. Wasije wakaweka branch zao za microfinance kwenye hospital kubwa (kama hawajaweka) itakuwa balaa. Itokee una mgonjwa mahututi anahitaji dawa, pesa iko katika kadi ya ATM na ATM inakuambia " service unavailable. Please try later.
 
Hawa jamaa cjui wanafirisika mana hata mikopo wamesitisha ni mwezi wa tatu sasa.Mimi kurenew kadi na kuipata ilinichukua miezi mitano.Nimeamua kuwahama kabisa
 
Wapendwa wanajamii,

Mimi nimekuwa ni mteja wa CRDB Bank kwa miaka si chini ya 12. Mwanzoni nilijivunia kuwa mteja wa CRDB kwa jinsi walivyokuwa wakiboresha huduma kila mara. Lakini kwa sasa CRDB ni benki ya hovyo kuliko mfano. Usijaribu kuamini kuwa ATM zao zina fedha muda wote utaadhirika! Usijaribu kununua bidhaa kwa kutunia credit card zao utaumbuka.

Usiamini huduma yao ya "Simbanking" utaboreka maana kila mara wanarekebisha mitambo! Siku za weekend ndio balaa kabisa ATM zinaenda " kupumzika Coco beach " hadi weekend ipite hivyo usijisumbue kutafuta pesa Jumamosi au Jumapili. Cha ajabu CRDB ina wafanyakazi wengi tu ambao vitendea kazi vyao ni "Smartphones" na kila muda "wanazichungulia na kuzipangusa" zisichafuke. Shame on you CRDB! Nawapongeza NMB maana wameamua kuwapiku hawa wanaochezea biashara.

Huduma za NMB zinaridhisha ila labda kama wewe una kadi ya CRDB na unataka kuitumia katika ATM za NMB. Kitakachokupata ni kuambukizwa magonjwa ya CRDB ukiwa katika ATM ya NMB. Nimeamua nahama sitaki kuteswa na pesa zangu na nimechoka kuadhirika na kikadi kilichoandikwa CRDB Tembo card na nyingine ya ovyo kuliko wanaita Premium Gold Visa Card. Kazi kwenu mnaoipenda CRDB.

Binafsi CRDB wamenikera kwenye mikopo yao. Wanafanya makato yasiyo eleweka alafu mteja unaambiwa kwa nini hukuwajulisha kwamba kuna tatizo, ukiwaeleza wanakwambia tunashughulikia. Mwezi unaofuata wanakukata tena, ukiuliza unaambiwa wanashughulikia. Sina hamu na hii benki ya kimei.
 
CRDB kwa sasa imepwaya sana, alafu wewe wa EQUITY kibenki caha Kenya nyamaza kabisa, kwa sasa NMB ndo habati ya MUJINI
 
Binafsi CRDB wamenikera kwenye mikopo yao. Wanafanya makato yasiyo eleweka alafu mteja unaambiwa kwa nini hukuwajulisha kwamba kuna tatizo, ukiwaeleza wanakwambia tunashughulikia. Mwezi unaofuata wanakukata tena, ukiuliza unaambiwa wanashughulikia. Sina hamu na hii benki ya kimei.

CRDB imepanuka sana, ina services nyingi lakini ukiangalia kwa makini hawajawekeza equally kwenye raslimali watu, malalamiko haya sasa yamezidi na yote haya utakuta ni incompetence ya staff wao.
 
Back
Top Bottom