Bank M-Connecting the dots...

jmushi1, yawezekana wapo wanaokubaliana na mimi kuwa adui mkubwa wa taifa hili ni CCM; niliamini hivyo, naamini hivyo na nitaendelea kuamini hivyo. Sijui tuko wangapi tulioikataa CCM toka kuasisiwa kwake mwaka 1977 lakini mwasisi wa CCM, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kutambua kosa lake la kuanzisha hili zimwi alisikitika sana. Bahati mbaya ni kwamba wakati huu ukweli unajiweka wazi kwake, hakupata nafasi ya kuongoza mapambano dhidi ya hilo zimwi; zimwi lilimwahi akaaga dunia akihuzunika na kulia kwa uchungu.

Hakuna muujiza utaweza kufanyika kuliokoa hili taifa ikiwa bado iko mikononi mwa CCM na ili Tanzania ijikwamue kutoka lindi la umasikini wa kujitakia, CCM lazima ipigwe vita na kushindwa. Bila hivyo ni kujidanganya. Nchi hii ilijaaliwa kila aina ya neema na hakuna nchi ndani ya bara hili lililokuwa na utajiri wa asili kama Tanzania lakini hivyo hivyo hakuna nchi barani Afrika linaloongozwa na chama kama CCM. Wana CCM wa leo wamezaliwa humo humo, wakalelewa humo humo, wakakulia humo humo, wakakomaa na kufuzu humo humo;

Ukweli mchungu...kila awamu litakuwa ovu kuliko lililotangulia.
 
Huyu Sanjeev Kumar ni raia wa Tanzania?
 
Huyu Sanjeev Kumar ni raia wa Tanzania?
Bank M ilianzishwa mwaka 2006, wakati mambo ya EPA ndo yanaanza! yeye ndiye founder wa bank M! Sasa sijui kama ni rai au la! Chavda yeye naye alitimliwa, pengine hakuwa raia!
 
Samahani mkuu, sentensi ya kwanza, unaamini adui siyo ccm bali ni viongozi au ni error?
 
Hivi hizi scandals kubwa namna hii zilizoiumiza nchi kwa kiwango cha kutisha kwa namna ya kutisha pia ina maana hakuna wa kuja kusafisha hata kama kuna kuogopa wakuu. Nachojua trail ya uhalifu huwa ipo ikifanyiwa uchunguzi wa kipelelezi yote yanakuwa wazi hata kama miaka 50 imepita. Ina maana wanaogopa nchi kutikisika halafu mambo yanaendelea tu. Kweli Tanzania mifumo ya kuilinda kiuchumi haijaweza kutusaidia sana tumesaidiwa kwa kiasi kidogo tu. Kama kuna taarifa zaidi tuzitoe tu. Ni aibu vizazi vinapita kimaskini tu wenye meno wachache wanatafuna na kufaidi na vizazi vyao.
 
Atajiunga na ccm na yote yataisha hayo.
 
Yote haya wakulaumiwa ni ccm kwa maana hao wote walioifisadi na wanaoendelea kuifisadi nchi ni wanachama wao hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…